Usiwe na haraka unapohitaji mpenzi wa kweli mtandaoni.

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,723
9,189
Kutafuta mpenzi mtandaoni ni suala ambalo linaonekana la ajabu mbele ya akili za watu. Ajabu zaidi ni pale unapotaka jambo hilo lifanikiwe ndani ya siku hiyo hiyo.
Watu tunaoingia mitandaoni ndio sisi sisi tunaoishi mitaani.
Mitandaoni ni namna nyingine ya kuonana na watu ingawa sio ana kwa ana.
Najua humu wapo watu single wanaojiheshimu na ambao wangehitaji mume/mke wa ukweli lakini namna ya kufikisha hitaji lao huwa ni utata, wengine hufikiria wataonekanaje, wengine huofu endapo hawatofanikiwa lengo lao watakuwa wamepoteza muda.
KWA WANAUME:
kama ungependa kupata mchumba JF usifanye haraka. Humu tunajuana kwa michango tunayotoa. Kwa kiasi fulani unaweza kujua fulani ana tabia fulani inayokuvutia. Jaribu kujenga mazoea. Unaweza kumuadd as a friend then ukawa unaMPM kumsalimia, akitoa threads zake changia kadri uwezavyo, ukimkosa online kwa siku kadhaa kavisit profile yake. Akirudi ataona jina lako ni mmoja wa aliyevisit profile lake.
Hayo yote ni kujenga ukaribu na kumjua vizuri mwenzio kabla hujaamua kurusha ndoano.
UkiMPM epuka kumdadisi sana mambo yake binafsi, epuka kutanguliza namba ya simu katika hatua za awali na epuka kuongelea mapenzi.
Kama kweli una nia usikurupuke. Ukikurupuka hata sisi tunastuka.
NB: sijamaanisha mtu anayefanya niliyoyataja anatafuta uchumba.
Nawasilisha.

Ni kweli usemayo japo kuna wengine watayapiga ila penye nia pana njia! nawajua watu kadhaa waliokutana kwenye mitandao na wamefunga ndoa na wanafurahia life yao...
Kila la kheri kwa wanatafuta :smile-big::smile-big:

Hehehhe ngoja nianze kufuatilia waliotembelea profilelangu usikute mume mtarajiwa hua anaangalia kila nikikosekana!!!

Husninyo ushauri mzuri kweli.....binafsi mtu anaetafuta jamvini hata kama nakidhi vigezo siwezi kumPM nimwambie mimi nna unayotaka!!Kwahiyo angalieni wale wanaowavutia kimawacho (michango) tngenezeni mazoea nahuko mbeleni mkishajuana vizuri ndo unaangalia kamaanakufaa na wewe unamfaa mnaweka mambo sawa!!

Asante Husninyo,naamini hizo zote ulizotaja ni njia bora sana za kupata uhusiano mzuri kuliko ile ya kuanzisha thread,hata hivyo naanza na ww.......lol

nawajua watu kadhaa waliokutana kwenye mitandao na wamefunga ndoa na wanafurahia life yao...
Kila la kheri kwa wanatafuta :smile-big::smile-big:

wapo watu wengi tu wanakutana mtandaoni na wanadumu. Kikubwa ni namna mtavyokutana. Ukitaka mambo ya fasta fasta utaibuka na mtu wa ajabu. Lol!

Ha ha ha we mchokozi yaani yaani tangu nikwambie shem wako nilimpata hapa imekuwa taabu...umenirusha live haya bana...

Ha ha ha we mchokozi yaani tangu nikwambie shem wako nilimpata hapa imekuwa taabu...umenirusha live haya bana...

Husninyo ushauri mzuri kweli.....binafsi mtu anaetafuta jamvini hata kama nakidhi vigezo siwezi kumPM nimwambie mimi nna unayotaka!!

wengi hatuwezi kumPM. Mbaya zaidi unapoenda kucheki profile yake unakuta kajoin leo.

Asante Husninyo,naamini hizo zote ulizotaja ni njia bora sana za kupata uhusiano mzuri kuliko ile ya kuanzisha thread,hata hivyo *naanza na ww.......*lol

hahaha! Unaanza na mimi. Mmh! Msimgeuzie kibao mwalimu wenu.
Mwalimu amewapa maujanja tu.

Ha ha ha we mchokozi yaani tangu nikwambie shem wako nilimpata hapa imekuwa taabu...umenirusha live haya bana...

afadhali utuambie mlianzaje anzaje ili wenzio 2sikurupuke. Lol!
Au ndio yule alikuanzishia sred. Hahahaha!

afadhali utuambie mlianzaje anzaje ili wenzio 2sikurupuke. Lol!

Au ndio yule alikuanzishia sred. Hahahaha!

Acha kuyeyusha mbele za watu unajua kila kitu km umesahau ngoja nikuforwadie PM yako

hahaha! Unaanza na mimi. Mmh! Msimgeuzie kibao mwalimu wenu.
Mwalimu amewapa maujanja tu.

kuanza na mwl.si mbaya ili kumwonyesha kuwa somo limeeleweka..lol! Hili la kucheki watu wa kny profile nimecheka sana maana nimeliona wengi wanakuwa wageni!!!!!!

Hii thread ina relate na aliyoleta Ruta " Hatari za kufanya mapenzi na mtu usomjua". You need time to study your online partner asijekuwa serial killer!

teh teh teh! Si unoko Dena ntazingatia alichosema huyu binti wa mpwapwa ili tufahamiane kdg

Wewe hebu twende chumbani watoto bado hawajalala...acha hizo bana nini lkn na wewe bama.,?

Back
Top Bottom