Utabiri wangu kuhusu yale yatakayojiri mwaka 2014

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
Sayari itakayo tawala mwaka wa 2014 ni Mercury au Attwarid

Mercury-Attarid inahusika na mambo yanayohusiana na Adabu, Malezi mema, Mantiki, Kupata kitu, Fasihi ya lugha, Ufahamu, Uelewa, Elimu, Urafiki, Hila na kudanganya, Hesabu, Vitabu, Sanaa za aina zote, Ukatibu au Ukarani, Shule au Kumpeleka mtoto shule.

Vile vile inahusiana na mambo ya Nakshi, masuala ya Urembo, kuandaa majeshi, nidhamu na leo ni siku nzuri kuvaa nguo za hariri. Kwa ujumla ni Sayari ya mapato.
Katika utabiri mfupi wa mwaka ni kusema;
1. Tutarajie hali ya maisha kupanda.
2. Dola kupata nguvu dhidi ya sarafu kadha za duniani.
3. Vifo vya wasanii au watu mashuhuri kiserikalini.
4. Mwaka huu tunatarajia kupata ajali mbaya ya barabarani
5. Viongozi kuridhisha uongozi kwa wanao katika nchi za nje sababu ya ugonjwa.
6. Msururu wa mauwaji ya watu mbalimbali kuendelea.
7. Melewano ya mzozo wa S.Sudan yakitatuliwa na jumuia ya kimataifa.
8. Mzozo ndani ya Jubilee kuendelea.
9. Jubilee serikali ya Kenya kuanza utimizaji wa baadhi ya ahadi zake.

Mengine ntawaelezea kadri siku zinapoanza. Nawatakia mwaka mpya mwenye fanaka.
 
tetetette hv mzizi mkavu pia ni mtabiri wa hali ya hewa? ahaaaa samahani ni mtabiri wa mambo mbalimbali? nauliza tu mkuu.
 
Vipi Lowassa atavuka huu mwaka kwa jinsi stroke inavyomwandama?
Naomba ufafanuzi katika hili
 
Mzizi kweli ni mult-talented. Hadi kwenye unajimu umo ndugu yangu? Haya bana kila la heri, natumaini huu ubashiri wako utakuwa wa kweli.
 
Unatabiri mafuriko kwenye kipindi cha masika uku ukijua miundo mbinu mibovu.

Ajali mbaya ziko kila mwaka. Na utatuzi wa south sudan tayari jeshi la umoja limeongeza idadi ya askari wake na mazungumzo yanaendelea.

Umeme umepanda hivo vitu vingi vitapanda sababu vinatengenezwa viwandani na uko wanatumia umeme ata vyakula vitapanda sababu unga na mchele ukobolewa kwa mashine.

Umeleta usanii kila kitu kiko wazi.

Na ata mizozo ya Jubilee haijaanza leo imeshaonekana na wasanii hawajaanza leo kufa ata mwaka jana walikufa.

Hivo hakuna ulilotabiri kila kitu kiko wazi ni sawa na kutabiri mwaka huu rais jk ataenda marekani
 
Sayari itakayo tawala mwaka wa 2014 ni Mercury au Attwarid

Mercury-Attarid inahusika na mambo yanayohusiana na Adabu, Malezi mema, Mantiki, Kupata kitu, Fasihi ya lugha, Ufahamu, Uelewa, Elimu, Urafiki, Hila na kudanganya, Hesabu, Vitabu, Sanaa za aina zote, Ukatibu au Ukarani, Shule au Kumpeleka mtoto shule.

Vile vile inahusiana na mambo ya Nakshi, masuala ya Urembo, kuandaa majeshi, nidhamu na leo ni siku nzuri kuvaa nguo za hariri. Kwa ujumla ni Sayari ya mapato.
Katika utabiri mfupi wa mwaka ni kusema;
1. Tutarajie hali ya maisha kupanda.
2. Dola kupata nguvu dhidi ya sarafu kadha za duniani.
3. Vifo vya wasanii au watu mashuhuri kiserikalini.
4. Mwaka huu tunatarajia kupata ajali mbaya ya barabarani
5. Viongozi kuridhisha uongozi kwa wanao katika nchi za nje sababu ya ugonjwa.
6. Msururu wa mauwaji ya watu mbalimbali kuendelea.
7. Melewano ya mzozo wa S.Sudan yakitatuliwa na jumuia ya kimataifa.
8. Mzozo ndani ya Jubilee kuendelea.
9. Jubilee serikali ya Kenya kuanza utimizaji wa baadhi ya ahadi zake.

Mengine ntawaelezea kadri siku zinapoanza. Nawatakia mwaka mpya mwenye fanaka.

Sijaona utabiri wowote hapo, haya yote uliyoyalist ni mambo ambayo hayana budi kutokea.
Hata usingetabiri yatatokea tu.
 
Back
Top Bottom