Utafiti: Plastiki yapatikana ndani ya Samaki

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
Je unapenda kula samaki ?
11.jpg

Ikiwa unapenda Dagaa Pweza,Pelege,Mwatiko, Papa, Kiduwa, Kambale,Tilapia ama samaki wa aiana yeyote yule basi unapaswa kusoma taarifa hii ya utafiti.

Wanasayansi nchini Japan wanasema wamekuta plastiki nyingi ndani ya mwili wa samaki, katika bahari inayozunguka Japan.

Watafiti kutoka chuo cha Kilimo na Teknolojia cha Tokyo, wamekuta chembe chembe za plastiki katika asili mia 80% ya matumbo ya dagaa, waitwao 'anchovies'', waliovuliwa katika bahari iliyoko nje ya Tokyo.
Chembechembe za plastiki, kutokana na mifuko ya plastiki au urembo, zinanyonya kemikali za sumu, ambazo zinaingia ndani ya matumbo ya samaki na ndege.

Plastiki hizo zimepatikana katika samaki wa Marekani, Uingereza, hadi Indonesia, pia katika nyangumi, chaza na ndege wa pwani.

Habari kutoka BBC SWAHILI
 
Hii imetafsiriwa, nikisoma nakosa maana halisi ya habari wenyewe!
Kwamba plastiki kuwa tumboni mwa samaki inasaidia kunyonya sumu, wanashawishi watu wale sana samaki??
 
Back
Top Bottom