Usiku wa Habari TBC1 Kwishney

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,711
12,067
Baada ya mpiganaji Jeri Muro kupata matatizo, kipindi hiki sasa hakina tija kabisa, kimekua ruined.
Mkuu Jerry alitisha kwenye"ripoti Maalum ITV, na baada ya kuhamia TBC1 alianzisha kipindi kilichovuta hisia za wengi cha "usiku wa Habari, TBC1.

Tulikua 'tukiinjoi' na habari za kiuchunguzi, zilizojaa skendo,ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa sasa hatuoni sababu ya kulala saa tano usiku. Kipindi kimejaa maswali yalio-fremiwa,ya kumpa promo anayehojiwa,ka vile mwandishi ameonywa 'ukilikoroga utalinywa mwenyewe.'

Tulikua tukishuhudia, kesho yake wakuu lazima waje watoe tamko,au hatua, na kibongobongo, tume zilikua zinaundwa, sa ivi hakuna kitu,hakuna anaeangalia, kwa mbaaali Sudi Mnete anajitahidi.

Hakuna maswali ya titi for tat, yaan maswali ni ya kiuoga uoga tu. Hakuna tofauti na kipindi cha Daladala.

Au ni TV yangu tu wakuu!!, kama sio basi naomba hiki kipindi kifutwe.
 
Mie nimeacha kukiangalaia siku nyiiingi tu. Last week katika kupitia pitia channel nilipozama TBC kwenye usiku wa habari nikakuta stori za nguva!
 
I share similar views mpiganaji!!!! The content is well spoilt before it goes on air.... It is a bit discouraging that there is one and only one courageous journalist who is capable of unearthing the scandalous and pitious reports in this country, Jerry Muro.
 
hakuna kitu kabisa,
hivi case yake (J MUro) inaendeleaje?
 
Baada ya mpiganaji Jeri Muro kupata matatizo, kipindi hiki sasa hakina tija kabisa, kimekua ruined.
Mkuu Jerry alitisha kwenye"ripoti Maalum ITV, na baada ya kuhamia TBC1 alianzisha kipindi kilichovuta hisia za wengi cha "usiku wa Habari, TBC1.

Tulikua 'tukiinjoi' na habari za kiuchunguzi, zilizojaa skendo,ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa sasa hatuoni sababu ya kulala saa tano usiku. Kipindi kimejaa maswali yalio-fremiwa,ya kumpa promo anayehojiwa,ka vile mwandishi ameonywa 'ukilikoroga utalinywa mwenyewe.'

Tulikua tukishuhudia, kesho yake wakuu lazima waje watoe tamko,au hatua, na kibongobongo, tume zilikua zinaundwa, sa ivi hakuna kitu,hakuna anaeangalia, kwa mbaaali Sudi Mnete anajitahidi.

Hakuna maswali ya titi for tat, yaan maswali ni ya kiuoga uoga tu. Hakuna tofauti na kipindi cha Daladala.

Au ni TV yangu tu wakuu!!, kama sio basi naomba hiki kipindi kifutwe.

Hatuhitaji makanjanja yanayodai rushwa kwa kutumia pingu! Nini usiku wa habari? Unafiki mtupu! Alikuwa anajifanya kufichua maovu kumbe yeye ndiye kitovu cha maovu!
 
Yaani hata mimi niliacha kukiangalia kitamboooooooo baada ya mpiganaji kuwekewa zengwe. Hivi najiuliza kama mpaka leo angekuwepo sijui serikali ya mheshimiwa ingekuwa inahemea wapi.

Haya bwana hapa ndipo inapotimia ile methali isemayo... "Kwa nani sijui(hapa nimesahau kidogo) huenda kilio na kwa muoga huenda kicheko.
 
Nadhani kipindi hicho kitatumiwa sana wakati wa kampeni!
 
Naungana na wengi kuhusu kipindi hiki kukosa mvuto. Dawa sio kukifuta, bali kumuweka mtangazaji mwenye mvuto kama level ya Jerry.

Hii ni kawaida kwa TV pesonalities wakiondoka mvuto hupungua, hata CCN mwaka huu Larry King anastaafu na ndio mwisho wa Larry King Live, ila wataibuka wengine na vipindi vingine. Kwenye utangazaji, zaidi ya profesionalism, vipaji binafsi na muonekano pia vina play part ya kuwashika watazamaji.

