Utafanyaje.......

Song'ito

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
348
147
Tufanye mathalan ulipata nafasi ya kwenda kujiendeleza kimasomo nchi za magharibi katika kutafuta shahada ya uzamivu, muda wa shahada ni miaka 4... shule yako hiyo haikuruhusu kurudi nyumbani bongo mara kwa mara kutokana na kukaba na pia gharama kali ya usafiri wa anga , mdogo wako wa kiume anayekufata anaishi mji mmoja na unaoishi wewe na mkeo, unapoondoka unamsisitiza asiache kuitembelea familia yako na kuijulia hali, wewe umeoa na una watoto watatu na mkeo wakati unaondoka, na mdogo wako nae ana mke na watoto....

Baada ya miaka 2 unabahatika kurudi likizo nyumbani na kukuta mkeo ni mja mzito wa miezi 7 au 8, unambana hasa akueleze ni mimba ya nani, mwishoni anakuambia ni ya mdogo wako na anaomba msamaha kwa kuwa alipitiwa na shetani, na umbali ulichangia kumtia majaribuni.....
katika hali hiyo, Ingelikuwa ni wewe ungechukua uamuzi gani?
 
Tena unasamehe sabini mara elfu saba.

We acha kabisa usifanye mchezo na kulea mtoto unayejua siwako hata angekua kapewa na baba nisingekubali msamaha mbaya zaidi ni kua mdogo wangu yuko hapo namuona.sitakubali kabisa kwanza heshma na ndugu yangu haipotena pia ukimsamehe wataendeleza game
 
Tena unasamehe sabini mara elfu saba.
Hali kama hii huwa ni ngumu siku zote na ukiangalia baba wa mtoto atakayezaliwa unamjua. hapa heshima hupungua kwa ndugu husika na hatimae unaanza uadui mkubwa sana kati ya ndugu hao..... mke anasameheka ila sasa yule mtoto ndio machungu yanapoibukia.....
 
mi kwa upande wangu nitawasamehe wote kwa walilotenda, lakini sitaishi tena na huyo mwanamke wala huyo mtoto.
 
mi kwa upande wangu nitawasamehe wote kwa walilotenda, lakini sitaishi tena na huyo mwanamke wala huyo mtoto.
nakupata mkuu, nini juu ya futue ya watoto wako wengine? utaishi nao au wataishi na mama yao, na je unajua kuwa malezi ya mzazi mmoja ni ya tabu na watoto wengi wanaolelea malezi hayo hawapo vizuri kitabia? najaribu kuibua changamoto tu katika hili..
 
Samehe upate thawabu kwa Mungu

jiweke katika nafasi ya huyo mheshimiwa, tufanye ni wewe sasa!! utasamehe kutoka moyoni na kuendelea na maisha na mkeo kama zamani mkinywa kufurahi na kucheka kama awali?
 
Shetani alimpitia huyo mdogo wa mume tu na yeye je?.....Kama ni mimi nasemehe namove on...
 
Songíto;3730749 said:
jiweke katika nafasi ya huyo mheshimiwa, tufanye ni wewe sasa!! utasamehe kutoka moyoni na kuendelea na maisha na mkeo kama zamani mkinywa kufurahi na kucheka kama awali?

ni ngumu but kuna wa2 wameumbiwa mioyo ya kusamehe,kama yeye ni mmojawapo asamehe na maisha yaendelee
 
ukitaka kumpa talaka atataka mgawane ngawira pasupasu... namsamehe kwa hila..nawnda kupima dna na madogo then nauza mali zote kwa mkupuo halafu nduki kali na ntakaobaini ni wanangu...BUT JIBU LANGU NI MATHALAN
 
haya bana nimekusoma mkuu.....
 
Back
Top Bottom