USIRI WA LOWASSA huu hapa!

kumbe rais ajae anatoka ccm?

Ndo maana nguvu nyingi inatumiwa na baadhi ya watu kuhakikisha wanajitakasa ndani ya chama chao. Siye tulio huru, wanasema haiwezekani kugombea madaraka
 
Kama sio hili tishio la Alshabab ningetafuta watu wa aina yako ili tuone namna tutakavyokwenda Airpot kumpokea Lowasa kwa kushinda vita!!! HAKUNA KAMA LOWASA Yeye akisikia kunauchaguzi achukue Form tu kura zipo wazi, nchi hii ikikosa mtu kama Lowasa ni afadhali tujaribu Jeshi maana uswahili umezidi
yaani ww ndo wazimu kamili lete kiboko upate 5 pap
 
Stop this crap! Lowassa would never be a president of this nation! Tumechoka na hii Lowassa's sycophancy! Lowassa amepata nguvu kwa kujua Mwakyembe hayupo kusema ukweli wote.

Let us pray for the return of Mwakyembe... Fisadi ni fisadi na hatuwezi kujaribu maisha yetu kwa kumpa fisadi nchi! Tanzania ina watu wazuri na waadilifu, hatuwezi ku-recycle mafisadi!

Nanukuu hotuba ya mwakyembe alipo kuwa akiwasilisha ripoti iliyokuwa ikuchunguza mambo ya richmond alisema haya ni machache mengine tumeacha kuyosoma hapa kwa maslahi ya usalama wa taifa letu! Hapo ndio siri nzito ilipo. Hapo penye maslahi ya usalama wa taifa letu kuna rais ndani yake tusiwe na haraka utayajua mengi tu, ukimtafakari jairo na ugumu uliopo wa kung'oka wizara hiyo utajua siri nyingi zipo pale.
 
.... namnukuu EL, " kama shida ni UWAZIRI MKUU, basi..."
:embarassed2:

hakufanya home work ya kutosha kuwadadavulia wa Tz wakati ule au anamlazimisha JK ajitoe mhanga kwa kuueleza umma wa Tz kuwa yeye JK "alimpotosha" EL katika maamuzi. Ni sawa EL ni mtendaji mahili sana - hilo waa tu ndo soo.
 
Ndugu zangu nianze kwa kusema mi sina undugu na Lowasa wala sifahamiani naye zaidi ya kumwona kwenye vyombo vya habari lakini nimekuwa na IMANI naye kubwa tangu zamani na nimekuwa nikiwaeleza watu uzuri na faida ya lowasa kwa taifa letu,wengi wamekuwa wakionesha kumkubali ila wanadai ni fisadi jambao ambalo hawawezi kuthibitisha.

Sasa ninashukuru Mungu lowassa amechukua ushauri wangu wakueleza ukweli KWAMBA YEYE SI GAMBA kwani alimshauri raisi mapema kabisa kwa kuuvunja mkataba wa Richmond lakina raisi akakataa kwa kisingizio makatibu wakuu wamemkataza.sasa Gamba ni nani? Hapa,je? Ni raisi aliyeukingia kifua au makatibu wakuu?,mi naona mungu ameamua kuikomboa TANZANIA.nianze kueleza faida za lowassa kuwa raisi wetu 2015.

1. Lowassa ni mchapa kazi tunaona namna alikuwa akitenda wakati akiwa waziri alikuwa akiwa na ziara mkoani kila mtu alikuwa anajiaanda mpaka makondakta walikuwa wanavyaa sare, nchi ilikuwa inahofu katika uwajibikaji lakini tangu amekuja kipenzi cha watanzania mtoto wa mkulima mzee wakulia na mzee asiyona maamuzi kazi yake ni kuomba tu ili hali anamamlaka ya kikatibu, hivyo dhana ya uchapakazi kwetu inatija kwanchi yetu,tunamwitaji lowasa amalizie shule za kata ambazo aliwai kusema hakupanga ziwe kama zilivyo leo.

2. Lowassa amechafuka sana hivyo anahasira ya kujisafisha jambo ambalo litafanya ajitume kuejesha heshima yake pia hana uccm tena kwani wengi wamejitokeza kumponda hili lina tija kwetu wananchi kwani serikali ya kishikaji itaishia 2015 wakati huo wakina nape watakuwa wamestaafu siasa baada ya kutumiwa kama kisemeo cha ba riz.

3. Lowassa anathubutu kufanya maamuzi magumu kumbukeni mradi wa maji shinyanga ambao alitakiwa na sheria kuomba kibali cha kuchukua maji ziwa Victoria kutoka misri lakini alifanya kwa faida ya watanzania bila kuogopa nchi za magharibi.

Hakika lowassa anastahili kuwa raisi kama CCM inataka ibaki hai vinginevyo wamwache Dr slaa aende ikulu japo mmbowe naye ameanza kumpinga slaa naye mmbowe ni gamba la aina yake anataka yeye awe raisi wakati sisi wananchi tunamtaka slaa na huu ni mpango wa wanafiki wanajiita wanaharakati,wahataki watu wachapa kazi waingie ikulu zaidi wanataka vibaraka wao ambao watalinda biashara zao.

4. Lowassa anakubalika ndani ya chama,watendaji wa kati na wachini wengi wanamkubali lowassa kama ccm ikimsimamisha kazi itakuwa nyepesi kuliko ilikuwa na huu anayepita. MWISHO NDUGU ZANGU LOWASA ANAFAA KUWA RAISI WETU tofauti naye CCM hakuna wengi ni wanafiki tu.na kama haitakuwa hivyo Chadema juweni mtu ambaye watanzania wanaimani naye dani ya cdm ni DR SLAA kama mpango wa kutomsimamisha utafanikiwa basi mjuwe chadema imefikia KIFO chake.

Huu ni mtazamo wangu usio na ushabiki wa pande wowote.LOWASSA USIOGOPE WATANZANIA WENGI WANAKUPENDA.

Haiitaji Phd kutambua uelekeo wako ndugu acha mchele uwe mchele na pumba ziwe pumba.
 
Hata mimi namkubali kwa kipindi kile alipokua waziri mkuu alipotaka kuleta mvua za kichina zinyeshe pale bwawa la Mungu natumaini hapa tulipo yusingekua na mgao wa umeme! Lakini swala la uraisi labda akagombee kule Monduli!
 
maamuzi mengine magumu ya Lowasa ni kutatua shida ya Mtera kwa kuleta wana sayansi wa Siam (Thailand) walete nvua ya kutengeneza inyeshe kwenye bwawa!!!

macinkus
 
Ndiyo maana rais mstaafu Mkapa alisema Watanzania ni wavivu wa kufikiri wengi walimlaumu.
Hili la EL lilimalizwa siku nyingi wakati swala la richmond likiwa moto pale rais aliposema kwamba kilichompata EL ni AJALI YA KISIASA.
Sasa ukitafakari na kama sio mvivu wa kufikiri utabaini ya kwamba EL hakuwa na kosa.
 
Watanganyika tuna tatizo la kukosa kujiamini na kuweka matumaini yetu kwa watu(individuals).
mi nadhani tunatakiwa kujenga taasisi imara zitakazotuletea watu safi kutuongoza na si kuweka matumaini kwa watu...mara, unajua bila fulani...ah nchi itayumba, bila fulani nchi haitokwenda popote! huu ni upuuzi, nchi itadumu na watu watapita.

Kenya kabla ya uchaguzi wa hapa majuzi ulioleta maafa na baadaye mapatano ya Mwai Kibaki na Raila Odinga waliweka matumaini kwa mtu mmoja Samuel Kivuitu....aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kwamba hahongeki...lakini wapi...maji yalipozidi unga akaitwa ikulu amtangaze kibaki kuwa mshindi huku jaji mkuu akiwa pembeni!

Hatuoni sawa, basi hata masikio nayo hayasikii?
 
Kama sio hili tishio la Alshabab ningetafuta watu wa aina yako ili tuone namna tutakavyokwenda Airpot kumpokea Lowasa kwa kushinda vita!!! HAKUNA KAMA LOWASA Yeye akisikia kunauchaguzi achukue Form tu kura zipo wazi, nchi hii ikikosa mtu kama Lowasa ni afadhali tujaribu Jeshi maana uswahili umezidi
mpango wake wa mwisho kabla ya kumweza, ilikuwa ni jengo la kitega uchumi ! Si unaona sasa limepoa ! Jamaa ujasiri wake nmkubwa ni kujilimbikizia !
 
Mimi nafikiri suala sio kuwajadili watu kuwa anafaa au hafai, wananchi ndio wanaojua. Tunachotaka sisi ni kitu kimoja kikubwa, tuwe na katiba ambayo itatuhakikishia kuwa tunapata kiongozi kwa ridhaa ya wananchi na katiba hiyo hiyo iwape wananchi uwezo wa kumuhukumu na hata kumuondoa Raisi au kiongozi yeyote wa umma kama anatumia madaraka yake vibaya. Hatuhitaji kupredict behaviours za watu hapa, yeyote agombee ashinde kihalali, lakini ajue kuna katiba ambayo inaweza kumuondoa at any time kama atakutwa na makosa. Tungekuwa na katiba ya namna hii mbona watu wangenyooka siku nyingi!

Ubaya ni kwamba serikali haitaki kuona jambo hili likifanyika, wanataka tuendelee na mambo yaleyale tu. Kwa aliyoyasema Lowasa kuwa Raisi anafahamu A-Z kuhusu Richmond, nakuambia tungekuwa na katiba nzuri mbona angekwenda na maji Rais wa sasa! Tunataka katiba ambayo itatupa tume huru ya uchaguzi, mahakama, TAKUKURU etc etc. Tunataka katiba ambayo hata mimi nikiamua kugombea Ubunge pasipo chama, kama wananchi wananikubali niweze kugombea, kuondokana na ule mtindo ati wa kubuild concensus sijui ukumbi wa Chamwino, what the hell is this! Watu wanaiba rasilimali za nchi halafu mnaenda kukubaliana mumlinde? sheria za wapi hizi!

Naunga mkono kundi la "KATIBA YA WANANCHI", wewe je?
 
Back
Top Bottom