Utafiti mpya, umaarufu wa Lowassa washuka, Rais Magufuli apaa

TAFITI GANI HIZI.?!! MLISOMEA WAPI HIVI NYIE?!! NI WAZI MLISOMEA VYUO VISIVYO NA MADAWATI! UTAFITI GANI HUU?!
 
uchaguzi hata ukirudiwa leo nampigia kura lowasa

Hata Akili Zake Mnafanana Hivyo Wenye AKILI Zilizotuzidi Hatutakushangai Ila Kwa Sasa Si Tu Tanzania Bali Hata Dunia Nzima Inatambua Kuwa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ni Ndugu Dr. John Pombe Joseph MAGUFULI. Nimemaliza!
 
Hizo kura zilipigiwa wapi??I doubt na watu kuvunjiwa nyumba???Ngoja tusubiri
 
Cha msingi ni kujua lengo la tafiti hii. Na hitimisho lake. Habari imezungumzia matokeo na si lengo na hitimisho.
 
Lowasa ndie Rais halal... Huyo wa ccm ataanguka kwa aibu Mungu atamshusha kumpisha aliyechaguliwa
Mungu mlinde Rais wetu Lowasa
 
View attachment 322728

Matokeo ya utafiti mpya uliofanywa mapema mwezi huu yanaonyesha kuwa umaarufu wa Rais John Magufuli umeongezeka kufikia asilimia 74.5, akimuacha mbali mpinzani wake wa karibu kwenye Uchaguzi Mkuu, Edward Lowassa.

Magufuli alishinda mbio za urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, akipata asilimia chache kuliko wagombea wengine kutoka CCM, lakini amejiongezea umaarufu kutokana na hatua ambazo amekuwa akichukua tangu alipoapishwa Novemba 5, 2015.

Katika uchaguzi huo, Dk Magufuli alipata kura milioni 8.8 sawa na asilimia 58.47, akifuatiwa na Lowassa aliyepata kura milioni 6.07, sawa na asilimia 39.97.

Lakini utafiti huo uliofanywa na taasisi ya Ms Infotrak Researc and Consultant na Ms Midas Touche East Africa kwa kuwahoji watu 1,200 wenye umri wa zaidi ya miaka 18 katika kanda sita na mikoa 15, unaonyesha kuwa Magufuli ameongeza umaarufu kwa takriban asilimia 20, huku Lowassa akishuka kwa asilimia 20 pia.

Katika utafiti huo, Lowassa anaonekana kushuka hadi asilimia 20.1.

Wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Anna Mghwira aliyepata asilimia 1.1, Hashimu Rungwe (0.4), Fahmi Dovutwa (0.2), Lutalosa Yemba (0.1), Janken Kasambala (0.1) na Machmillan Lyimo aliyepata asilimia 0.0. Asilimia 3.5 ya walioulizwa swali hilo walikataa kujibu.

Vilevile, wananchi walipouliza iwapo Uchaguzi Mkuu ukifanyika leo wangemchagua nani kati ya makada waliojitokea kugombea urais mwaka jana, wengi wamemtaja Magufuli.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba wanawake wengi ndiyo wanamuunga mkono Magufuli ikilinganishwa na wanaume.

Asilimia 77.9 ya wanawake wanasema wapo tayari kumchagua tena kuwa Rais iwapo kutakuwa na uchaguzi mpya, wakati wanaume wanaosema hivyo ni asilimia 71.5 pekee.

Kinyume na ilivyo kwa Magufuli, utafiti umebaini kwamba Lowassa anapendwa zaidi na wanaume huku asilimia 22.6 wakisema wapo tayari kumchagua kuwa rais. Ni asilimia 17.4 ndiyo wametoa maoni kama hayo kwa Magufuli.

Kwa upande wa kanda; Kanda ya Zanzibar ndiyo inayoongoza kwa ‘kumkubali’ Magufuli ikiwa na asilimia 91.6, ikifuatiwa na Kanda ya Kati yenye asilimia 81.6, Kanda ya Kaskazini (77%), Kanda ya Pwani (72.7) na Kanda ya Ziwa asilimia 67.6.

Alipoulizwa kuhusu matokeo ya utafiti huo, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa George Shumbuso alisema kuongezeka kwa umaarufu wa Rais Magufuli kunatokana na utendaji wake kugusa kero za wanyonge.

Alisema Watanzania wengi hata wale waliokuwa wakiunga mkono vyama vya upinzani, wameanza kukubaliana na Magufuli kutokana na namna alivyoweza kufanya mambo makubwa na yenye umuhimu kwa Taifa ndani ya muda mfupi.

“Hakuna Rais aliyefanya mambo makubwa namna hii ndani ya siku 100 ndiyo maana wanyonge wameonekana kumkubali kwa sababu amegusa na kuonyesha wazi nia ya kumaliza changamoto zao,” alisema.

“Hata ikitokea uchaguzi ukafanyika sasa nina uhakika Magufuli atashinda kwa sababu wananchi wamebaini wazi kuwa anachokizungumza ndicho anachomaanisha. Si siasa kama ambavyo imezoeleka kwa wanasiasa wengine.”

Kauli hiyo iliungwa mkono na mwenyekiti wa Tanzania Labour Party na mbunge wa zamani wa Vunjo, Augustine Mrema aliyesema kuwa Watanzania walifanya uchaguzi sahihi kumuweka Magufuli madarakani.

Alisema katika kipindi cha siku 100 kiongozi huyo amefanya miujiza ambayo hakuna Mtanzania ambaye alifikiria kuwa ingeweza kufanyika.
===========================

Huo Utafiti, Ni wa hadaa sana Kama Ule wa Twaweza, Uliopanga kurahisisha CCM Kupora Ushindi. Kwanini Nasema Hivi,

1) Utafiti Huo Ungelikuwa fair kama baada ya siku 100 za Magufuli za kuwa Rais, Angekaa Pembeni, ampishe naye Lowassa awe na siku zake 100 Kisha Kwa Kuwa Variables na Events ni sawa then Unaweza Kuwashindanisha Nani Kafanya Vizuri Katika siku 100 za Urais. Kwa Kuwa Hili haliwezekaani, Wanaofanya Tafiti za Kipumbavu na Kizandiki, Wajitafutie Kazi ya Maana.
2) Hivi Kama silaha pekee uliyonayo ndani ni Panga, Akaja Fisi, Mtoto akukuuliza Tumuue na Nini? Ukasema Panga, Je tunaweza Kuwaahakikishia watu kuwa Ungelichagua Panga iwapo Katika Nyumba yako Ungekua na Vyote Panga na Bunduki?.
Acheni Hadaa, Mtafute Kazi ya Kufanya
 
Waliofanya utafiti huu kwa kipindi hiki inabidi niwashangae tu, ni kama vile wanajifurahisha. Kipindi cha siku mia ni kipindi cha "honeymoon" Huu sio wakati mwafaka wa tathmini. Kwangu mimi, tathmini yenye kubeba uhalisia wa utendaji wa mkuu wa nchi ni ile ambayo ingefanywa baada ya kufikisha miaka miwili na nusu akiwa ofisini.
Mkuu Twaweza umeisahau, kujikomba komba wasisahauliwe
 
Tafiti uchwara hizi..siasa za uchaguzi zimeisha..Rais ni mmoja tu. JPM..lowassa ni mwananchi. mkafanye UTAFITI kwenye shida za Watanzania. tumsaidie mh. Rais.
 
wakati wa kufanya huu utafiti na majukumu ya watu hawa ni lazima ushindi uende kwa Magu. yeye ndiye yuko jukwaani mwenzake yuko benchi
 
Who's Lowassa By The Way?
si yule waziri mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya ufisadi ya Richmond saga? alipoona saga lile litamkalia kooni akaamua kukimbilia kujiuzuru harakaharaka kabla kamati ya bunge haijatoa mapendekezo ya hatua za kumchukulia. ana bahati? ?
 
Propanda za kipunguani zilizopitwa na wakati

Siasa ni matukio

Umaarufu wa mwanasiasa yoyote siyo smooth.Bali una badilika kutokana na matukio

Tofauti na wanamziki

Lowassa umaarufu wake uliporomoka vibaya sana baada ya kashfa nzito ya Richmond

Watu tukamsahau

Lakini umati aliokuwa anaujaza 2015 ulitokea wapi?

Lowassa anajua kujipanga
Hakurupuki

Na mapungufu anayoyaonyesha 'Mr.I am politicians' ndiyo yatakayo ongeza umaarufu wa Lowassa Let alone juhudi zake binafsi!
unataka kusema hujui umati ule ulikuwa ukitengenezwaje kamanda ?
 
View attachment 322728

Matokeo ya utafiti mpya uliofanywa mapema mwezi huu yanaonyesha kuwa umaarufu wa Rais John Magufuli umeongezeka kufikia asilimia 74.5, akimuacha mbali mpinzani wake wa karibu kwenye Uchaguzi Mkuu, Edward Lowassa.

Magufuli alishinda mbio za urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, akipata asilimia chache kuliko wagombea wengine kutoka CCM, lakini amejiongezea umaarufu kutokana na hatua ambazo amekuwa akichukua tangu alipoapishwa Novemba 5, 2015.

Katika uchaguzi huo, Dk Magufuli alipata kura milioni 8.8 sawa na asilimia 58.47, akifuatiwa na Lowassa aliyepata kura milioni 6.07, sawa na asilimia 39.97.

Lakini utafiti huo uliofanywa na taasisi ya Ms Infotrak Researc and Consultant na Ms Midas Touche East Africa kwa kuwahoji watu 1,200 wenye umri wa zaidi ya miaka 18 katika kanda sita na mikoa 15, unaonyesha kuwa Magufuli ameongeza umaarufu kwa takriban asilimia 20, huku Lowassa akishuka kwa asilimia 20 pia.

Katika utafiti huo, Lowassa anaonekana kushuka hadi asilimia 20.1.

Wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Anna Mghwira aliyepata asilimia 1.1, Hashimu Rungwe (0.4), Fahmi Dovutwa (0.2), Lutalosa Yemba (0.1), Janken Kasambala (0.1) na Machmillan Lyimo aliyepata asilimia 0.0. Asilimia 3.5 ya walioulizwa swali hilo walikataa kujibu.

Vilevile, wananchi walipouliza iwapo Uchaguzi Mkuu ukifanyika leo wangemchagua nani kati ya makada waliojitokea kugombea urais mwaka jana, wengi wamemtaja Magufuli.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba wanawake wengi ndiyo wanamuunga mkono Magufuli ikilinganishwa na wanaume.

Asilimia 77.9 ya wanawake wanasema wapo tayari kumchagua tena kuwa Rais iwapo kutakuwa na uchaguzi mpya, wakati wanaume wanaosema hivyo ni asilimia 71.5 pekee.

Kinyume na ilivyo kwa Magufuli, utafiti umebaini kwamba Lowassa anapendwa zaidi na wanaume huku asilimia 22.6 wakisema wapo tayari kumchagua kuwa rais. Ni asilimia 17.4 ndiyo wametoa maoni kama hayo kwa Magufuli.

Kwa upande wa kanda; Kanda ya Zanzibar ndiyo inayoongoza kwa ‘kumkubali’ Magufuli ikiwa na asilimia 91.6, ikifuatiwa na Kanda ya Kati yenye asilimia 81.6, Kanda ya Kaskazini (77%), Kanda ya Pwani (72.7) na Kanda ya Ziwa asilimia 67.6.

Alipoulizwa kuhusu matokeo ya utafiti huo, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa George Shumbuso alisema kuongezeka kwa umaarufu wa Rais Magufuli kunatokana na utendaji wake kugusa kero za wanyonge.

Alisema Watanzania wengi hata wale waliokuwa wakiunga mkono vyama vya upinzani, wameanza kukubaliana na Magufuli kutokana na namna alivyoweza kufanya mambo makubwa na yenye umuhimu kwa Taifa ndani ya muda mfupi.

“Hakuna Rais aliyefanya mambo makubwa namna hii ndani ya siku 100 ndiyo maana wanyonge wameonekana kumkubali kwa sababu amegusa na kuonyesha wazi nia ya kumaliza changamoto zao,” alisema.

“Hata ikitokea uchaguzi ukafanyika sasa nina uhakika Magufuli atashinda kwa sababu wananchi wamebaini wazi kuwa anachokizungumza ndicho anachomaanisha. Si siasa kama ambavyo imezoeleka kwa wanasiasa wengine.”

Kauli hiyo iliungwa mkono na mwenyekiti wa Tanzania Labour Party na mbunge wa zamani wa Vunjo, Augustine Mrema aliyesema kuwa Watanzania walifanya uchaguzi sahihi kumuweka Magufuli madarakani.

Alisema katika kipindi cha siku 100 kiongozi huyo amefanya miujiza ambayo hakuna Mtanzania ambaye alifikiria kuwa ingeweza kufanyika.
===========================
Cheap politics
 
ni yule Waziri mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya Richmond. sio waziri mkuu mstaafu ??, ni aliyejiuzuru kwa kashfa. we should make this clear always
Kwanini hamkumshitaki mahakamani nyie lumumbaz...mburulaz wa buku 7 ?
 
Back
Top Bottom