Nakumbuka enzi ya kile kipindi cha Kiti Moto, baada ya kipindi kufa, zianzishwa talk show kibao, Malumbano ya Hoja, Gnerali on Monday, Jee Tutafika, Hamza Kasongo Hour etc etc, lakini kwa mtazamo wangu bado hakikutokea kipindi kilichofikia mvuto wa kiwango cha 'Kiti Moto'.

TBC wananakiwa wafungue zaidi milango ya personal creativity kwa watangazaji wake ili wapewe tuu muongozo na kuruhusu vipaji husika ndivyo vimiliki screen, sio kumlazimisha Sudi Mnette kuvaa viatu vya Jerry.
 
Wangelitumia njia ya watu wanakuwa na STUDIO zao na wanatengeneza vipindi vyao wenyewe na KUVIUZA kwenye TV kwa makubaliano. Pia hata kama wana vipindi kwenye STUDIO za ITC au TBC1, basi wasiwaingilie. Tatizo ni kuwa kwa nchi za chama kimoja kama Tanzania, hilo haliwezekani kabisa.

Hata nchi kama USA, nimeshashuhudia mtu akifukuzwa kazi. Kama mtakuwa mnamkumbuka yule dada wa South Africa kwenye kipindi cha INSIDE AFRICA aitwaye Tumi Makgabo alimlima maswali Rais George Bush na kilichofuata ni KUNYANG'ANYWA VIZA yake ya USA na hapohapo kufukuzwa kazi CNN. CNN walishindwa hata kuongelea hii habari nzima na wakagusiagusia kwa mbali na kuonyesha tu kisehemu Bush akijitetea kwa hasira saaana "We are not. We are not..................."

talk_with_tumi_img.jpg
 
Hi wadau kabla sijachangia hii hoja naomba mnijuze: Hivi TBC ni ya CCM mbona huwa hawaripoti ripoti matukio ya CHADEMA au CUF? Nije kwenye hoja sasa. hata mimi hiki kipindi nilisha acha kuangalia toka Jeri Muro aondoke. Kwishny kabisa.
 
HawaHi wadau kabla sijachangia hii hoja naomba mnijuze: Hivi TBC ni ya CCM mbona huwa hawaripoti ripoti matukio ya CHADEMA au CUF marakwa mara kama wanavyofanya kwa CCM? Nije kwenye hoja sasa. hata mimi hiki kipindi nilisha acha kuangalia toka Jeri Muro aondoke. Kwishny kabisa.
 
Wangelitumia njia ya watu wanakuwa na STUDIO zao na wanatengeneza vipindi vyao wenyewe na KUVIUZA kwenye TV kwa makubaliano. Pia hata kama wana vipindi kwenye STUDIO za ITC au TBC1, basi wasiwaingilie. Tatizo ni kuwa kwa nchi za chama kimoja kama Tanzania, hilo haliwezekani kabisa.

Hata nchi kama USA, nimeshashuhudia mtu akifukuzwa kazi. Kama mtakuwa mnamkumbuka yule dada wa South Africa kwenye kipindi cha INSIDE AFRICA aitwaye Tumi Makgabo alimlima maswali Rais George Bush na kilichofuata ni KUNYANG'ANYWA VIZA yake ya USA na hapohapo kufukuzwa kazi CNN. CNN walishindwa hata kuongelea hii habari nzima na wakagusiagusia kwa mbali na kuonyesha tu kisehemu Bush akijitetea kwa hasira saaana "We are not. We are not..................."

talk_with_tumi_img.jpg

Kumbe haki huwa haitakiwi kufanyiwa kazi loh
 
hakuwa sucked alitaka kuhamia nyumbani ili awe freelancer, kwani hadi saa kuna projects anafanya za CNN anawauzia anapata hela nyingi zaidi. Ya Jery Muro ni ubaya wa utawala wetu wa kitanzania, jeshi la police na watawala wote kwa ujumla, nyota ikingaa badala wainourish wanaipaka black ili iwe dull! shame to we tzs!
 
Back
Top Bottom