Utafanyeje pale unapogundua mchumba ako aliwahi kutoa mimba?

Mcheza Karate

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
690
350
Wadau,

Habari za mchana huu, naomba tubadilishane mawazo kwa hili.

Una mchumba ambaye bado kama miezi 2 kufunga pingu za maisha.
Kila kitu kipo tayari lakini unafika kugundua kuwa mchumba ako aliwahi kushika mimba na akatoa lakini kabla hajawa na mahusiano na wewe.

Na wakati mnaanza uhusiano alikuficha kuhusu hilo na anakataa kabisa kukutana kimwili na wewe hadi pale mtakapofunga ndoa.

Hivi kama ni wewe utafanyaje? Binti anakubania kutoa mzigo kwa gia ya kuwa yeye msafi lakini unagundua kuwa sivyo kwani hadi aliwahi kuchoropoa KIUMBE na maandalizi ya ndoa yako tayari.

Nawasilisha
MK.
 
Du!
Wewe una uhakika kuwa hukuwahi kumtoa mtu mimba?
Hizi hukumu za wanaume zinakuwa na mfumo dume!
Kama hakupi mzigo ina maana hata kama alifanya kosa wakati huo basi alishajirekebisha, anataka upate kitu QUALITY siku ya siku!
 
Kuhusu kutoa Mimba unaweza kumsamehe,no one is perfect atakuwa aliteleza,BUT usikubali kuoa bila
kula mzigo,utakuja kujilaumu maisha yako yote mkuu!!Never ever do that...utauziwa mbuzi kwenye gunia
 
PakaJimmy umesema ukweli maelezo hakuna!ajiulize katika maisha yake kuna wangapi aliowaacha na mimba kwa kujua au kwa kutokujua!
Kwa njinsi nilivyo muelewa mtoa mada kuwa alikuwa na matarajio makubwa sana yakuwa huyo mchumba wake hapendelei sana mambo ya kuduuu kwa sababu hata yeye muoaji kanyimwa sasa kinachomuumiza akili baada ya kugundua kuwa alishawahi kutoa kwa mwingine na mimba juu, Kwa upeo wangu kosa lilifanywa na huyo mchumba wake kwa kutokumueleza kwanini hapewi mpaka ndoa ingawa huko nyuma alishawahi kutoa
 
chambua kwa undani maelezo yako
Kwa sababu mchumba amesha onja radha nyingine huko inabidi jamaa naye apime asije ambiwa kibamia, au haifanyi vizuri kama ya nani...... wakati wameshaingia kwenye ndoa, na jamaa pia inawezakana naye kapita huko alikuwa kwa akina naniii asije akamwambia mwenzie sio tamu, bwawa au imekaaje nk, hii yote inataokana na kuanza kujaribu sehemu tofauti na ndio maana siku hizi kuna kulinganisha hata wakiwa kwenye ndoa so ni muhimu kupimana uwezo kwanza isije ikapelekwa kule hapo baadae baada ya kuona kiwango duni
 
Kuhusu kutoa Mimba unaweza kumsamehe,no one is perfect atakuwa aliteleza,BUT usikubali kuoa bila
kula mzigo,utakuja kujilaumu maisha yako yote mkuu!!Never ever do that...utauziwa mbuzi kwenye gunia
wanaume bana mnanichekeshaga sana du inaonyesha 90 ya wanandoa ni wazinzi waliokubuhu du?
 
Wadau,

Habari za mchana huu, naomba tubadilishane mawazo kwa hili.

Una mchumba ambaye bado kama miezi 2 kufunga pingu za maisha.
Kila kitu kipo tayari lakini unafika kugundua kuwa mchumba ako aliwahi kushika mimba na akatoa lakini kabla hajawa na mahusiano na wewe.

Na wakati mnaanza uhusiano alikuficha kuhusu hilo na anakataa kabisa kukutana kimwili na wewe hadi pale mtakapofunga ndoa.

Hivi kama ni wewe utafanyaje? Binti anakubania kutoa mzigo kwa gia ya kuwa yeye msafi lakini unagundua kuwa sivyo kwani hadi aliwahi kuchoropoa KIUMBE na maandalizi ya ndoa yako tayari.

Nawasilisha
MK.
mpaka hapo mshukuru mungu mkeo sio mgumba mkuu
 
Duu ingenipa kufikiria mambo yafuatayo ...
1. Ni muongo
2. Si muaminifu kwenye maisha yake
3. Hayuko makini kwenye mahusiano yake, alipataje mimba wakati kuna njia za kutosha kuzuia mimba? Anyway mimba alifanikiwa kutoa, ingekuwa UKIMWI je, nao angetoa?
4. Kutoa mimba maana yake ni kupotezea uhai wa kiumbe kisicho na hatia, nitahisi kumuogopa!

Ila pia inawezekana makosa ya hapo juu yalimfanya
1. Kuwa muongo maana angekwambia ukweli usingekubali kumuoa
2. Kukunyima mzigo maana angekupa yangeweza kumtokea yale yale kama ya mwanzo
3. Kabadilika na kuamua kuwa mwaminifu kwa Mungu wake na kwako pia!

Nakushauri mkuu soma maelezo hapo juu, akili ya kuambiwa changanya na ya kwako na AMUA mwenyewe, LOL!
 
Huyo dadainao nyesha alijifunza kutokana na makosa ya wezekana wengi walisha gusa mzigo kwa minadi ya ndoa ndiyo maana anakubania hadi utimize ahadi
 
Du!
Wewe una uhakika kuwa hukuwahi kumtoa mtu mimba?
Hizi hukumu za wanaume zinakuwa na mfumo dume!
Kama hakupi mzigo ina maana hata kama alifanya kosa wakati huo basi alishajirekebisha, anataka upate kitu QUALITY siku ya siku!
PakaJimmy mtoa mada alikuwa anajua atakutana na kitu sildi hakijabanduliwa karatasi
 
Last edited by a moderator:
Duu ingenipa kufikiria mambo yafuatayo ...
1. Ni muongo
2. Si muaminifu kwenye maisha yake
3. Hayuko makini kwenye mahusiano yake, alipataje mimba wakati kuna njia za kutosha kuzuia mimba? Anyway mimba alifanikiwa kutoa, ingekuwa UKIMWI je, nao angetoa?
4. Kutoa mimba maana yake ni kupotezea uhai wa kiumbe kisicho na hatia, nitahisi kumuogopa!

Ila pia inawezekana makosa ya hapo juu yalimfanya
1. Kuwa muongo maana angekwambia ukweli usingekubali kumuoa
2. Kukunyima mzigo maana angekupa yangeweza kumtokea yale yale kama ya mwanzo
3. Kabadilika na kuamua kuwa mwaminifu kwa Mungu wake na kwako pia!

Nakushauri mkuu soma maelezo hapo juu, akili ya kuambiwa changanya na ya kwako na AMUA mwenyewe, LOL!

Duh, kaazi kweli kweli... kujiuliza maswali yote hayo nitaja kufa kwa presha, chezea huyu kiumbe mwanamke weye...
Mie huwa siangalii nyuma hata kidogo, pale pale nilipoanzia ndio pananihusu, mambo yake ya ujanani yatanifaa nini mie,,,

Mama Ngina hebu songa ugali tule sie...
 
Back
Top Bottom