usilale ukiwa kazini

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Mahakama moja nchini Malaysia imemhukumu kwenda jela miaka mitano mwizi mmoja aliyekutwa kalala katika nyumba aliyovunja kwenda kufanya wizi.
110210102351_man_asleep_310x130_corbis.jpg




Usilale ukiwa 'kazini'..

Mtandao wa habari wa Canadian press umemkariri mwendesha mashitaka Mohammad Ashraff Diah akisema mwizi huyo alivunja nyumba moja kusini mwa Malaysia wiki iliyopita na kujilaza kitandani na kupitiwa na usingizi fofofo.

Mwenye nyumba hiyo aliporejea asubuhi alimkuta mwizi huyo bado kalala, na kuamua kuita polisi kabla ya mwizi huyo kuamka. Mwizi huyo alikurupuka baada ya polisi kuwasili, na kujaribu kukimbia. Mwizi huyo alikamatwa na dola kadhaa alizokuwa ameimba katika nyumba hiyo. Mwendehsa mashikata Ashraff amesema juzi Jumatano kuwa mwizi huyo alikiri makosa ya wizi, ingawa hakusema lolote kuhusu suala la kulala..
 
lazima alikunywa vilevi tu huwezi kulala kazini kwani mwizi amekuwa komba au ngeleja
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom