Usitegemee ukweli kutoka kwa Dk. Steven Ulimboka!!

Ukweli huo unatosha kwenda Mahakani?!

Hapo penye maandishi mekundu ndio wapi?
By the way kumbuka kwamba, kama wewe ni mwoga, mwenzako si mwoga katika kutetea kile anachoamini kwamba ni sahihi. Ndio sababu sisi wengine tulio sekta binafsi tumekomaa na serikali (SSRA) ili warekebishe sheria ya mafao. Huwezi kusikia mfanyakazi wa serikali akiilalamikia sheria ile kandamizi kamwe! Hao usalama unaowahofia na wenyewe ni waathirika wa mishahara midogo, ndio sababu wanavujisha mambo mengi sana ya kiofisi katika vyombo vya habari, ili tujue kinachoendelea. Kumbuka kwamba, hao unaowahofia:-
-Wanaathirika na mgao wa umeme kama mimi na wewe
-Wanaathirika na kupanda kwa bei za mafuta na vyakula kama mimi na wewe
-Wanauguliwa na Wanafiwa na ndugu zao kama ilivyo kwangu na kwako
-Huwa wanastaafu utumishi wa umma na kuendelea kusotea mafao yao kama wengine
-Watakufa kama ilivyo kwa mwanadamu yoyote yule
Nadhani nimeeleweka. Ondoa uoga

 
Back
Top Bottom