Usomi dhidi ya Elimu = Ujinga wetu

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Tangu tuingie kwenye utandawazi na siasa za vyama vingi hapa Tanzania kila mtu anataka kuonekana msomi. Siku hizi kuna vyuo vikuu vingi sana hapa nyumbani (vingine uchwara) ambavyo watanzania wengi wanasoma huko. Lakini jambo pekee linalojitokeza kwenye jamii yetu tuko makini sana kuwa wasomi bila ya kujali kama tunaelimika.

Tunao wasomi wengi wa nyanja mbalimbali lakini mpaka sasa wengi wao wameshindwa kututhibitishia kama usomi wao unaendena na elimu iliyokusudiwa. Kila mtu anataka kuwa msomi, lakini ni wangapi wetu leo hii tunataka kuelimika? Hapo ndipo tulipokwama.Mtu ana shahada ya Uzamivu (PHD) anawezaje kusaini mkataba feki? Siasa zetu na uchumi wetu hauwezi kubadilika bila ya kuwa na wasomi wenye elimu ya kutosha.

Samahani kwa kutumia lugha ya KIswahili ambayo si ya kisomi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom