Usichokijua kuhusu Yusuf Manji

Song il gok

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
878
936
Kwanza kabisa fahamu kwamba Yusuf Manji alichaguliwa na wanayanga mwaka 2012, Yanga ikiwa haifanyi vizuri katika mpira ukilinganisha na wahasimu wake Simba. Baada tu ya Yusuf Manji kuingia madarakani, mwaka 2012 Yanga ikatwaa ubingwa wa Ligi Kuu. Tangia kipindi hicho hadi sasa Yanga imeshatwaa ubingwa mara 3.

Hivi karibuni watu wamezua sintofahamu juu ya adhma ya Yusuf Manji Jangwani. Nia na madhumuni ya Manji kwa Yanga ni kuwekeza ili klabu iwe na uwezo mkubwa zaidi na siku moja iweze kushindana kimataifa na hata iweze kutwaa ubingwa wa Afrika.
Kuna mambo mengi ambayo watu wengi hawajui kuhusu Yusuf Manji. Yeye kama Mwenyekiti ndiye aliyependekeza na kuwezesha kupandishwa mishahara kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi iliosababisha kwa namna moja au nyingine kuleta mafanikio ya Yanga tunayoiona leo.

Fahamu kwamba mkataba kati ya TBL na Yanga ulipokwisha muda wake mwaka huu, hakuna hata kampuni moja iliyojitokeza kwa ajili ya udhamini mpya. Manji kwa mapenzi yake akaona aende kuiombea Yanga udhamini kutoka katika kampuni ambayo alishawahi kuwa mwenyekiti wake.
Kwa kuangalia yote ambayo Manji ameyafanya kwa kujitoa kwa hali na mali, inashangaza kwamba mtu anaweza simama akasema kwamba kuna dalili za rushwa wakati hata huko nyuma, Manji alifanya mambo yote kwa uwazi kabisa. Tujiulize, ufisadi ni kutoa au kuchukua hela? Na je Manji amekuwa akitoa au kuchukua hela Yanga?

Kwa mapenzi yake kwa klabu pamoja na mpira wa Kitanzania, Manji amekua akichangia kwa kiasi kikubwa lakini leo watu ambao hatujawahi kuwasikia wakichangia lolote kwenye mpira wanapaza sauti na kuleta kashfa zisizokuwa na ushahidi wowote. Wanamichezo wenzangu pamoja na wapenzi wote wa mpira, tuwakatae watu wa haina hii kwa nguvu zote.

Mafanikio waliyoyapata Yanga ndani ya kipindi ambacho Manji amekuwa mwenyekiti sio yakuyabeza hata kidogo, tukifanya mchezo tunaweza rudi kule tulipotoka. Si unajua msemo wa adui yako muombee njaa? Ndio wanachotuombea watani wetu.
Mwezi Julai 2016 Yusuf Manji alichaguliwa na wanachama wa Yanga kwa asilimia 100 kuwa mwenyekiti kwa kipindi cha pili mfululizo. Hii inadhihirisha ni jinsi gani wanachama wa Yanga walivyo bado na imani na mwenyekiti wao.
Watu watambue kwamba Manji hajaanza kujihusisha au kuichangia Yanga mwaka 2012 pindi alipoutwaa uwenyekiti bali alianza kipindi cha nyuma zaidi na Yanga imekua ikinufaika kwa miaka mingi sana.

Ukiachana na mpira Yusuf Manji pia amekua na mchango mkubwa sana hapa Tanzania. Kupitia makampuni yake ameweza kuwapatia ajira Watanzania wengi sana. Licha ya hayo yote, pale anapojaribu kuwekeza upande wa pili wa michezo watu wanaleta hoja za kumpinga na kutaka kudhoofisha azma yake ya kutaka kuleta mabadiliko yenye tija.

Yusuf Manji amekuwa ni mwanzilishi wa “Africa Against Ebola Solidarity Trustee“ ambayo ilikua chini ya uangalizi wa Thabo Mbeki ilyokuwa na lengo la kutokomeza Ebola barani Afrika. Manji ameweza kusimamia na kufanikisha uchangishwaji wa mamilioni ya pesa na yeye akiwa mmoja kati ya wachangiaji wakubwa katika mfuko huo. Hata baada ya kufanya yote hayo, Manji hajawahi kujitangaza kwa hayo yote ambayo ameyafanya.

Dunia imekuwa ikitambua michango ya Yusuf Manji na hadi kumpa tuzo mbalimbali. Mfano, mwaka 2015 alipewa tuzo ya Iconic business leader of the year ambayo pia alishawahi kupewa pia Sheikh Ahmed Bin Saeed Maktoum, Chairman and CEO of Emirates na watu wengine wengi maarufu.
Katika siasa aliamua kuingia katika kinyanganyiro cha udiwani ambao watu wengi walidhania ni cheo kidogo kwa mtu mwenye wadhifa wake lakini alifanya hivyo ili kuweza kuwafikia zaidi watu kwa ukaribu. Amekua akichangia sana katika sekta ya Elimu Mbagala Kuu. Licha ya haya yote anayofanya bado kuna watu wanaamua kumvunja moyo kwa kupinga mipango ambayo anataka kuendelea kuitekeleza kwa ajili ya jamii ya Tanzania.
Yusuf ambae amekaririwa na Saleh Jembe Blog kuwa “wamuache amechoka” ni kuonyesha kuwa yeye pia ni binadamu na anaumia kama wanavyoumia binadamu wengine.

Pale mtu anapoamua kuchangia pesa zake binafsi kwa ajili ya jambo jema,hatuna budi wananchi pamoja na viongozi kumtia moyo na kumpa ushirikiano ili azma iweze kufikiwa. Yusuf Manji hajawahi kuchukua kitu chochote Yanga wala hajawai kuomba kitu kutoka kwa Yanga au wanachama wake zaidi ya ushirikiano.

Hatuna budi kumwachia Manji akaendelea kuiboresha timu yetu iwe ya kimataifa zaidi na kutufanya wana Yanga tuendelee kufurahia ushindi na wapenzi wa mpira nchini wakijionea Yanga inavyosonga mbele. Maana nyuma sie kwetu mwiko.

manji 3.jpg
 
Acha kumpigia chapuo, mbona upande mbaya wake hujauweka? Au hausikii tuhuma tuhuma za rushwa na upigaji unaomuhusu?Yeye siyo Mungu wala tajiri pekee Anayeweza kuisaidia yanga, ni muda muafaka sasa yanga kujisajili kama kampuni, siyo kumkodisha mtu mmoja timu bila kuwa na uhakika akimaliza mda wake nini kitafuatia.

Tatizo mnapenda sana kulamba makalio ya wenye fedha, yanga ina uwezo wa kugenerate mapato yatakayoiwezesha kuwa club kubwa africa, inahitaji viongozi waendeshaji wazuri si kwa kuwa mtu ni mwanachama tuu wa siku nyingi au ana hela mnamchagua kuwa mwenyekiti

Kwanza anatakiwa aondoke na jopo la viongozi wote waliopo sasa yanga ipate viongozi wapya, hatuwezi kuwa na viongozi wenye mentality za kipuuzi kabisa, wanaowaza kwenda quality plaza kuvuta pesa kwa mwenyekiti, Yangs inahitaji visionary leaders watakaoitoa katika hali ya utegemezi wa mtu mmoja.

Hivi uyo manji baada ya kupewa timu, Mungu akamchukua yanga itakuwa wapi?au baada ya miaka miwili akasusa tutafanya nini?mtu mwenyewe anasusa susa kama mtoto wa kike
 
Boss tuhuma gani za rushwa unazoziongelea na upigaji upi? Leo hii hapa nikuambia jielezee utaelezea mazuri yako au mabaya yako? Jenga hoja kwanini asipewe sio unaanza kubishashana na facts.
 
Wabongo mko na midomo na maneno mengi na njaa tu, wala hamchangii timu. Mwacheni yusuph amiliki timu na faida yake inaonekana. Sasa mnampiga vita iweje?mbona hamchangii hata kadi ya uanachama. Wabongo bana.. Majungu tu na fitina.. Hakuna maendeleo

Kaka a

Ahsante sana kaka..Bora useme wewe..kuna wengine hata wakiambiwa Dodoma hakuna bahari atabisha tu kwasababu yeye miaka yake yote anaishi Dar.
 
Kwanza kabisa fahamu kwamba Yusuf Manji alichaguliwa na wanayanga mwaka 2012, Yanga ikiwa haifanyi vizuri katika mpira ukilinganisha na wahasimu wake Simba. Baada tu ya Yusuf Manji kuingia madarakani, mwaka 2012 Yanga ikatwaa ubingwa wa Ligi Kuu. Tangia kipindi hicho hadi sasa Yanga imeshatwaa ubingwa mara 3.

Hivi karibuni watu wamezua sintofahamu juu ya adhma ya Yusuf Manji Jangwani. Nia na madhumuni ya Manji kwa Yanga ni kuwekeza ili klabu iwe na uwezo mkubwa zaidi na siku moja iweze kushindana kimataifa na hata iweze kutwaa ubingwa wa Afrika.
Kuna mambo mengi ambayo watu wengi hawajui kuhusu Yusuf Manji. Yeye kama Mwenyekiti ndiye aliyependekeza na kuwezesha kupandishwa mishahara kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi iliosababisha kwa namna moja au nyingine kuleta mafanikio ya Yanga tunayoiona leo.

Fahamu kwamba mkataba kati ya TBL na Yanga ulipokwisha muda wake mwaka huu, hakuna hata kampuni moja iliyojitokeza kwa ajili ya udhamini mpya. Manji kwa mapenzi yake akaona aende kuiombea Yanga udhamini kutoka katika kampuni ambayo alishawahi kuwa mwenyekiti wake.
Kwa kuangalia yote ambayo Manji ameyafanya kwa kujitoa kwa hali na mali, inashangaza kwamba mtu anaweza simama akasema kwamba kuna dalili za rushwa wakati hata huko nyuma, Manji alifanya mambo yote kwa uwazi kabisa. Tujiulize, ufisadi ni kutoa au kuchukua hela? Na je Manji amekuwa akitoa au kuchukua hela Yanga?

Kwa mapenzi yake kwa klabu pamoja na mpira wa Kitanzania, Manji amekua akichangia kwa kiasi kikubwa lakini leo watu ambao hatujawahi kuwasikia wakichangia lolote kwenye mpira wanapaza sauti na kuleta kashfa zisizokuwa na ushahidi wowote. Wanamichezo wenzangu pamoja na wapenzi wote wa mpira, tuwakatae watu wa haina hii kwa nguvu zote.

Mafanikio waliyoyapata Yanga ndani ya kipindi ambacho Manji amekuwa mwenyekiti sio yakuyabeza hata kidogo, tukifanya mchezo tunaweza rudi kule tulipotoka. Si unajua msemo wa adui yako muombee njaa? Ndio wanachotuombea watani wetu.
Mwezi Julai 2016 Yusuf Manji alichaguliwa na wanachama wa Yanga kwa asilimia 100 kuwa mwenyekiti kwa kipindi cha pili mfululizo. Hii inadhihirisha ni jinsi gani wanachama wa Yanga walivyo bado na imani na mwenyekiti wao.
Watu watambue kwamba Manji hajaanza kujihusisha au kuichangia Yanga mwaka 2012 pindi alipoutwaa uwenyekiti bali alianza kipindi cha nyuma zaidi na Yanga imekua ikinufaika kwa miaka mingi sana.

Ukiachana na mpira Yusuf Manji pia amekua na mchango mkubwa sana hapa Tanzania. Kupitia makampuni yake ameweza kuwapatia ajira Watanzania wengi sana. Licha ya hayo yote, pale anapojaribu kuwekeza upande wa pili wa michezo watu wanaleta hoja za kumpinga na kutaka kudhoofisha azma yake ya kutaka kuleta mabadiliko yenye tija.

Yusuf Manji amekuwa ni mwanzilishi wa “Africa Against Ebola Solidarity Trustee“ ambayo ilikua chini ya uangalizi wa Thabo Mbeki ilyokuwa na lengo la kutokomeza Ebola barani Afrika. Manji ameweza kusimamia na kufanikisha uchangishwaji wa mamilioni ya pesa na yeye akiwa mmoja kati ya wachangiaji wakubwa katika mfuko huo. Hata baada ya kufanya yote hayo, Manji hajawahi kujitangaza kwa hayo yote ambayo ameyafanya.

Dunia imekuwa ikitambua michango ya Yusuf Manji na hadi kumpa tuzo mbalimbali. Mfano, mwaka 2015 alipewa tuzo ya Iconic business leader of the year ambayo pia alishawahi kupewa pia Sheikh Ahmed Bin Saeed Maktoum, Chairman and CEO of Emirates na watu wengine wengi maarufu.
Katika siasa aliamua kuingia katika kinyanganyiro cha udiwani ambao watu wengi walidhania ni cheo kidogo kwa mtu mwenye wadhifa wake lakini alifanya hivyo ili kuweza kuwafikia zaidi watu kwa ukaribu. Amekua akichangia sana katika sekta ya Elimu Mbagala Kuu. Licha ya haya yote anayofanya bado kuna watu wanaamua kumvunja moyo kwa kupinga mipango ambayo anataka kuendelea kuitekeleza kwa ajili ya jamii ya Tanzania.
Yusuf ambae amekaririwa na Saleh Jembe Blog kuwa “wamuache amechoka” ni kuonyesha kuwa yeye pia ni binadamu na anaumia kama wanavyoumia binadamu wengine.

Pale mtu anapoamua kuchangia pesa zake binafsi kwa ajili ya jambo jema,hatuna budi wananchi pamoja na viongozi kumtia moyo na kumpa ushirikiano ili azma iweze kufikiwa. Yusuf Manji hajawahi kuchukua kitu chochote Yanga wala hajawai kuomba kitu kutoka kwa Yanga au wanachama wake zaidi ya ushirikiano.

Hatuna budi kumwachia Manji akaendelea kuiboresha timu yetu iwe ya kimataifa zaidi na kutufanya wana Yanga tuendelee kufurahia ushindi na wapenzi wa mpira nchini wakijionea Yanga inavyosonga mbele. Maana nyuma sie kwetu mwiko.

View attachment 383886
Naona umekuja na barua ndefu ya kumsifia manji.
Huo msaad anaotoa wakati tunambia Yanga inadaia sh billion 5.6 kwa mda ambao yy akia madarakani hauoni huo ni ujinga?
 
Boss tuhuma gani za rushwa unazoziongelea na upigaji upi? Leo hii hapa nikuambia jielezee utaelezea mazuri yako au mabaya yako? Jenga hoja kwanini asipewe sio unaanza kubishashana na facts.
Hoja ambazo hujaziona katika bandiko langu

1. Succession plan - baada ya kukodishwa hiyo timu, nini kitafuatia?mfano akifariki manji nini kitatokea?mustakabali wa Yanga

2. Ushirikishwaji wa wanachama - yanga na simba ni timu za wanachama ambao wameilea tangu ilivyoanzishwa mpaka ilipofika, baada ya manji kuichukua yanga kwa 75% wanachama hawana chao, tuangalie timu ya simba na Mo, kachukua 51% na ka invest bilioni 20, 49% inaenda kwa wanachama, bado ni wamiliki wa timu yao kwa hiyo percent.

Manji ni mfanyabiashara, na biashara siku zote zina makandokando yake, tufanya biashara zake zimefail, je Yanga wana backup?25 ya profit ambayo inaweza isiwepo?

3. Ukiukwaji mkubwa wa taratibu za kumkabidhi timu, hata wazo lenyewe la kumkodisha ni kituko

4. Kutokuwa na imani na viongozi njaa waliopo yanga, viongozi wasiokuwa na ufanisi wa kuongoza team kwa malengo
 
Kwanza kabisa fahamu kwamba Yusuf Manji alichaguliwa na wanayanga mwaka 2012, Yanga ikiwa haifanyi vizuri katika mpira ukilinganisha na wahasimu wake Simba. Baada tu ya Yusuf Manji kuingia madarakani, mwaka 2012 Yanga ikatwaa ubingwa wa Ligi Kuu. Tangia kipindi hicho hadi sasa Yanga imeshatwaa ubingwa mara 3.

Hivi karibuni watu wamezua sintofahamu juu ya adhma ya Yusuf Manji Jangwani. Nia na madhumuni ya Manji kwa Yanga ni kuwekeza ili klabu iwe na uwezo mkubwa zaidi na siku moja iweze kushindana kimataifa na hata iweze kutwaa ubingwa wa Afrika.
Kuna mambo mengi ambayo watu wengi hawajui kuhusu Yusuf Manji. Yeye kama Mwenyekiti ndiye aliyependekeza na kuwezesha kupandishwa mishahara kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi iliosababisha kwa namna moja au nyingine kuleta mafanikio ya Yanga tunayoiona leo.

Fahamu kwamba mkataba kati ya TBL na Yanga ulipokwisha muda wake mwaka huu, hakuna hata kampuni moja iliyojitokeza kwa ajili ya udhamini mpya. Manji kwa mapenzi yake akaona aende kuiombea Yanga udhamini kutoka katika kampuni ambayo alishawahi kuwa mwenyekiti wake.
Kwa kuangalia yote ambayo Manji ameyafanya kwa kujitoa kwa hali na mali, inashangaza kwamba mtu anaweza simama akasema kwamba kuna dalili za rushwa wakati hata huko nyuma, Manji alifanya mambo yote kwa uwazi kabisa. Tujiulize, ufisadi ni kutoa au kuchukua hela? Na je Manji amekuwa akitoa au kuchukua hela Yanga?

Kwa mapenzi yake kwa klabu pamoja na mpira wa Kitanzania, Manji amekua akichangia kwa kiasi kikubwa lakini leo watu ambao hatujawahi kuwasikia wakichangia lolote kwenye mpira wanapaza sauti na kuleta kashfa zisizokuwa na ushahidi wowote. Wanamichezo wenzangu pamoja na wapenzi wote wa mpira, tuwakatae watu wa haina hii kwa nguvu zote.

Mafanikio waliyoyapata Yanga ndani ya kipindi ambacho Manji amekuwa mwenyekiti sio yakuyabeza hata kidogo, tukifanya mchezo tunaweza rudi kule tulipotoka. Si unajua msemo wa adui yako muombee njaa? Ndio wanachotuombea watani wetu.
Mwezi Julai 2016 Yusuf Manji alichaguliwa na wanachama wa Yanga kwa asilimia 100 kuwa mwenyekiti kwa kipindi cha pili mfululizo. Hii inadhihirisha ni jinsi gani wanachama wa Yanga walivyo bado na imani na mwenyekiti wao.
Watu watambue kwamba Manji hajaanza kujihusisha au kuichangia Yanga mwaka 2012 pindi alipoutwaa uwenyekiti bali alianza kipindi cha nyuma zaidi na Yanga imekua ikinufaika kwa miaka mingi sana.

Ukiachana na mpira Yusuf Manji pia amekua na mchango mkubwa sana hapa Tanzania. Kupitia makampuni yake ameweza kuwapatia ajira Watanzania wengi sana. Licha ya hayo yote, pale anapojaribu kuwekeza upande wa pili wa michezo watu wanaleta hoja za kumpinga na kutaka kudhoofisha azma yake ya kutaka kuleta mabadiliko yenye tija.

Yusuf Manji amekuwa ni mwanzilishi wa “Africa Against Ebola Solidarity Trustee“ ambayo ilikua chini ya uangalizi wa Thabo Mbeki ilyokuwa na lengo la kutokomeza Ebola barani Afrika. Manji ameweza kusimamia na kufanikisha uchangishwaji wa mamilioni ya pesa na yeye akiwa mmoja kati ya wachangiaji wakubwa katika mfuko huo. Hata baada ya kufanya yote hayo, Manji hajawahi kujitangaza kwa hayo yote ambayo ameyafanya.

