VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Ni utafiti wangu binafsi.Hapa ni sehemu ya kwanza kuuwakilisha.Ni hivi:ujumbe mfupi wa maneno wa simu za viganjani almaarufu kama 'sms' kwa kiasi kikubwa unachangia kudumaza elimu Tanzania. Hii ni kwasababu,wanafunzi wa Shule na Vyuo ambao hutumia simu za vikanjani kwa kutuma ujumbe,hulemazwa na uandishi wa kifupikifupi katika ujumbe na kujikuta wakiandika kifupi hata kwenye mitihani yao.
Katika utafiti huu,nilifanya mahojiano na maafisa mbalimbali wa Baraza la Taifa la Mitihani,Walimu na Wahadhiri pamoja na Wanafunzi wenyewe. Hoja ya msingi ni juu ya jinsi majibu ya mitihani yanavyoathiriwa na uandishi wa sms. Wengi wa Maafisa,Walimu na Wahadhiri wamekiri kuwepo na kukua kwa tatizo hilo na kudai kuwa majibu ya wanafunzi na wanavyuo hayaeleweki kwa kuwa yanaandikwa 'kihuni'. Wakatoa mfano wa sentensi kama 'Tanzania is a democratic country' ambapo wanafunzi huandika 'Tz z a dmcrtic cntry'.
Wanafunzi nao wamekiri kwa wingi wao kuwa sms hulemaza na kuwaharibia majibu katika mitihani waifanyayo. Wanafunzi hao wakawaasa wenzao na wengine kujenga utaratibu wa kuandika kwa kirefu sms zao ili wasije kulemaa katika uandishi hata wa mambo muhimu ya kimtihani.
Katika utafiti huo,nimewahoji Maafisa 11,Walimu 20,Wahadhiri 20 na Wanafunzi wa Shule na Vyuo 45. Niliuanza 2011 na kuukamilisha 2012. Nitauweka katika mtindo wa ripoti hivi karibuni. Asanteni Wakuu...