Nyumbu
Senior Member
- May 22, 2008
- 141
- 1
Mkuu wangu hakuna ugumu kabisa ktk kuunganisha Chadema na CUF isipokuwa wote wameingizwa mjini na UDINI.
Hii sio kweli. Nimeshakaa mara kadhaa na viongozi wa vyama vya upinzani tukijaribu kuunganisha nguvu wakati wa uchaguzi ili tuwe na mgombea mmoja wa upinzani. Nina diriki kusema ukindoa CUF vyama vingine vyote vya upinzani ni mapandikizi au viongozi wao wa juu ni vibaraka vya CCM. Kwa namna moja au ingine huwa wanafadhiliwa au wanawezeshwa na CCM kwa vile wanatumia hivi vyama kama miradi ya kutafutia pesa. Tatizo la CUF ni kwamba uongozi wao wa juu una concentrate kwenye siasa za zanzibar tu. Hawako tayari ku compromise chochote when it comes to mainland politics. Na hii ndio sababu waliamua kumweka Lwakatare pembeni ambaye alikuwa anawasumbua na kelele zake za Ubara. Naomba ujiulize ni kwanini wabunge wa CUF na CHADEMA wanashirikiana vizuri sana bungeni ilhali viongozi wa CUF kila siku wako kwenye majukwaa wakiiponda CHADEMA? Wabunge wa CUF macho yao yako Dodoma, viongozi wa CUF macho yao yako Pemba na Unguja.
.