Utafanya nini utakapoambiwa kuwa wewe ni mgumba wakati mkeo aliishakuzaliwa watoto wawili?

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
Utafiti umeonyesha kuwa karibu 40% ya wanaume waliokwenda kupima Muhimbili wamegundulika kuwa wagumba. Je itakuwaje iwapo daktari atakwambia kuwa wewe huwezi kushikisha mimba wakati mke aliishakuzaliwa watoto wawili au watatu unaoamini ni wako na unawapenda kichizi? Kwa habari zaidi bonyeza hapa.
 
Kama tayari umekwisha assume watoto ni wako kwa nini kwenda kupima? Na hata kama tayari kuna watoto basi assume amewa-adopt na habari iweimekwisha!!

Halafu hiyo 40% idadi yake ni ngapi? isijekuwa wanne (4) kati ya kumi (10) waliokwenda kupima. Ni waliokwenda mwaka jana au toka kipimo hicho kiingie Bongo?
 
kuna tatizo la uandishi wa taarifa hii, ni asilimia 40 ya wanaume waliofika muh ndio wenye tatizo na si ya wanaume wote wa tanzania, kwa maneno mengine watafiti walitumia convinient sampling na si systematic random sampling, hivyo idadi ya wanaume hao waliofika muh haiwezi kuwakilisha wanaume wote wa tz
 
Kwanini kuandikia mate wakati mmewekewa link? Bonyeza pale ndipo muweze kupata basis ya kutoa dukuduku zenu vilivyo. It is just simple-bonyeza link.
 
Utamshukuru mkeo kwa kukusitiri, si ajabu ndugu zako walishaanza kuchonga mama wa watu akaona aokoe jahazi. Kakaa kwa adabu na heshima hujastuka wala nini (hapo I assume na ww hukuanza kuleta nyodo wakati mmechelewa kupata mtoto). Sh@t happens!
 
nitamwambia mke wangu hongera kwa kunifichia aibu

hlafu wanaume siku hizi mbona mnamatatizo mengi? mara ugumba, mara kukosa/kupungua nguvu?
muache kula chipsi mayai aaarrrgh
 
hata kama utakua unawatoto wawili wa kwako kabisa ugumba unaweza kukupata kama mtafiti alivyo fafanua sababu za ugumba. so link uweze fahamu
 
Ningeamua kusoma tena andiko manake linaonekana haliko sawa, kusoma between lines and i will cross all the t's na dotting all the i's. Ukweli lakini utabaki kuwa ukweli
 
Nitamshukuru sana mke wangu kwakunizalia watoto kabla sijapata huo ugumba,yaani nitaamini kuwa huo ugumba nimeupata baada ya kupata watoto,na kwamtindo huo maisha yataendelea!!!
 
Utafiti umeonyesha kuwa karibu 40% ya wanaume waliokwenda kupima Muhimbili wamegundulika kuwa wagumba. Je itakuwaje iwapo daktari atakwambia kuwa wewe huwezi kushikisha mimba wakati mke aliishakuzaliwa watoto wawili au watatu unaoamini ni wako na unawapenda kichizi? Kwa habari zaidi bonyeza hapa.

Ugumba unaweza kukupata baada ya kuwa na watoto pia. Mimi nitaacha mambo yawe siri kama yalivyo, yanini kuhangika, kunyang'anywa watoto na kudhalilika mtaani? Maisha yenyewe mafupi. Yanini kuwachanganya na kuwashangaza watoto kwa kuwaambia mimi sio baba yao. Ila kama ni kweli inauma sana kujua kwamba mimi ni mgumba ila mke wangu ana watoto ambao sio wakwangu, ndoa itakuwa sio ndoa tena ila nitaifanya kuwa siri kati yangu na mke, nitamuomba Mungu aniwezeshe kuwa na moyo wa uvumilivu kupita kawaida ili kumalizia siku za kuishi hapa duniani.
 
Utamshukuru mkeo kwa kukusitiri, si ajabu ndugu zako walishaanza kuchonga mama wa watu akaona aokoe jahazi. Kakaa kwa adabu na heshima hujastuka wala nini (hapo I assume na ww hukuanza kuleta nyodo wakati mmechelewa kupata mtoto). Sh@t happens!
..Eh! kaazi kweli kweli..!!
 
Jinsi kinababa
wanavyowahangaishaga kinamama
kwa swala hili
inaumizaga saaana,
put urself under the shoes za
huyo mkeo anayejibiwa
kuwa ni mgumba,ooops
waweza kufa.na mianaume mingine
hovyooo ikiambiwaga ikapime badala ikubali atabisha
na kung'ang'ania
kwamba mkewe ndo anamatatizo!
Kwamba eti ulitoa mimba sana ndo maana!
Hata kwetu hapa yupo
mjinga wa hivyo,
 
Back
Top Bottom