Usiingie kwenye mgomo kama hujafanya yafuatayo!!!!!

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
614
Watu wengi huingia kwenye migomo mbalimbali kwa kukurupuka na matokeo yake ni kushindwa kufikia malengo yao.Watanzania wengi hasa walio kwenye ajira hutegemea mishahara na posho ambapo hawana hakiba ya kuendesha maisha yao hata kwa mwenzi mmoja.Hata huu mgomo wa walimu sidhani kama watafanikiwa kwa kiwango wanachotarajia kwani wengi hutegemea ajira tu na hawana namna ya kuenendesha maisha yao bila mshahara. Hii ndiyo maana ukifika tarehe za mwisho wa mwezi walimu hufurika kwenye mabenki ili kuchukua mishahara yao ili wasije wakaadhirika.Nashauri walimu pamoja na wafanyakazi wengine wajitahiti sana kuwa na vyanzo mbadala vya mapato ili wasitishwe na vitisho vya kuwafukuza kazi n.k. Ukiwa unategemea mshahara tu ni rahisi sana kutishwa na kama unategemea mshahara tu nashauri uwe mpole maana huna jeuri kwa mwajiri. walimu watakapofika kwenye mabenki na kukuta mishahara yao haijaingizwa nadhani kesho yake msimamo utalegea, ila wakijihadhari mapema na kuhakikisha wana vyanzo vya pesa vingine hilo halitakuwa tatizo.!!!
 
Angalizo lingine, walimu wengi wana mikopo kutoka kwenye mabenki, saccos, vikoba n.k ambapo hutakiwa kurejesha pesa taslim kila mwisho wa mwezi! sielewi itakuwa vipi endapo mwajiri atasitisha kulipa mishahara kwa walimu watakaoendelea na mgomo huu??
 
Ni ukweli mtupu unakuta mtu ana miaka kumi kazini lakini hata elfu hamsini hana ktk akaunti. Mgomo huu mwajiri asipotoa mshahara unaweza kukosa nguvu.
 
Huo ni ushauri Mzuri, lakini kama kuna madai yao ya msingi serikali iyatekeleze maana isije ikatumia unyonge huo kuwa wataeenda wapi watarudi tu, ujue hawa ndiyo wanaotumika kwenye shughuri nyingi za serikali ikiwa ni pamoja na uchaguzi. Wakiweza kuichukia serikali ujue kitanuka hapo baadaye.
 
Madai yenyewe yanahusu ongezeko ya hizo posho na mishahara, hivi mwalimu anapata wapi pesa ya kusave katika mfumuko huu wa bei? Alafu ni kwanini ili mtumishi wa serikali/mwalimu ili kuishi vizuri lazima wawe na shughuli zingine za ziada? Nini maana ya kufanya kazi sasa?
Waalimu lazima watambue kuwa hii ni 'struggle' dhidi ya hali zao duni kwenda kwenye hali bora zaidi. Katika 'struggle' ya haina yoyote husitegemee kukosa majeraha au hata kifo. Hiyo ndio bei yake na ni lazima ilipwe. Kinachotakiwa ni uvumilivu na kutokukata tamaa hata kama huna kitu sababu ndicho unachopigania. Pona haraka Dk Ulimboka damu yako inawaokoa wengi.
 
Watu wengi huingia kwenye migomo mbalimbali kwa kukurupuka na matokeo yake ni kushindwa kufikia malengo yao.Watanzania wengi hasa walio kwenye ajira hutegemea mishahara na posho ambapo hawana hakiba ya kuendesha maisha yao hata kwa mwenzi mmoja.Hata huu mgomo wa walimu sidhani kama watafanikiwa kwa kiwango wanachotarajia kwani wengi hutegemea ajira tu na hawana namna ya kuenendesha maisha yao bila mshahara. Hii ndiyo maana ukifika tarehe za mwisho wa mwezi walimu hufurika kwenye mabenki ili kuchukua mishahara yao ili wasije wakaadhirika.Nashauri walimu pamoja na wafanyakazi wengine wajitahiti sana kuwa na vyanzo mbadala vya mapato ili wasitishwe na vitisho vya kuwafukuza kazi n.k. Ukiwa unategemea mshahara tu ni rahisi sana kutishwa na kama unategemea mshahara tu nashauri uwe mpole maana huna jeuri kwa mwajiri. walimu watakapofika kwenye mabenki na kukuta mishahara yao haijaingizwa nadhani kesho yake msimamo utalegea, ila wakijihadhari mapema na kuhakikisha wana vyanzo vya pesa vingine hilo halitakuwa tatizo.!!!

Ushauri wako una mawazo mgando, kwa sababu ya shida ndo uuze utu wako. Wewe na serikali kama mna ubia. Maana serikali inafanya hivyo kutulipa kidogo ili tushindwe kujitetea kwa vile hatuna chanzo kingine cha mapato.

Niwatie moyo walimu tusiogope vitisho. Na ielewke kuwa hakuna ukombozi bila maumivu. Leo Tanzania tuko huru baada ya baadhi ya watu kuweka uhai wao rehani. Tupambane si kwa ajili yetu bali hata kwa vizazi vijavyo.

Nimekumbuka wimbo wa Bahati Bukuku "Alipoianza safari------" Kabla ya mgomo wapo waliotutia moyo lakini wengine walitudhihaki eti hawawezi mara ooh hao ni vilaza, Leo tumeamua oh tulijua hawatafanikiwa----

Watanzania tuungeni mkono mgomo huu si muhimu kwa walimu tu bali kwa watu woote.

MAPAMBANO BADO YANAENDELEA ALUTA CONTINUA.
 
Maneno mazito haya! Kuipomea serikali ya vichaa inabidi u-double check kwanza.
 
Maneno mazito haya! Kuigomea serikali ya vichaa inabidi u-double check kwanza.
 
Kauli za wasaliti zinajidihirisha unapozisoma au kuzisikiliza. Watu hawa hawakosekani katika jamii ya binadamu, wasiopenda maendeleo ya wenzao.
 
Ushauri wako una mawazo mgando, kwa sababu ya shida ndo uuze utu wako. Wewe na serikali kama mna ubia. Maana serikali inafanya hivyo kutulipa kidogo ili tushindwe kujitetea kwa vile hatuna chanzo kingine cha mapato.

Niwatie moyo walimu tusiogope vitisho. Na ielewke kuwa hakuna ukombozi bila maumivu. Leo Tanzania tuko huru baada ya baadhi ya watu kuweka uhai wao rehani. Tupambane si kwa ajili yetu bali hata kwa vizazi vijavyo.

Nimekumbuka wimbo wa Bahati Bukuku "Alipoianza safari------" Kabla ya mgomo wapo waliotutia moyo lakini wengine walitudhihaki eti hawawezi mara ooh hao ni vilaza, Leo tumeamua oh tulijua hawatafanikiwa----

Watanzania tuungeni mkono mgomo huu si muhimu kwa walimu tu bali kwa watu woote.

MAPAMBANO BADO YANAENDELEA ALUTA CONTINUA.

PAMOJA SANA MKUU. Kesho ni mgomo tena mwanzo mwisho.
 
Zingatieni haya jamaa kayaandika itafika mda hamjui hata pa kuelekea.
 
Ushauri wako una mawazo mgando, kwa sababu ya shida ndo uuze utu wako. Wewe na serikali kama mna ubia. Maana serikali inafanya hivyo kutulipa kidogo ili tushindwe kujitetea kwa vile hatuna chanzo kingine cha mapato.Niwatie moyo walimu tusiogope vitisho. Na ielewke kuwa hakuna ukombozi bila maumivu. Leo Tanzania tuko huru baada ya baadhi ya watu kuweka uhai wao rehani. Tupambane si kwa ajili yetu bali hata kwa vizazi vijavyo.Nimekumbuka wimbo wa Bahati Bukuku "Alipoianza safari------" Kabla ya mgomo wapo waliotutia moyo lakini wengine walitudhihaki eti hawawezi mara ooh hao ni vilaza, Leo tumeamua oh tulijua hawatafanikiwa----Watanzania tuungeni mkono mgomo huu si muhimu kwa walimu tu bali kwa watu woote.MAPAMBANO BADO YANAENDELEA ALUTA CONTINUA.
Huwezi kupigana vita wakati unanjaa pasipo na umoja pana unafiki "mtoto wa tajiri akionywa mtoto wa masikini tega sikio"
 
ni heri kuumia kidogo na kupata raha kwa muda mrefu walimu wasiogope kufukuzwa kwani wao ni muhimu na watarudishwa tu hata kama watafukuzwa leo na watakaporudi hali ikiwa imebadilishwa wataishi vizuri kwa muda mrefu. kuliko kuogopa kuishi kwa shida kwa muda mfupi na hali sasa wanaishi kwa shidashida kwa miaka yote wanayotumikia serikali.
komaeni walimu
 
Zingatieni haya jamaa kayaandika itafika mda hamjui hata pa kuelekea.

Namwogopa mwalim kuliko hata polisi mwenye bunduki na risasi zake.
Kama mwalim atamwambia mtoto H2O ni Carbondioxide nani atambadilisha huyu mtoto tena ili aelewe kuwa ni water?
Mwl asichezewe hata kidogo anaweza kuleta maafa makubwa sana nchini.
Rejea "SOMETIMES IN APRIL" mwanzo kabisa watu wanaanza...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom