Utafiti: Je mafuta ya taa hupunguza hamu ya ngono?

cDNA

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
353
348
UTANGULIZI

Mafuta ya taa ni distillate ya mafuta ya petroli ghafi. Matumizi ya mafuta ya taa ghafi katika vyakula vya shule za bweni imekuwa jambo la kawaida katika Afrika Mashariki na nchi nyingine kwa miaka mingi, na imani iliyojengeka ni kuwa yanasaidia kupunguza hamu ya kufanya ngono (libido) kwa wanafunzi walio katika kipindi kigumu mno cha kubalehe (kupevuka). Katika milo yao ya shule za bweni, wanafunzi wamekuwa wakiwekewa dozi za mafuta ya taa kama sehemu ya vyakula pasi na utashi wao.

Ktk mchakato wa kubalehe baadhi ya homoni maalum hutolewa ambazo kimsingi ndizo huibua mabadiliko ya kimaumbile (secondary sexual characteristics) ili kuwawezesha vijana kuwa na uwezo wa kusababisha/kushika mimba (kuzaliana). Moja ya homoni hizo ni testosteron ambayo husababisha kuongezeka kwa ari ya kufanya ngono, upanuzi wa viungo vya uzazi kama vile uume na korodani, uzalishaji wa mbegu za kiume, ongezeko la misuli n.k. (kwa wavulana).

Mbali ya kuwa ufanisi wa mafuta ya taa katika kupunguza ari ya sexual intercouse haujawahi kuthibitishwa kisayansi na wala uchunguzi wa madhara katika mwilini haujafanyika lakini yameendelea kutumika mashuleni.

Utafiti ulioundwa Kenya kufuatilia athari zake ktk kiwango cha testosteron kwenye serum (blood), pia hematological, biochemical na histopathological changes. Utafiti ulitumia panya dume wanaolingana uzito walio na umri wa wiki 6 ambao kwa wao ndio kipindi cha kupevuka (balehe). Panya hao walikuwa wanapewa chakula cha aina moja na treatments za aina moja kasoro ktk suala la mafuta ya taa.

NJIA ZILIZOTUMIKA KWENYE UTAFITI

Panya waliwekwa ktk makundi matatu; control group (waliokuwa wanapewa distilled water), waliokuwa wanapewa dozi ya chini (10 μl ya mafuta ya taa) na waliokuwa wanapewa dozi ya juu (300 μl ya mafuta ya taa).

Samples za damu za panya hao zilichukuliwa mkiani siku ya 7 na siku ya14. Mwishoni mwa utafiti (siku ya 28) samples za damu zilikusanywa kupitia moyo kuchomwa baada ya panya hao kusinziishwa kwa klorofomu. Tishu za sehemu za ndani za tumbo (stomach), umio (esophagus) na ubongo zilichukuliwa baada ya kuwapasua panya ili kuchunguza tissues za viungo hivyo.

MATOKEO YA UTAFITI

  1. Mafuta ya taa hayakuwa na athari katika uzito wa panya.

  2. Mafuta ya taa yalipelekea kuongezeka kwa viwango vya homoni ya Testosteron ktk serum (damu) kwa wanyama waliopewa mafuta ya taa.

  3. Mafuta ya taa yalipelekea kuongezeka kwa matukio ya kushambuliana na kutoana damu kwa panya walipewa mafuta hayo. Hii ilitokana na kuongezeka kwa vitendo vya uchokozi na ukorofi miongoni mwa wale waliopewa mafuta ya taa. Mtafiti anasema kuwa iliongezeka ugumu ktk kuwapatia dozi zao za mafuta ya taa panya wa kundi hili kutokana na utata wao.

    Kwa wale panya ambao hawakupewa mafuta ya taa haikuonekana tofauti katika tabia zao kabla na wakati wa majaribio.

  4. Mafuta ya taa hayakuwa na athari ktk ufanyaji kazi wa Ini (liver) na Figo (Kidney).

  5. Mafuta ya taa yalipelekea kuongezeka kwa White blood cells, Red blood cells na Platelets, kutegemeana na dozi ya mafuta ya taa waliyopewa.

  6. Mafuta ya taa yalisababisha ugonjwa wa gastritis kwa panya waliopewa mafuta hayo. Pamoja na kuwa na milo sawa na hali sawa za mazingira, panya wasiopewa mafuta ya taa hawakuwa na dalili za gastritis.

    Gastritis; Ni kuvimba, kuwasha, au kumomonyoka kwa ukuta wa ndani ya tumbo (stormatch lining).

  7. Mafuta ya taa hayakuleta magonjwa yoyote ktk ubongo na esophagus.
UCHAMBUZI WA MATOKEO YA UTAFITI

Kuongezeka kwa viwango vya testosteron kutokana na matumizi ya mafuta ya taa ktk chakula (shule za bording) kwa namna fulani kunahusishwa na kuongezeka kwa kesi za vijana hao kujihusisha na ngono ktk umri mdogo na hatimae kusababisha kuongezeka kwa kesi za magonjwa ya zinaa, mimba za utotoni na fujo kama vile migomo mashuleni.

Kuongezeka kwa red blood cells (RBC) kutokana na kutumia mafuta ya taa kwenye chakula inaweza kuwa na faida ya kuongeza uwezo wa damu kubeba oksijeni.

Kama ilivyoelezwa awali, kulikuwa na ongezeko la white blood cells kwa panya waliopewa mafuta ya taa. Hii inadhaniwa kuwa inatokana na mfumo wa kinga ya mwili (body immune system) kujihami dhidi ya components za mafuta ya taa.

HITIMISHO

Utafiti unapendekeza njia mbadala, madhubuti na salama ya kudhibiti msongo wa ngono (libido) kwa wanafunzi wa shule za bweni.

SOURCE (RESEARCH ARTICLE)

Njorogea RW, Machariab BN, Sawec DJ and Maiyohc GK 2015 Effects of crude kerosene on testosterone levels, aggression and toxicity in rat. Toxicology Reports. 2: 175–183.
 
Kitu cha boarding hicho. Mafuta ya taa kwenye mchicha.

Ila sina uhakika hiyo kupunguza hamu ya ngono
 
Mkuu usinikumbushe Tosa siku wakiwa wanakuja Iringa girls a.k.a Zoo tulikua tunapigwa futa la taa wiki nzima kabla ya disco. Ila vidume pamoja na futa la wiki nzima bado tulikua tunadindisha
Ha ha ha ha umenikumbisha mbaliii Sana Enzi za zoo unakuta mlunza kalikoleza futa kweli kweli
 
Tulikuwa tunadanganywa eti yamedondokea bahati mbaya kumbe wanatuongezea fujo na hamu ya zinaa (kwa mujibu wa utafiti alioudokoa kwenye source yake)
 
Enzi za MAZENGO kwa mzee Shed!
hahaha kumbe ilkuwa kuongeza ukorofi tu, ndio maana vurugu zilkuwa nyingi sana miaka ile mashuleni.
 
*****...ilboru nimenyweshwa sana mafuta ya taa..till mpaka nkawa nikisikia tu harufu.naenda kununua msosi umenyeni..
huyo toxicologist itabidi aendelèe kudadavua vizuri utafiti wake..
 
UTANGULIZI

Mafuta ya taa ni distillate ya mafuta ya petroli ghafi. Matumizi ya mafuta ya taa ghafi katika vyakula vya shule za bweni imekuwa jambo la kawaida katika Afrika Mashariki na nchi nyingine kwa miaka mingi, na imani iliyojengeka ni kuwa yanasaidia kupunguza hamu ya kufanya ngono (libido) kwa wanafunzi walio katika kipindi kigumu mno cha kubalehe (kupevuka). Katika milo yao ya shule za bweni, wanafunzi wamekuwa wakiwekewa dozi za mafuta ya taa kama sehemu ya vyakula pasi na utashi wao.

Ktk mchakato wa kubalehe baadhi ya homoni maalum hutolewa ambazo kimsingi ndizo huibua mabadiliko ya kimaumbile (secondary sexual characteristics) ili kuwawezesha vijana kuwa na uwezo wa kusababisha/kushika mimba (kuzaliana). Moja ya homoni hizo ni testosteron ambayo husababisha kuongezeka kwa ari ya kufanya ngono, upanuzi wa viungo vya uzazi kama vile uume na korodani, uzalishaji wa mbegu za kiume, ongezeko la misuli n.k. (kwa wavulana).

Mbali ya kuwa ufanisi wa mafuta ya taa katika kupunguza ari ya sexual intercouse haujawahi kuthibitishwa kisayansi na wala uchunguzi wa madhara katika mwilini haujafanyika lakini yameendelea kutumika mashuleni.

Utafiti ulioundwa Kenya kufuatilia athari zake ktk kiwango cha testosteron kwenye serum (blood), pia hematological, biochemical na histopathological changes. Utafiti ulitumia panya dume wanaolingana uzito walio na umri wa wiki 6 ambao kwa wao ndio kipindi cha kupevuka (balehe). Panya hao walikuwa wanapewa chakula cha aina moja na treatments za aina moja kasoro ktk suala la mafuta ya taa.

NJIA ZILIZOTUMIKA KWENYE UTAFITI

Panya waliwekwa ktk makundi matatu; control group (waliokuwa wanapewa distilled water), waliokuwa wanapewa dozi ya chini (10 μl ya mafuta ya taa) na waliokuwa wanapewa dozi ya juu (300 μl ya mafuta ya taa).

Samples za damu za panya hao zilichukuliwa mkiani siku ya 7 na siku ya14. Mwishoni mwa utafiti (siku ya 28) samples za damu zilikusanywa kupitia moyo kuchomwa baada ya panya hao kusinziishwa kwa klorofomu. Tishu za sehemu za ndani za tumbo (stomach), umio (esophagus) na ubongo zilichukuliwa baada ya kuwapasua panya ili kuchunguza tissues za viungo hivyo.

MATOKEO YA UTAFITI

  1. Mafuta ya taa hayakuwa na athari katika uzito wa panya.

  2. Mafuta ya taa yalipelekea kuongezeka kwa viwango vya homoni ya Testosteron ktk serum (damu) kwa wanyama waliopewa mafuta ya taa.

  3. Mafuta ya taa yalipelekea kuongezeka kwa matukio ya kushambuliana na kutoana damu kwa panya walipewa mafuta hayo. Hii ilitokana na kuongezeka kwa vitendo vya uchokozi na ukorofi miongoni mwa wale waliopewa mafuta ya taa. Mtafiti anasema kuwa iliongezeka ugumu ktk kuwapatia dozi zao za mafuta ya taa panya wa kundi hili kutokana na utata wao.

    Kwa wale panya ambao hawakupewa mafuta ya taa haikuonekana tofauti katika tabia zao kabla na wakati wa majaribio.

  4. Mafuta ya taa hayakuwa na athari ktk ufanyaji kazi wa Ini (liver) na Figo (Kidney).

  5. Mafuta ya taa yalipelekea kuongezeka kwa White blood cells, Red blood cells na Platelets, kutegemeana na dozi ya mafuta ya taa waliyopewa.

  6. Mafuta ya taa yalisababisha ugonjwa wa gastritis kwa panya waliopewa mafuta hayo. Pamoja na kuwa na milo sawa na hali sawa za mazingira, panya wasiopewa mafuta ya taa hawakuwa na dalili za gastritis.

    Gastritis; Ni kuvimba, kuwasha, au kumomonyoka kwa ukuta wa ndani ya tumbo (stormatch lining).

  7. Mafuta ya taa hayakuleta magonjwa yoyote ktk ubongo na esophagus.
UCHAMBUZI WA MATOKEO YA UTAFITI

Kuongezeka kwa viwango vya testosteron kutokana na matumizi ya mafuta ya taa ktk chakula (shule za bording) kwa namna fulani kunahusishwa na kuongezeka kwa kesi za vijana hao kujihusisha na ngono ktk umri mdogo na hatimae kusababisha kuongezeka kwa kesi za magonjwa ya zinaa, mimba za utotoni na fujo kama vile migomo mashuleni.

Kuongezeka kwa red blood cells (RBC) kutokana na kutumia mafuta ya taa kwenye chakula inaweza kuwa na faida ya kuongeza uwezo wa damu kubeba oksijeni.

Kama ilivyoelezwa awali, kulikuwa na ongezeko la white blood cells kwa panya waliopewa mafuta ya taa. Hii inadhaniwa kuwa inatokana na mfumo wa kinga ya mwili (body immune system) kujihami dhidi ya components za mafuta ya taa.

HITIMISHO

Utafiti unapendekeza njia mbadala, madhubuti na salama ya kudhibiti msongo wa ngono (libido) kwa wanafunzi wa shule za bweni.

SOURCE (RESEARCH ARTICLE)

Njorogea RW, Machariab BN, Sawec DJ and Maiyohc GK 2015 Effects of crude kerosene on testosterone levels, aggression and toxicity in rat. Toxicology Reports. 2: 175–183.
Inawezekana, maana kama kuna lead ndugu yangu utamtesa mama Njile...
 
Imewasilishwa vizuri lakini panya na human kuna tofauti fulani.
 
Back
Top Bottom