Usichekelee Kutumbuliwa Wenzako, Chunguza Mchango Wako

Ozzanne Issakwisa

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
288
239
Nilipokuwa kijana mdogo, nilitaka kuibadirisha dunia,

Nilipojua ni ngumu kubadirisha dunia, nikasema nitajaribu taifa langu,

Nilipoona ni vigumu kubadirisha taifa langu, nikaona nguvu nielekeze kwa mji wangu,

Sikuweza kubadirisha mji, nikajaribu kubadirisha familia yangu,

Sasa, nikiwa mzee, nimetambua kitu pekee ninachoweza kufanya ni kujibadirisha mimi mwenyewe,

Na kwa haraka nimetambua kwamba kama toka zamani ningejibadirisha, ningeambukiza mabadiriko kwa familia,

Mimi na familia, tungeambukiza mabadiriko mji wetu,

Mji nao ungeleta matokeo mazuri kwa taifa, na kwa hakika ningeweza kubadirisha dunia.


Mtawa asiyejulikama 1100 A.D.,

MAONI

Usitegemee kutendewa jambo kubwa na mtu mwingine zaidi ya wewe,

Ukitambua hilo hutalaumu sana, maana lawama nyingi ni kukwepa majukumu,

Mbona twatoa lawama zote kwa daktari wa zamu, kwa mgonjwa aliyepata ajali, ati "kafa kwa kukosa MAJI"?!!!

Mbona hatuulizi kapataje ajali? Alikuwa akiendesha kwa kasi? Hakuvaa helmet? n.k

Watu watatumbuliwa kila siku kwa uzembe wao, au kwa shinikizo letu, lakini hatutawafanya malaika,

Wewe pekee waweza kuwa malaika, maana unaweza kubadirika,

Mabadiriko yanaanza na wewe, pale ulipo.

Mfanyabiashara fungua duka mapema, watu wawahi kazini,

Sote tuwahi makazini, tulijenge taifa lenu,

Kisha tulipe kodi, tupate maji hospitali,

Daktari wewe si Mungu, lakini wito wako ni kutuongezea walau sekunde moja ya maisha,

Ofisa ushuru kusanya mapato, hospitali zipate dawa,

Afisa ardhi acha usumbufu, yule mwananchi asipate magonjwa ya presha,

Hakimu tenda haki, yule mjane apate stahili zake, watoto waende shule

Sote tunategemeana, tujitafakari kabla ya kulaumu.
 
Back
Top Bottom