Usishabikie tu, tafakari kisha pima

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
1,467
513
Sote tunashabikia ushindi au kuanguka kwa wagombea mbalimbali wa ubunge. Ni kweli kesi hizi zina time limit na serikali iliingia kibindoni ili kesi hizi zisikilizwe. Kweli siasa imetukuzwa na ndo maana hata wataalam wetu wanakimbilia huko. Je unajiuliza ni mahabusu wangapi walioko katika magereza yetu kwa zaidi ya hata miaka kumi na kesi zao hazijasikilizwa? Ni upuuzi tu. Na ndo maana wanasiasa wanajilipa vizuri, wanatuibia, hatufanyi kazi tunawazungumzia wao, kila kawa mwandishi wa habari wa kutafuta na kusoma habari zao.Laiti tungalijua gharama kubwa tena isiyo na tija ya wanasiasa wetu hawa, hawa watu wa longolongo, wajanjajanja, miungu watu, wala vya haramu hawa. Haingii akilini msomi kama Shivji akifundisha na kulipwa kiduchu anatokea mtu kama maji marefu au lusinde analipwa zaidi ya mil 7 na hadhi ya uheshimiwa, diplomatic paspot etc. Ni upuuzi tu!
 
Na ndio maana nitaendelea kusema.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Back
Top Bottom