Usikubali mtu yeyote akujue hapa JF

pole sana lakini kama ukiendelea kusumbuliwa toa report kwenye vyombo husika

Vyombo husika c vya hao hao magamba? c ndo atamalizwa kabisa? kikubwa nadhani ni kupost vtu ambavyo una uhakika navyo. otherwise hakuna matatizo
 
Badili Id yako! Muombe PAW aibani kabisa hiyo na aitangaze hapa kuwa episodes kala bani ya maisha!
 
ni makosa makubwa kwa mtu yeyote kukujua au kujua id yako hapa jf
kuna dada mmoja amenijua na tukapeana user name zetu huko facebook
yaani ananifatilia sana halafu inaonekana ni mfuasi wa magamba na mimi nayachukia magamba
nahisi atawaonyesha magamba nyumbani kwangu,sasa hivi nimekosa amani
nimekutana naye jana akaniangalia kwa jicho la husuda
nimekosa amani kabisa hapa jf,naomba msifanye makosa kama hayo wakuu!

JF ni unanimous forum... Siyo mahali pa kutafutia Wachumba hapa.

Kuna member mmoja hapa, ni School mate wangu Kibaha, na wote tulikuwa tunaishi bweni la Scandia, ni mimi tu ninayemfahamu kwa sababu anatumia jina lake. Yeye hanifahamu.

Licha ya hayo, siasa ni mchezo mchafu, you need to play with the "right crowd". Mie sina ubavu wa kupigana, kwa hiyo Siasa zangu ziko "confined" kwa Babu yangu, The late Baba wa Taifa, Mw. Julius Kambarage Nyerere.
 
Mkimuona nyani ngabu ana ID nyingi mnamuona hana akili sometimes ngabu ana akili kidogo.
 
Mkimuona nyani ngabu ana ID nyingi mnamuona hana akili sometimes ngabu ana akili kidogo.

Nyie siku moja mpange mkutane sehemu ya wazi Jangwani au Mnazi Moja..

halafu zipingwe mpaka mmoja anyooshe mikono.. Mtatualika baadhi ya members
 
Duh afadhali umenistua nilikuwa na mpango wa kukutana na kidosho wa JF siku ya J2 itabidi nimpoteze ahaaa aaaa,kwanza unaweza kukuta ni lidume mwenzangu hafuu ikawa tabu bin tafrani JF kweli kiboko.
tehtehthete.................!!!!!!!!!!!
 
kama wewe ni 'mwanaharakati' humu ndani kuwa na tahadhari

lakini kama wewe unakuja na kuingia jukwaa la mmu,chit chat na jokes na sports...
ondoa wasi wasi

Naam BOSS ukiwa ni mchangiaji mzuri kule jukwaa la siasa ogopa sana maana unaweza kulambishwa vya kulambishwa kama ikitokea kujuana kwa karibu na wale wa Magamba wanaopigia debe mafisadi ndani ya CCM/Serikali. Ni hatari sana hata kwa familia yako.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom