Uso kwa uso na mtoto wa Rais Mwinyi (mbunge wa A/M)utetezi wake kuhusu watoto wa vigogo na vyeo

Mara ningi siwezi na nasipendi kujadili watu. Lakin Dr Hussein Mwinyi ana utashi mkubwa ndio maana alichaguliwa kuwa mbunge wa Mkuranga kabla kuvuka maji na kuchaguliwa mjini unguja. Pasi na shaka yoyote ana mvuto mkubwa sana kwa wapiga kura wake na ndio maana akachaguliwa.

Kama utajiepusha na utumwa wa akili wa kuona KUWA NI DHAMBI KUBWA KWA MTOTO WA KIGOGO KUGOMBEA UONGOZI na kujali uwezo na utashi wa uongozi wa jamii utakuwa umejitenga sana na dhambi ya ubaguzi kwa watoto wa vigogo.

Mimi nakushauri angalia vigezo na maamuzi yote yanabaki kwa wapga Kura ambao ndio wanaomchagua au kumbwaga.

Pole sana

Nadhani wewe ndio unastahili pole...utajadili vipi siasa bila kujadili wanasiasa(watu)?.......nina hakika kabisa ''DR'' HUSSEIN asingekuwa katika siasa kama si kwa baba yake kuwa Rais......achilia mbali kuwa ''Daktari''
 
Nafikiri cha kutambua hapa si kwamba watu wanalalamika kwamba mtoto wa kiongozi asiwe na yeye kiongozi,hapana!,swala ni kwamba anatumia jina la mzazi wake kupata hiyo nafasi!.Kama mzee mkubwa,mtoto na mama wamepita,na hawajapita kihalali,wametumia jina la mkuu.Hilo ndo linalalamikiwa,inatakiwa kwenye uchaguzi wowote kuwe na fair play.

NaKUBALIANA nawe Mkuu. Naongeza Jina na OFISI ya Bwana kujipatia nafasi. Kwa Mfano huko LINDI ni "nani hajipendi" achukue fomu ya kuchuana na FIRST LADY? GHivyo kujiondoa kwa wagombea "WAZURI" kuliko first lady ilikuwa ni WOGA kwa MKE wa RAIS
 
Nadhani wewe ndio unastahili pole...utajadili vipi siasa bila kujadili wanasiasa(watu)?.......nina hakika kabisa ''DR'' HUSSEIN asingekuwa katika siasa kama si kwa baba yake kuwa Rais......achilia mbali kuwa ''Daktari''

Labda asingekuwa mwanasiasa, ila elimu yake ameipatia Uturuki pasina shaka yoyote. Alihitimu. Na mama yake alipokwenda sherehe za mahafali, alikaa kwenye hoteli ya kawaida (hakuenda kama First Lady wa nchi), magazeti ya Uturuki yakapata mengi ya kusema.
 
Kimsingi, linapokuja suala la Ubunge au teuzi nyengine za kidemokrasia, hatupaswi kuwalaumu watoto wa vigogo hata kidogo, badala yake tunapaswa kujilaumu sisi wananchi tunaowachagua; kwamba tunapumbazwa na majina (iwapo hana uwezo)

Kwa nafasi za kuteuliwa au kupachikwa, tatizo halikomi kwenye CCM tu. CCM wanaongoza, lakini na CHADEMA hawapo nyuma. Wanawake wa viti maalum bungeni kwa vyama vyote viwili wanathibitisha uozo huo ulipo.

Misho wa yote, tunarudi kule kule kuwa mwenye kuweza kubadili hili ni mwananchi.

Mwalimu kwa chadema ntakubishia kidogo......tatizo watu wenye uwezo wa uongozi wengi ni waoga kujiunga upinzani hivyo kuacha nafasi ziende kihivyo.......nakumbuka mwaka 1992 Mzee Mtei alivyokuwa anahangaika kushawishi watu na double pick-up yake bila mafanikio....waliojiunga naye wakawa ni ndugu na rafiki wa karibu......na wakakibeba chama kilivyo.....sio rahhisi leo uwabwage kabla ya kupata replacements
 
Labda asingekuwa mwanasiasa, ila elimu yake ameipatia Uturuki pasina shaka yoyote. Alihitimu. Na mama yake alipokwenda sherehe za mahafali, alikaa kwenye hoteli ya kawaida (hakuenda kama First Lady wa nchi), magazeti ya Uturuki yakapata mengi ya kusema.

Baba yake singekuwa Rais nani angempeleka huko uturuki? Kumbuka uwezo wake kishule pia
 
Mwalimu kwa chadema ntakubishia kidogo......tatizo watu wenye uwezo wa uongozi wengi ni waoga kujiunga upinzani hivyo kuacha nafasi ziende kihivyo.......nakumbuka mwaka 1992 Mzee Mtei alivyokuwa anahangaika kushawishi watu na double pick-up yake bila mafanikio....waliojiunga naye wakawa ni ndugu na rafiki wa karibu......na wakakibeba chama kilivyo.....sio rahhisi leo uwabwage kabla ya kupata replacements

What do you mean "sio rahisi uwabwage"?

Kwa hiyo viti maalum ni fadhila? Kuwa walikisaidia chama kwa hiyo sasa tuwape watoto, wakwe, wake, ndugu, hawara nafasi?

Basi sababu ndio hizo hizo wanazotumia CCM. Kuwa kuna watu wamejenga chama, ndio wanarudisha fadhila kwa kuweka watoto wao, wakwe, wake, ndugu, hawara kwenye nafasi za Chama na serikali.

Sababu yoyote itakayotumika ku-justify hali ya CHADEMA kwenye upendeleo kwa watoto wa vigogo ndio hiyo hiyo itakayotumika kwa CCM.
 
Nafikiri kama ni kweli hiyo ndo tatizo. Kupeana nafasi za BOT na serikalini wakati mtu hafai kwa lolote. Anapewa kwa vigezo vya rushwa.

Mnabishana hoja ambayo wenye akili timamu wameona na wanasubiri kuchukua hatua, hiyo sio sahihi kabisa, mbona hata hao wazazi wao utendaji ni sifuri
 
What do you mean "sio rahisi uwabwage"?

Kwa hiyo viti maalum ni fadhila? Kuwa walikisaidia chama kwa hiyo sasa tuwape watoto, wakwe, wake, ndugu, hawara nafasi?

Basi sababu ndio hizo hizo wanazotumia CCM. Kuwa kuna watu wamejenga chama, ndio wanarudisha fadhila kwa kuweka watoto wao, wakwe, wake, ndugu, hawara kwenye nafasi za Chama na serikali.

Sababu yoyote itakayotumika ku-justify hali ya CHADEMA kwenye upendeleo kwa watoto wa vigogo ndio hiyo hiyo itakayotumika kwa CCM.

Mwalimu umekwenda mbali sana.......sasa wasipopewa hao ndugu nani apewe hivyo viti maalumu? Binafsi siafiki viti maalumu...halafu usisahu CCM iko madarakani nan CAHDEMA haiko
 
Wakuu,
Hivi karibuni nilihudhuria kikao cha wabunge wa Afrika mashariki kilichohusu utawala bora. Huko nilipata fursa ya kukutana Mtoto wa Rais Mstaafu Ali Hasan Mwinyi ambaye pia ni mbunge wa Afrika Mashariki. Kikao hicho kiliongozwa na m/kiti na mbunge wa afrika mashariki kutoka Burundi.

Wakati wa majadiliano niliibua hoja nyingi ya kuonesha udhaifu wa serikali ktk kutekeleza utawala bora. Mojawapo ya hoja hizo ni kuhusu watoto wa wakubwa kupewa fursa ya uongozi serikalini na ktk nafasi za kisiasa isivyo halali, jambo ambalo ni kinyume na utawala bora. Hoja yangu hiyo ilimuibua Mbunge Mwinyi na kulazimika kuijibu. Mh. mwinyi alisema huwa ninapokuwa kwenye vikao kama hivi huwa sijibu hoja kama hizi moja kwa moja lakini hii nalazimika kuijibu kuweka rekodi sawa ila akasisitiza kwa upande wa familia yake tu - Rais mstaafu Mwinyi. Baada ya kikao tulilazimika kuendeleza mjadala huo kwa ufupi wakati wa chakula cha mchana + wadau wengine.

Majibu yake kwa ujumla ya kutetea watoto wa vigogo kupata vyeo vikubwa ni kama haya yafuatayo.

Kwanza alisema ktk familia yao ( Rais Ali Hasan Mwinyi) walioko ktk nafasi za kisiasa kupitia ccm ni yeye na Kaka yake Husein Mwinyi (waziri) tu, kati ya watoto 8 au 9 hivi (Idadi kamili imenitoka) Japo hakusema wale wengine wana nafasi gani na wapi? Kwa hiyo, katika upendeleo huo wao hawapo.

Pili, akasema watoto wa viongozi kama watanzania wengine nao wana haki ya kupata fursa hizo, ila tu wawe na uwezo wa kufanya shughuli hizo na akasema mimi na kaka yangu Husein kazi tuliyopewa tunaiweza na hatujapendelewa. sote tulipigiwa kura na kupata ubunge (kaka pia ni mbunge)

Tatu, alisisitiza kwamba kwa kawaida watoto wa wachunguji hupenda kazi za wazazi wao - uchungaji. Vivyo hivyo, watoto wa Mashekh nao ni mashekh. kwa mantiki hiyo ni kawaida sana kwa mtoto wa Rais kutamani siasa, siyo kawaida kutoipenda. Akasema hata kule Amerika Gorge Bush (mstaafu) ni mtoto wa Rais.
Clinton naye alikaribia kuipata nafasi ya mumewe nk. mifano ni mingi duniani.

Nne, mtoto wa kiongozi si tu kwamba anaipenda siasa lakini pia anajifunza mbinu, mikakati na kila aina ya mahitaji yatakayomfanikisha yeye kufanikiwa kama baba yake. Na mtoto Rais au kiongozi mkubwa anakuwa amejifunza kutoka kwa mhusika mwenyewe (horse Mouth) ambaye amefanikiwa mpaka kufikia kiwango cha juu. Hivyo, inategemewa kuwa mtoto wa Rais atakuwa na mafunzo mengi au uzoefu mwingi wa kufanikiwa ktk nafasi za kisiasa kama baba yake aliyefikia mafanikio ya juu sana, hivyo mtoto wa mwanasiasa mkubwa ana nafasi kubwa ya kufanikiwa.

My take;
Hoja hii nimeileta baada ya kuona listi inayozungushwa ktk simu na JF ya vigogo 13 waliowapenyeza watoto wao ktk nafasi za kisiasa kupitia ccm (japo sijathibitisha ukweli wa listi hiyo).

Je huu utetezi unatosha kutetea watoto wa vigogo waliojaa ktk nafasi za serikali na siasa? Bado nakumbuka listi ya watoto wa vigogo benki kuu?

Pamoja na kwamba nilimbana kwa BMW(baba, mama na Watoto) ya JK ktk siasa hakutaka kuwatetea specific leaders japo alitoa maelezo hayo ya jumla tu kama hapo juu.

Naomba kuwasilisha.

Ndio Matatizo ya sisi Watanzania tunaulizana Maswali ya kiurafiki sana; Swali lingepaswa yeye kuulizwa ni kuwa Ina Maana Baba yako alivunja AZIMIO LA ARUSHA na KULI-REPLACE na AZIMIO LA ZANZIBAR ambalo liliua JESHI LA KUJENGA TAIFA ili nyinyi watoto wake wa RAIS ALLY HASSAN MWINYI; Muweze kuingia kwenye SIASA? Sababu Mlisoma nje na MLIGUSHI JESHI LA KUJENGA TAIFA kwahiyo MSINGE WEZA KUFANYA KAZI SERIKALINI na pia KUWA WABUNGE

KWAHIYO BABA YENU KWAWAFANYIA SHORT-CURT... KWA KUVUNJA JKT..

HAYO NDIO YA KUULIZA sio MENGINE...

* CHADEMA kweli Maswali Hayo Rahisi??
 
What do you mean "sio rahisi uwabwage"?

Kwa hiyo viti maalum ni fadhila? Kuwa walikisaidia chama kwa hiyo sasa tuwape watoto, wakwe, wake, ndugu, hawara nafasi?

Basi sababu ndio hizo hizo wanazotumia CCM. Kuwa kuna watu wamejenga chama, ndio wanarudisha fadhila kwa kuweka watoto wao, wakwe, wake, ndugu, hawara kwenye nafasi za Chama na serikali.

Sababu yoyote itakayotumika ku-justify hali ya CHADEMA kwenye upendeleo kwa watoto wa vigogo ndio hiyo hiyo itakayotumika kwa CCM.

Chadema hawana tatizo hilo kihivyo, ni hoja inayolazimishwa na ccm ili ionekane sote tuwachafu. Hata hivyo, napenda tusihame mada nataka tuhusishe mada hii na utawala bora zaidi.
 
Mwalimu kwa chadema ntakubishia kidogo......tatizo watu wenye uwezo wa uongozi wengi ni waoga kujiunga upinzani hivyo kuacha nafasi ziende kihivyo.......nakumbuka mwaka 1992 Mzee Mtei alivyokuwa anahangaika kushawishi watu na double pick-up yake bila mafanikio....waliojiunga naye wakawa ni ndugu na rafiki wa karibu......na wakakibeba chama kilivyo.....sio rahhisi leo uwabwage kabla ya kupata replacements

Nakubaliana na wewe. Watu wengi hawajui kuwa huko nyuma kupata mgombea ilikuwa kazi ngumu sana ndani ya Chadema. Sasa wale wachache waliojitolea wakati huo leo baada ya Chadema kukubalika ndo watu wanawatuhumu. Siyo sawa.

Mada yangu ni uwepo wa watoto wa vigogo na jinsi walivyoathiri utawala bora nchini.
 
Mwalimu umekwenda mbali sana.......sasa wasipopewa hao ndugu nani apewe hivyo viti maalumu? Binafsi siafiki viti maalumu...halafu usisahu CCM iko madarakani nan CAHDEMA haiko

Unataka kusema hakuna watu wengine kwenye chama isipokuwa hao watoto wa vigogo?

Let's be real, Watanzania tunapenda sana kupapatikia majina. Haijalishi mtu yupo kwenye chama gani

Mtu kama yule "Mbunge wa Maryland," unadhani amepewa nafasi ya viti maalum kwa sababu gani, zaidi ya jina?

Wananchi tukatae hii, kwa kila eneo. Kila mtu asimame kwa merits zake mwenyewe.
 
NaKUBALIANA nawe Mkuu. Naongeza Jina na OFISI ya Bwana kujipatia nafasi. Kwa Mfano huko LINDI ni "nani hajipendi" achukue fomu ya kuchuana na FIRST LADY? GHivyo kujiondoa kwa wagombea "WAZURI" kuliko first lady ilikuwa ni WOGA kwa MKE wa RAIS

Nafikiri hii ndo hoja ya msingi, watu kumhofia mke wa Rais.Na mimi naamini hilo tatizo liko pande zote kwa viongozi na wapiga kura. Swali ni kwa nini watu wanamhofia mke wa Rais. Je, ukishindana na mke wa Rais utashtakiwa? Nadhani kuna mifano mibaya inayowatisha wananchi. Ukishindana na mkubwa unaumia kimya kimya. Japo huwezi kuthibitisha chanzo cha maumivu hayo.
 
Nakubaliana na wewe. Watu wengi hawajui kuwa huko nyuma kupata mgombea ilikuwa kazi ngumu sana ndani ya Chadema. Sasa wale wachache waliojitolea wakati huo leo baada ya Chadema kukubalika ndo watu wanawatuhumu. Siyo sawa.

Mada yangu ni uwepo wa watoto wa vigogo na jinsi walivyoathiri utawala bora nchini.

Kwa hiyo nawe pia unasema kuwa watu wamepewa nafasi kwa sababu za kulipa fadhila? Zaidi ya hapo, hata sababu hiyo haisimami wenyewe. Kina Rose Kamili, Somebody Lissu, nao utawaweka wapi kwenye "waasisi wa chaam"

Tuwe serious walau kidogo. Huwezi ukazungumzia watoto wa vigogo CCM ukaacha kutupia macho kwenye CHADEMA.

Uozo huo uko kwa jamii nzima ya Tanzania. Hakuna aliye mbora hata chembe.
 
Aweda, huyo (MP) Mwnyi, awaombe watz radhi, hawa watoto wa viongozi wetu shule wanazosoma ni tofauti sana na ndg zetu, wao wametengenezwa kuwa watawala na sisi watawaliwa, lkni hata wazazi wao wengi wao bado wako madarakani, hivyo wanachokifanya ni kugawana, wewe kaa hapa..... wewe pale.... na wewe kule, laiti hayo yangefanyika na maisha ya watz yakawa bora, hilo lisingekuwa tatizo, tazama watu walivyochoka... maisha magumu huku wao watawala wanaendelea kuwapa watoto wao nafasi nzuri, just wait.....
 
Hiyo mifano yako inalingana vipi na siasa? Kwani watoto wako wanapigiwa kura kuwa wachumi kama wewe au wanakaa darasani? Unjua kwa nini jamii nyingi zilikataa usultani na ufalme? Ntakwambia ni kwa sababu ya kufanya automativc power transfer ambayo si sahihi! Yule mama na mwanaye wamepita huko walikogombea bila kupingwa wewe mtoto wako alikuwa mchumi bila mtihani? I will be supriesed if you say yes.

Je unajuwa Mwinyi kamfadhili mangapi Kikwete kisiasa na Kikwete asijibu shukrani?

jamaa amekueleza vizuri sana kwamba mtoto hupenda kuiga anachofanya mzazi wake au kile anachokiona kila siku katika maisha yake hususan kinachomvutia.ndio maana watoto wa wachezaji nao wamekuwa wachezaji,masheikh nao wamekuwa masheikh,wachungaji na wanasiasa pia.sasa wewe kwa kuwa unaelewa ila unalazimisha kujifanya huelewi ng'ang'ana hapo.ukweli ndio huo.
 
Kwa hiyo nawe pia unasema kuwa watu wamepewa nafasi kwa sababu za kulipa fadhila? Zaidi ya hapo, hata sababu hiyo haisimami wenyewe. Kina Rose Kamili, Somebody Lissu, nao utawaweka wapi kwenye "waasisi wa chaam"

Tuwe serious walau kidogo. Huwezi ukazungumzia watoto wa vigogo CCM ukaacha kutupia macho kwenye CHADEMA.

Uozo huo uko kwa jamii nzima ya Tanzania. Hakuna aliye mbora hata chembe.

Wote unaowataja wamefanya kazi nzuri sana chadema. Rose inadhaniwa na wengi Hanang kuwa alishinda ubunge akachakachuliwa. Kujustify hilo angalia idani ya madiwani ni nusu kwa nusu. Vivyo hivyo kwa sista Lissu alifanya kazi kubwa. Hoja yangu tusiipindishe. Kwamba hawa watoto wa vigogo ni kweli wamepata hizo kihalali kama anavyodai mh. Mwinyi. Kama sivyo tufanyeje ili mambo yakae vizuri? Maana hata wao wamepita kwenye mifumo iliyowekwa.
 
jamaa amekueleza vizuri sana kwamba mtoto hupenda kuiga anachofanya mzazi wake au kile anachokiona kila siku katika maisha yake hususan kinachomvutia.ndio maana watoto wa wachezaji nao wamekuwa wachezaji,masheikh nao wamekuwa masheikh,wachungaji na wanasiasa pia.sasa wewe kwa kuwa unaelewa ila unalazimisha kujifanya huelewi ng'ang'ana hapo.ukweli ndio huo.

Rais wa Migomo,
Hilo siyo tatizo. Swala langu ni je, hawa watoto wa vigog wote wamepita kihalali?
Unakumbuka habari ya watoto wa vigogo BOT walio na vyeti vya kufoji? Sijui ile habari imeishia wapi?
 
Back
Top Bottom