Uswazi kuna raha zake, wazijua?

Unatembea na mswaki wako ukiwa mdomoni mpaka dukani kununua sigara.
Akiongea sasa, mipovu ya dawa ya mswaki ina tiririka kidevuni.
Uswazi ni Full Vituko asikwambie mtu

Kukutana na mwanamama na rollers zake kichani; kajifunga taulo na swaki mdomoni hapo dukani kwa Mangi siyo kitu cha kushangaza!
 
Nashukuru maisha yangu yote sijaishi uswazi,lakini ipo siku nimemtembelea msela wangu uswazi tumekaa ndani tunasubiri wali umebanikwa uani , kwenda kuchungulia anarudi anasema jamaa wameiba wali na sufuria lake...............

hahahahahaha, yani nimecheka mpaka nimemwamsha mtoto.
 
akina mama wanaoshinda nyumban tabu tupu. . yan wakiona umepika kapilau na wenyewe hao. ukinunua hiki na wenyewe wananunua. yan full mashindano. ukisuka yeboyebo nao wanasuka kha!
 
Kukutana na mwanamama na rollers zake kichani; kajifunga taulo na swaki mdomoni hapo dukani kwa Mangi siyo kitu cha kushangaza!

We acha tu,
wa Masaki hapawezi Uswazi.
Kila siku shughuli,watu wanachanga kutunzana,full kigodoro mpaka kunakucha, Full Kiduku.
Gongo linanyweka kama kazi,kubashiana ndo mpango mzima.
Ila Mpoki alishasema,
Daily News haliuzwi Tandale kwa Mtogole
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom