Uso kwa Uso na Mtikila- Akataa Hongo ya Millioni 100!


Nimelipia kwa makini hili bandiko la tuhuma za mauaji kwa ku fake accidents!, wajameni "karma' is real!, mdomo huumba!. nawaombeni sana wanasiasa na wana jf tuchunge sana kauli zetu!.

Mfano fuatilia hii thread hapa jf
[h=3]Jamaa apata ajali.
[/h]Soma watu walisema nini,


Hivyo wandugu, kauli huumba. Tuwe Makini sana na kauli zetu!. Nilipozungumza na Mtikila kwenye uzi huu, alimzungumzia muuaji fulani anayepanga mauaji kwa ajali, na alimtaja!, kama ni kweli, hiyo 'karma' ya kifo cha Mtikila pia itamkuta!, karma haikwepeki!, lakini kama Mtikila, alimzushia tuu, jambo kubwa kama hili!, then ni kauli ya Mtikila Ndio iliyokiumba kifo chake!.

Tuchunge sana kauli zetu.

Pasco





ikimzungumzia huyu jamaa!, na baada tuu ya wiki, angalia kilichompata!, jamaa huyo huo mkono ni hadi leo!.

Mkuu Pasco mbona kama hauko straight .. kama ulizungumza nae kuhusu muuaji anayepanga mauaji kwa ajali na unaona wazi kifo chake kina utata unashindwa kuunganisha dots?
 
Leo baada ya kushinda kesi yake, na kugomea kukamatwa, nimemkumbuka, na kuipitia tena hii post, huku nikijiuliza kama nimebadili msimamo kuhusu Mtikila, nimejikuta sijabadili, bali insanity yake very unpredictable, sometimes he works for the better, and sometimes he works for the worse!.
P.

Mkuu bado unaamini he was insane?
Mi nadhani ukirejea alichokwambia kuhusu Chadema na CUF kutokuwa wapinzani wa kweli imedhihirika kuwa ni kweli!
 
Mama-Mtikila.jpg


Hiki ndicho ameongea mbele za wanahabari:

Ndugu Wana-Habari,

Kabla sijawaeleza kilichonilazimisha kuwaomba kuongea nanyinyi, kwanza niwarudishe nyuma kama miaka saba iliyopita, ndipo maisha ya Baba, Mchungaji, Mwenyekiti na mume wangu, Mchungaji Christopher Reuben Mtikila yalipoanzwa kuwindwa:-

MAUWAJI YA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE

Mara tu baada ya kifo cha mbunge huyo, mchungaji Mtikila alitoa ripoti maalumu juu ya mauaji yake ambayo ilimjengea uadui kati ya baadhi ya vyama vya siasa pamoja na wafanyabiashara wakubwa ambao hadi leo ni wapinzani wa serikali hapa nchini.--Mchungaji Mtikila hadi anafikwa na mauti aliendelea kupata upinzani wa aina hiyo hiyo kwa sababu mchungaji Mtikila aliendelea kudai haki ya marehemu Chacha Zakayo Wangwe.

MAUAJI YA BULIGI

Hii ilimwongezea uadui baada ya kusema/kuandika ukweli juu ya watutsi wa nchi jirani kuvamia nchi yetu kwa mtindo wa kujifanya wafugaji wasio hama. L.I.F. ilibaini uharamia huo kuwa hawakuwa wafugaji bali walikuwa askari wa Jeshi la Rwanda waliokuwa na mpango wa kutumika na Chama kimoja cha siasa hapa nchini ili kuleta mapigano yatakayo zaa mapinduzi. Jambo hili lilisababisha Rais wa Rwanda, Paulo Kagame kutamka hadharani kuwa angemkamata Mwenyekiti wa chama chetu cha DP--kwa lengo la kumuua na Serikali yetu inajua hilo. Mara baada ya ripoti hiyo kutolewa na Mchungaji Mtikila "operation Kimbunga" ilizaliwa na kuponya nchi yetu; lakini chuki na uadui uliendelea dhidi ya Mchungaji Mtikila.

MCHAKATO WA URAIS NDANI YA CCM

Ikumbukwe kuwa mara baada ya mchakato wa kutafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM kuanza DP ilitoa ripoti iliyowahusu wagombea sita wa CCM waliotumia mapesa mengi na kuanza kampeni kabla ya muda na kusisitiza kuwa Lowasa ni mtu asiefaa kuwa Rais wa nchi yetu. Na baada ya kuhama CCM, Mwenyekiti wetu aliendelea kutoa tahadhari hadharani jinsi Lowasa asivyofaa kuwa Rais wa nchi yetu hivyo likaendeleza uadui wake na Chama.

VITISHO--KUANZA

Mchungaji Mtikila alipata nafasi ya kuongea katika kipindi kinachorushwa na STAR TV cha asubuhi "TUONGEE" ndipo alipoanza kupata vitisho toka kwa watu mbali mbali wengine kupitia kwenye simu wengine uso kwa uso. Kipindi cha kwanza kilirushwa tarehe 25/9/2015 na kufuatwa na cha tarehe 27/9/2015. Alipotoka studio hiyo asubuhi ya tarehe 27/9/2015 ndipo watu waliodai wametumwa na Mhe. Edward Ngoyai Lowasa na Mhe Frederick Sumaye walimuomba wampe nusu bilioni na apewe maovu ya mgombea urais wa CCM ili afunike-alivyowamaliza wao.

Mchungaji Mtikila aliwapuuzia mbali wale wajumbe waliyotumwa kwani aliawaambia kuwa yeye siyo malaya wa kuuza utu wake kwa tende na haluwa. Yakumbukwe kuwa mahojiano kwenye hivyo vipindi viwili kwenye STAR TV hayakuwa yanatetea mtu au chama yalikuwa yanatetea Taifa letu lipate Rais anayefaa.

Kwa hiyo basi wale waliochukizwa na mahojiano hayo ni wale amabo hawakubaliani na mawaidha ya Mchungaji Mikila aliyokuwa anawatahadharisha watanzania juu ya Mh. Lowasa kuwa hatari kwa usalama wa taifa letu kama atakuwa Rais wa nchi yetu. Hao watu ndiyo waliopanga mpango mzima wa mauaji ya Mh. Mtikila ambaye ni mume wangu.

Wakati yuko Bunda mjini watu wasiofahamika walimfuatafuata na tarehe 26/9/2015 gari lake lilifukuzwa na gari usiku wakati alipokuwa anatoka Bunda kwenda Mwanza kufanya mahojiano ya tarehe 27/9/2015 na Star Tv.

MPANGO WA MAUAJI HALISI

Mchungaji Mtikila alitafutiwa gari na Victor James Manyahi ambayo ilikuwa na madereva wawili. Mchungaji madereva hakuwajua. Hata mimi madereva hao sikuwajua wala sikuwaona. Walikodiwa kutoka wapi sijui, wala sijui wanafanana vipi. Na wala sijui Victor Manyahi alikodi gari hilo kwa nani na makubaliano yepi sijui.

Kwa hivyo basi, kwenye gari aliyosafiri nayo Mchungaji Mtikila kulikuwamo madereva wawili na Mgaya Patrick (tunayemfahamu). Wakati wanakwenda gari lilipata ajali Makambako. Wakati wanarudi wakapata “ajali” Msolwa Mchungaji akapatwa na mauti peke yake. Ajali ilikuwa mbaya sana-IKAUWA MTU MMOJA AMBAYE NI MCHUNGAJI MTIKILA NA HAKUKUWA MAJELUHI HATA MMOJA.-Cha ajabu kwangu ni kuwa mtu ambaye alikuwa ni mlinzi wa kujitolea (body guard) Mgaya Patrick sijawahi kumuona usoni mwangu kabla na hata baada ya mazishi kuja kuniambia kilichotokea eneo la ajali. Pamoja na juhudi zangu zote za kumpigia simu mara kadhaa aje anijuze Mgaya Patrick hajatokea hadi sasa ndugu zangu wanahabari ninapoongea nanyi. Lakini si kwamba huyu mtu hayupo, yupo lakini sijaonana naye, kwa nini sijui. Je ndugu zangu wanahabari nimuweke Mgaya Patrick kwenye fungu gani?

Ndugu Wana-Habari, baada ya kuwaelezea yote hapo juu nakuja kwenye suala nililowaomba nikutane nanyi ili niongee mbele yenu kuwa sikubaliani na uchunguzi kuwa Mchungaji Christopher Reuben Mtikila amekufa kwa ajali. Sikubaliani na kazi ya Polisi kuwa wamefunga file lao kutokana na Post-mortem report kuwa mauti yaliotokana na ajali. Nafuta kabisa taarifa--iliyotoka katika gazeti la Nipashe chini ya kichwa cha habari kuwa “FAMILIA YAFUNGUKA KIFO CHA MTIKILA”-ilitolewa mapema mno. Kila mwanafamilia alikuwa hajawa tayari kutoa kauli yoyote. Kwa niaba ya Chama na familia ya Mchungaji Christopher Reuben Mtikila naomba tusaidiwe yafuatayo kusudi haki ya mpendwa wetu-ionekane--inatendeka:-

Kwa sababu mtandao umeanza kuficha ukweli ili kulinda wauaji; tunaomba Mheshimiwa Rais aingilie utata wa kifo cha Mheshimiwa Mchungaji Christopher Reuben Mtikila kwa kuunda tume ya uchunguzi isiyohusisha polisi.

Tunaiomba mamlaka ya mawasiliano yaani Tanzania Communications Regulatory Authority, TCRA itusaidie yafuatayo:-

(a)----Mtu aliyeweka picha kwanza alfajiri kuonyesha mauti ya Mhe Mchungaji Mtikila alikuwa wapi? Kwenye tukio? Au ni hao wauaji walikuwa wanatoa taarifa kwa waajiri wao kuwa wamekamilisha kazi!

(b)----Mtu aliyeweka picha ya Dr. Jean-Bosco Ngendahimana kwenye mtandao kuwa ndiye anahusika na mauti ya Mhe. Mch. Mtikila na kumusingizia kuwa amekamatwa na polisi akiwa anajiandaa kukimbia;

(c)-----Wote wanaoendelea kumhusisha Dr. Jean-Bosco Ngendahimana na mauaji ya Mhe. Mchungaji Mtikila, tuwafahamu ili watueleze vizuri.

Ukweli na haki ni vya Mungu hakuna anayeweza kuviua au kuvizuia. Tunategemea Mungu atawatumia watendaji wa Serikali/nchi yetu wenye nia njema, na makusudi yaliyonyooka kwa ajili ya nchi yetu ili Mhe. Mchungaji Mtikila apewe haki dhidi ya wauaji wake.

Asanteni,

Georgia C . Mtikila,

-KM DP/Msemaji-Familia

Georgina you're good for nothing as was your husband Mtikila

Kumbe kichaa cha marehemu kilikuwa kinaambukiza!!

Akamfufue mme wake basi! Am sorry to say this ila huyu mama inabidi apimwe akili zake kwanza kama Yuko sawa
Mbona mama wenyewe anaonekanika kama kichaa!!!ccm wanafufua hadi wafu trip hii!!

Masikini huyu Mama, kumbe ni kweli ukiolewa na mtu, mkaishi kwa muda mrefu, then mke na mume hatimaye mnakuwa mmefanana!. Kwa wale ambao hamkuusoma uzi huu, Uso kwa Uso na Mtikila- Akataa Hongo ya Millioni 100! - JamiiForums
Katika pita pita zangu mchana wa leo jiji Dar es Salaam,

Nimekutana na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila katika ofisi fulani, yeye kaja na yake, nami na yangu hivyo tukaa waiting room pamoja kumsubiria mwenyeji wetu.

Na baada ya maelezo yote haya ya kukataa hongo ya milioni 100!, Mchungaji Mtikila alimalizia kwa ...(nakihifadhi) ili ndio uthibitisho kuwa he is not normal!.

My Take.
Mtikila is insane. Ningekuwa ni mwandishi wa habari, hayo aliyoyasema nikayaandika gazetini na majina yao, kesho yake mimi na gazeti langu tungeishia mahakamani for defamation!.


Pasco

upitieni tena, mlinganishe kile Mtikila alichonieleza, na hiki mkewe anachoeleza!, they are both insane!.

Baada ya kunieleza jinsi alivyokataa hongo ya milioni 100!, kuna kitu aliniomba, kwa heshima sikukitaja, na wala sikitaji, bali tuendelee tuu kumuombea Mungu ampumshishe kwa amani kwa sababu hata insane, ana haki!.

RIP Mchungaji Mtikila.

Pasco
 
Wandugu kwa tamaduni zetu Waafrika,mtu akishatangulia mbele ya haki si vema kuanza kumjadili na kumkandia mapungufu aliyokuwa nayo badala yake tumuombee ili Mungu Mwenyezi amsamehe dhambi zake;hivyo binafsi sijafurahishwa na majadiliano haya hebu tubadilike.
 
Mkuu Pasco naona ni ngumu kumeza hii kitu kwanza kabisa utaNegotiate vifo uhai wako na mtu ambae anataka kukuua tena unaenda hadi nyumban kwake.
Nikikua nataka kusema kitu ila kwa heshima za wafu namstiri tu.
 
Last edited by a moderator:
Leo baada ya kushinda kesi yake, na kugomea kukamatwa, nimemkumbuka, na kuipitia tena hii post, huku nikijiuliza kama nimebadili msimamo kuhusu Mtikila, nimejikuta sijabadili, bali insanity yake very unpredictable, sometimes he works for the better, and sometimes he works for the worse!.
P.
Hapa ndipo ulipokosea . He was not insane ila kisaikolojia ni wale watu ambao kujaza upepo na kutafuta uchokonozi ili apasuke vzr

Ni kama aina Fulani ya wanafunzi ambao huwa na details za kuhusu makosa flan afu wanakosa wa kuwa uliza una jipya Gani? Na hivyo kupeleka wao kutafuta mtu wamsimulie tuu ili kuchokonoa
 
Mkuu Pasco naona ni ngumu kumeza hii kitu kwanza kabisa utaNegotiate vifo uhai wako na mtu ambae anataka kukuua tena unaenda hadi nyumban kwake.
Nikikua nataka kusema kitu ila kwa heshima za wafu namstiri tu.
Hakua anaenda kichwa kichwa nadhan kuna vitu alikua anafanya kama vile kuomba ulinz wa polis na ndio maana unaona kuna sehem amekiri kwamba aliwah kutoa taarifa polis

Haya huyo aliyekuwa anamuita ninaamin kbs hakuwa na gut za kumaliza juu kwa juu manake alikuwa anajua yupo kwenye list yake ya serial killers na hajui taarifa zake zimefika wapi.

Nafikir kama alikua anaanda jins ya kumuua lazima angetumia mbinu clean kabisa kukwepa mikono yake kushukiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kma kuna watu ambao taifa hili haliwezi kuja kuwaelewa kwa miaka hii ya karibuni ni Mtikila. wengi mtasema ni kichaa lakini Mtikila alikuwa na akili nyingi sana mpaka kupitiliza.na kumuelewa ilibidi kwanza uwe na ukaribu wa akili zake bila hivyo uta conclude kirahisi kuwa ni insane. lakini kuna mambo aliwah kuyasema na yakawa.
 
Duuuh! gari inapinduka mara ya kwanza bado unarudi tena na gari ulikotoka,kwanini marehemu asingetumia hata public transport?
 
Sio ule waraka wa PaKa amepenyeza wanyarwanda i.e watutsi hapa tz 35,000 maana PaKa alimwitaga yeye ni dog. Naanza kuwaza labda ni wale wale waliomfetua risasi prof Jwani Mwaikusa maana huyu professa naskia baada ya kumtetea mnyarwanda mmoja mpaka akaachiwa huru PaKa aliapa kumtoa duniani. I hope na kifo chake kina baraka ya ile nchi ndogo maana hawa jamaani ni kwere

Nakumbuka nilifundishwa ukitaka kuwatambua hawa watutsi wana pua za kizungu na sura nyembamba na wengi wao wako kama wa-ethiopia ni hatari sana
 
Wanabodi,

Update:
5 years later, 4 October 2015
Kauli Huumba!, RIP Mchungaji Christopher Mtikila!.

Nisamehe kwa yote!.

Paskali
Unanikumbusha kifo cha mch Mtikila. Mazingira ya kifo chake kilichotokana na ajali yalinifikirisha sana, tena ajali ilitokea katika kipindi ambacho Mtikila alikuwa moto sana.
Ila ndo hivyo watu walizika na maisha yakaendelea.
Mkuu Mr Dudumizi , hapa kwenye kifo cha Mchungaji Mtikikila, umenikumbusha kitu!. Kiukweli haya mambo ya ajali za ajabu ajabu hii njia ya Dar Chalinze, na maeneo ya Tanga kwenye 'fundi' wengi, kumbe pia it's possible ajali zote sio ajali tuu, ajali nyingine ni 'ajali'. Kuna siku nilikutana na Mchungaji Mtikila mahali, akazungumzia mtu anayeuwa watu kwa ku fake accident Uso kwa Uso na Mtikila- Akataa Hongo ya Millioni 100! five years later Mchungaji Mtikila alikuja kufa kwa ajali ambayo ilikuwa ni kama a fake accident!.

Hivyo kuna ajali zinatokea zinakuwa ni ajali tuu na kuna ajali sio ajali tuu, ni 'ajali'
RIP Balozi Mushi!.
P
 
Mkuu Mr Dudumizi , hapa kwenye kifo cha Mchungaji Mtikikila, umenikumbusha kitu!. Kiukweli haya mambo ya ajali za ajabu ajabu hii njia ya Dar Chalinze, na maeneo ya Tanga kwenye 'fundi' wengi, kumbe pia it's possible ajali zote sio ajali tuu, ajali nyingine ni 'ajali'. Kuna siku nilikutana na Mchungaji Mtikila mahali, akazungumzia mtu anayeuwa watu kwa ku fake accident Uso kwa Uso na Mtikila- Akataa Hongo ya Millioni 100! five years later Mchungaji Mtikila alikuja kufa kwa ajali ambayo ilikuwa ni kama a fake accident!.

Hivyo kuna ajali zinatokea zinakuwa ni ajali tuu na kuna ajali sio ajali tuu, ni 'ajali'
RIP Balozi Mushi!.
P
Asante mkuu Pascal Mayalla kwa hakika ukiangalia mazingira ya baadhi ya vifo vya viongozi wetu mbali mbali vinavyotokana na ajali mbali mbali, utaona kwamba kuna kitu kinakuwa nyuma ya hizo ajali.

Na kwa vile victim wa ajali hiyo anakuwa ni mtu asiekuwa na mamlaka makubwa ndani ya nchi basi vifo hivyo au ajali hizo huachwa hivyo hivyo bila kufanyiwa uchunguzi wowote wa kina na mamlaka husika.

RIP marehem balozi.
 
Mkuu Mr Dudumizi , hapa kwenye kifo cha Mchungaji Mtikikila, umenikumbusha kitu!. Kiukweli haya mambo ya ajali za ajabu ajabu hii njia ya Dar Chalinze, na maeneo ya Tanga kwenye 'fundi' wengi, kumbe pia it's possible ajali zote sio ajali tuu, ajali nyingine ni 'ajali'. Kuna siku nilikutana na Mchungaji Mtikila mahali, akazungumzia mtu anayeuwa watu kwa ku fake accident Uso kwa Uso na Mtikila- Akataa Hongo ya Millioni 100! five years later Mchungaji Mtikila alikuja kufa kwa ajali ambayo ilikuwa ni kama a fake accident!.

Hivyo kuna ajali zinatokea zinakuwa ni ajali tuu na kuna ajali sio ajali tuu, ni 'ajali'
RIP Balozi Mushi!.
P
Mushi,eti balozi akose hata chawa wa kusafiri nae,kipindi hiki ambacho machawa ni wengi... R.I.P,inatikirisha,hasa ukizingatia na tuhuma za Austria,duuh!
 
Asante mkuu Pascal Mayalla kwa hakika ukiangalia mazingira ya baadhi ya vifo vya viongozi wetu mbali mbali vinavyotokana na ajali mbali mbali, utaona kwamba kuna kitu kinakuwa nyuma ya hizo ajali.

Na kwa vile victim wa ajali hiyo anakuwa ni mtu asiekuwa na mamlaka makubwa ndani ya nchi basi vifo hivyo au ajali hizo huachwa hivyo hivyo bila kufanyiwa uchunguzi wowote wa kina na mamlaka husika.

RIP marehem balozi.
Sio tuu hatufanyi uchunguzi bali unaweza kukuta na ajali hizo ni eneo hilo hilo, kijiji hicho hicho, and at the same same spot!
Eneo la kijiji cha Panda Mbili, ndipo alipopatia ajali Chacha Wangwe, alikuwa anajiendesha mwenyewe, akampa lift abiria Deus Malya, akajitambulisha ni dereva ana leseni ya Class C!, akajitolea kumuendesha!. Ikatokea ajali, gari ikapinduka, Wangwe no more yeye without scratch!. Alipoulizwa na polisi ajali imetokeaje akashindwa kunyoosha maelezo!. The same place, same spot Salome Mbatia akapata ajali hapo hapo and she was no more!. Na mimi nikaja kupata ajali hapa hapo na ile boda boda yangu!. Zikitafutwa data za zimetokea ajali ngapi zilizopoteza maisha ya watu, you might be surprised!. Halafu usikute kijijini hapo kuna bonge la "fundi'', sometimes inahitajika kucha tuu ya kidole kidogo cha mguu wa kushoto!, linapinduliwa basi zima!.

P
 
Wanabodi,

Katika pita pita zangu mchana wa leo jijini Dar es Salaam, n
imekutana na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila katika ofisi fulani muhimu sana ya umma, yeye kaja na yake, na mimi nimekwenda na yangu, hivyo tukaa waiting room pamoja facing each other, tunaangaliana huku tunamsubiria mwenyeji wetu.

Kwanza kwa ule Utanzania wetu na Uafrika wetu wa kawaida mtu ukifika mahali na ukakuta watu, its normal kuwasalimia ndipo unakaa!, Mchungaji Mtikila aliingia tuu na kukaa huku tunaangaliana!, hata habari hakuna!. Kwa vile yeye ni public figure, na ninamfahamu, hivyo ni mimi ndio nikawa wa kwanza nikamsalimia "shikamoo Mchungaji Mtikila". Ile tuu kumsalimia kwa kumtaja jina lake, huwezi amini alinijibu alinichangamkia sana na tukaanza kuchat.

Kwanza nilimuuliza kwa nini wapinzani hawaungani?.
Jamaa alishusha nondo nzito kwa kubonda wapinzani wote kuwa Tanzania, hakuna mpinzani yoyote isipokuwa ni yeye tuu!, tena kuhusu Chadema, ndio usiseme kabisa, eti ni afadhali ya CCM kuliko Chadema!. Alisema mengi mabaya kuhusu Chadema kwa lugha kali na matukano kibao, huku akizungumza kwa sauti ya juu, ofisini kwa watu!.

Nikamsisitizia, kwa vile chama tawala ni CCM, vingine vyote ni upinzani, jee haoni kuikandia Chadema na CUF at this time ya kuelekea uchaguzi mkuu ni kuikampenia CCM kwa mlango wa nyuma?, au ameshikishwa kidogo dogo?!.

Jamaa aliwaka sana akasema CCM imshikishe nani pesa, ndipo akasema "hapa nilipo, japo sina pesa ila nimekataa hongo ya milioni 100 sasa hivi! toka kwa fulani na akamtaja jina (naomba nilihifadhi hilo jina ili kuilinda hadhi na heshima ya JF, kutokana na nature ya tuhuma zenyewe, maana huyu mtu niliyetajiwa, kwa humu JF, ni "mtakatifu fulani" sana humu jf, na ni mmoja wa waheshimiwa wetu kitaifa, hivyo anaheshimiwa sana tuu humu jf).


"Niligundua kuwa ... (akamtaja) ni muuaji, anatoa pesa kutuma assassins kutekeleza mauaji mbali mbali na kisha kufake accidents!, alitoa shilingi milioni 120 kuwapa Wakenya fulani wawili kumuua ...(akamtaja..), ushahidi ninao!.

Mtikila akaendelea kudai kuwa, Mfanyabiashara huyo tajiri alipomgundua siri yake ya mauaji kwa ku stage accidents imefichuka, kwanza alimuita kwenye (Mtikila) kwenye moja ya vitega uchumi vyake (akataja kitegauchumi hicho, mahali kilipo, siku na saa) akampa offer ya hongo ya Sh. Millioni 10 ili afute jina lake kwenye dossier ya wauaji. Mtikila akamkatalia.( Akimaanisha analo andiko hilo la mauaji!).

Mara ya pili (tajiri) huyo alimuita ofisini kwake, (akataja siku, muda na ofisi ilipo!) akapanda dau toka ile milioni 10! mpaka milioni 50!, bado Mtikila alizikataa!. Ndipo tajiri huyo akamuita Mtikila nyumbani kwake (akataja siku, muda na eneo nyumba ilipo!) akampa offer ya Sh. Millioni 100!. Ndipo Mtikila alimkubalia kwa shurti ya tajiri huyo, kwanza akiri dhambi zake za mauaji, na pili atubu kwa Mungu kwa kupiga magoti kutubu kwa, Mungu mbele yake, akishamsamehe na Mungu, ndipo na yeye Mtikila, atamsamehe na ataipokea hiyo pesa kama asante yake!.
.
Tajiri akagoma kukiri makosa ya mauaji na akagoma kutubu!. Ndipo Mtikila akasimama akatoka nje!, ila anadai kila kitu amerekodi kwenye digital sound recorder yake, na sasa anasubiri tuu time muafaka ili amlipue!, na kudai ameisharipoti polisi ili na yeye asije kufa kwa staged accident!.

Ila pia Mtikila alikiri kupokea kitita cha fedha, milioni kadhaa kutoka kwa Rostam Aziz, akisema ni kweli nilikuwa na shida, nikaenda kukopa, ila nilipozipata fedha za kulipa, nilimpelekea Rostam ili nimlipe, Rostam akakataa kuzipokea kwa hoja kuwa amemsaidia tuu, hivyo deni ameshalipa sasa zimegeuka sadaka!.

Nikamuuliza yeye kama mtu wa Mungu, na ni kiongozi wa upinzani, na anajua wazi ufisadi wa Rostam, na mtu wa CCM, anakwendaje kwake kukopa, hivi hizo sio sehemu ya pesa chafu za Kagoda?. Alijibu kuwa mtu ukiwa na shida, unakwenda kukopa popote kwa yeyote mwenye pesa, hata kwa adui yako, ili utatue shida yako. Akasema pesa hata ziwe chafu vipi, zimeibiwa au za madawa ya kulevya, ukizitumia kutenda wema kama alivyofanya yeye, then pesa hizo zinakuwa zimesafishika na kutakasika, hivyo ni pesa safi kwa sadaka!.

Na baada ya maelezo yote haya ya kukataa hongo ya milioni 100!, Mchungaji Mtikila alimalizia kwa jambo moja la ajabu ...(naomba nilsilitaje, ili kumlindia hadhi yake) ili jambo hilo ndio uthibitisho kuwa he is not normal!.

My Take.
Ukimsikiliza kwa karibu, Mchungaji Mtikila is kama insane fulani hivi!. . Ningekuwa ni mwandishi wa habari wa magazeti, hayo aliyoyasema Mtikila nikayaandika gazetini na majina yao!, kesho yake mimi, mhariri wangu na gazeti langu tungeishia mahakamani for defamation!.


Pasco

Update:
5 years later, 4 October 2015
Kauli Huumba!, RIP Mchungaji Christopher Mtikila!.

Nisamehe kwa yote!.

Paskali
Alikufa Kwa aina ya kifo kilekile alichokutajia swali he ilikuwa faked accident? Na vipi kuhusu taarifa alizotoa polisi kuwa anatishiwa maisha.
 
Sio tuu hatufanyi uchunguzi bali unaweza kukuta na ajali hizo ni eneo hilo hilo, kijiji hicho hicho, and at the same same spot!
Eneo la kijiji cha Panda Mbili, ndipo alipopatia ajali Chacha Wangwe, alikuwa anajiendesha mwenyewe, akampa lift abiria Deus Malya, akajitambulisha ni dereva ana leseni ya Class C!, akajitolea kumuendesha!. Ikatokea ajali, gari ikapinduka, Wangwe no more yeye without scratch!. Alipoulizwa na polisi ajali imetokeaje akashindwa kunyoosha maelezo!. The same place, same spot Salome Mbatia akapata ajali hapo hapo and she was no more!. Na mimi nikaja kupata ajali hapa hapo na ile boda boda yangu!. Zikitafutwa data za zimetokea ajali ngapi zilizopoteza maisha ya watu, you might be surprised!. Halafu usikute kijijini hapo kuna bonge la "fundi'', sometimes inahitajika kucha tuu ya kidole kidogo cha mguu wa kushoto!, linapinduliwa basi zima!.

P
Nimependa zaidi hayo maneno 👇

Halafu usikute kijijini hapo kuna bonge la "fundi", sometimes inahitajika kucha tuu ya kidole kidogo cha mguu wa kushoto!, linapinduliwa basi zima!,

😂🤣🤣 Nimejikuta nacheka kwa sauti bila kutegemea, kama vile yanayotokea ni mazuri. Mungu atunusuru kwa kweli.
 
Back
Top Bottom