Dunia imekuwa ikitambua michango ya Yusuf Manji na hadi kumpa tuzo mbalimbali. Mfano, mwaka 2015 alipewa tuzo ya Iconic business leader of the year ambayo pia alishawahi kupewa pia Sheikh Ahmed Bin Saeed Maktoum, Chairman and CEO of Emirates na watu wengine wengi maarufu.
Katika siasa aliamua kuingia katika kinyanganyiro cha udiwani ambao watu wengi walidhania ni cheo kidogo kwa mtu mwenye wadhifa wake lakini alifanya hivyo ili kuweza kuwafikia zaidi watu kwa ukaribu. Amekua akichangia sana katika sekta ya Elimu Mbagala Kuu. Licha ya haya yote anayofanya bado kuna watu wanaamua kumvunja moyo kwa kupinga mipango ambayo anataka kuendelea kuitekeleza kwa ajili ya jamii ya Tanzania.
Yusuf ambae amekaririwa na Saleh Jembe Blog kuwa “wamuache amechoka” ni kuonyesha kuwa yeye pia ni binadamu na anaumia kama wanavyoumia binadamu wengine.

Pale mtu anapoamua kuchangia pesa zake binafsi kwa ajili ya jambo jema,hatuna budi wananchi pamoja na viongozi kumtia moyo na kumpa ushirikiano ili azma iweze kufikiwa. Yusuf Manji hajawahi kuchukua kitu chochote Yanga wala hajawai kuomba kitu kutoka kwa Yanga au wanachama wake zaidi ya ushirikiano.

Hatuna budi kumwachia Manji akaendelea kuiboresha timu yetu iwe ya kimataifa zaidi na kutufanya wana Yanga tuendelee kufurahia ushindi na wapenzi wa mpira nchini wakijionea Yanga inavyosonga mbele. Maana nyuma sie kwetu mwiko.

View attachment 383886
Wewe ni mnufaika binafsi wa Manji, mchumia tumbo tu huna lolote!!
Tunataka mwekezaji transparent, aweke bayana business plan yake ijadiliwe na wadau na wanachama wote, waulize maswali magumu, ayajibu waelewe sio kwa hila hizi za kuviziana promising the world but only to deliver a village, hapana! Manji na Mo are taking advantage ya njaa na umbumbumbu wa wananchama wa hizi klabu mbili; there is something sinister behind these moves by Manji na Mo
 
Naona umekuja na barua ndefu ya kumsifia manji.
Huo msaad anaotoa wakati tunambia Yanga inadaia sh billion 5.6 kwa mda ambao yy akia madarakani hauoni huo ni ujinga?
Sasa akiiendesha kibiashara hiyo migogoro ingekua imekwisha boss
 
Wewe ni mnufaika binafsi wa Manji, mchumia tumbo tu huna lolote!!
Tunataka mwekezaji transparent, aweke bayana business plan yake ijadiliwe na wadau na wanachama wote, waulize maswali magumu, ayajibu waelewe sio kwa hila hizi za kuviziana promising the world but only to deliver a village, hapana! Manji na Mo are taking advantage ya njaa na umbumbumbu wa wananchama wa hizi klabu mbili; there is something sinister behind these moves by Manji na Mo
When you say "something sinister" what do you actually mean, sir?!
 
simba na yanga ni majipu,yanapaswa kutumbuliwa ,hatukatai uwekezaji lakini hizi klabu zilikuwa na uwezo wa kujiendesha japo na kuwa na mwanzo wa hao wa wekezaji,inashanga kuona tamasha kubwa kama la simba day likifanywa kwa kipuuzi na kiujanja ujanja zaidi wakati lingeweza kuandaliwa vizuri na klabu ikanufaika zaidi ya hivi ,yanga inamashabiki zaidi ya miliojni 5 nchi nzima wameshindwa nini basi kubuni hata wazo la kuwachangisha hao wanachama miamia kwa ajili ya ujenzi wa uwanja tu?
 
Mkuu embu toa mbadala mwingine maana unajichanganya tuu. Yanga ndio imeshashindwa kujiendesha ndo maana Manji amekuja na mpango mkubwa zaidi
 
Msiwe mbumbumbu nyie Yanga ni zaidi ya Manji tatizo njaa,mnaona Manji ndio kila kitu hii ni hatari sana katika klabu kubwa kama Yanga,Yanga ilikuwepo na itaendelea kuwepo lakini Manji atapita kama walivyopita wengine wengi ,muhimu hapa tungetengeneza mfumo wa kuongoza klabu lakini hizi nyingine ni swaga tu.
 
Mkuu mbona povu?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom