Usingizi gani huu wa serikali?

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Jukumu la kwanza kabisa la serikali ni kulinda raia na kuhakikisha maisha ya wake yanakuwa bora kwa case ya Tanzania tazama ibara ya 8(1)(b) ya katiba ya Tanzania.

Nimeuliza swali, usingizi gani huu serikali? kwa kuwa naona serikali imekaa kimya bila kutoa tamko au kudhibiti madawa yanayouzwa kila kona ya nchi bila kujulikana uthabiti wa viwango vyake. Mathalani, kama unasafiri safari ndefu kwa basi, treni au soma magazeti mbalimbali ya udaku au ya michezo utaona jinsi wanavyonadi dawa mbalimbali zikiwa ni dawa ya meno(wengine huita dawa ya mswaki), dawa za kuongeza nguvu za kiume, dawa za kupunguza unene na kwamba wanavyoshauriwa kutokwenda hospitali maana si chochote na si lolote. Dawa hizi ni za asili na nyingi utaambiwa zimetoka Nigeria, Kongo, ufipa na umasaini. Wapo wanaouza za kutoka China zikiwa ni GNLD, FLP na TIANSH hizi husambazwa hadi maofisini na ukiangalia hazina hata mhuri wa TBS japo wa kuturidhisha tu.


Je, usalama wa afya mlaji unazingatiwaje?? Haya madawa yana ubora gani? maana isije kuwa mtu unatumia kumbe unajimaliza mwenyewe na kama mnavyojua ukiwa unaumwa kila utakachoambiwa ni dawa utakikimbilia tu.

Kwa nini serikali isitoe tamko ama kuthibitisha ama kuzuia usambazaji wa dawa hizo.
 
Back
Top Bottom