USIA wa Nyerere unaoishi leo

Mimi nangoja tuu kusikia kama hawa baraza la maskofu watamuenzi nyerere mpaka kuwa mntakatifu. Raisi yeyote duniani mwenye au aliyekuwa na secretary wawili regural secretary na private secretary hawezi kabisaa kuwa mtakatifu. Baraza la maaskofu ni lazima wachunguze kazi za private secretary kwanza ndipo wafikirie kutoa sacrament ya utakatifu kwa nyerere. Leo nimejifunza makubwa sana kuhusu nyerere. Kumbe UN na OAU walinyonda kutuunga mkono vita vyetu ingawa tulivamiwa! Hata Misri! Sasa kimbere mbele cha nyerere kuvunja uhusiano wa kibalozi na Israeli mwaka 1973kwa sababu ya Misri kupigwa na Israel kilikuwa cha nini?Kuweka palestinian Day nchini Tanzania na kuwatukana wayahudi kila mwaka wakati hakuna hata nchi moja ya waarabu wala OAU blacks iliyoungana na sisi kulaan amin na matendo yake, hii ilkuwa ni kumpandeza nani? Kweli kabisaa kuondoka nyerere madarakani ni kuchanua kwa Tanzania, naamini kabisa hili. Sasa kama yeye nyerere alikataa kufanya mazungumzo ya diplomasia na Uganda ili kuyamaliza mzozo kwa nini basi alilaani Israel kuchukua mateka yake Uganda? Tena alidai eti Israel ilipaswa kufanya mazungumzo ya kidiplomasia na Iddi amin ili mzozo umalizike kwa Usalama!!! Hii inawezekana kuwa sabau ya OAU na UN kutudhalau wakati wa mgogolo na Uganda!

umeandika pumba pumba pumba pumba pumba pumba pumba....
 
mkuu hivi unaposema wtz waliyaondoa majeshi ya idd amin kwa urahisi unamaanisha nini? kumbuka uvamizi ule ni wa kushtukiza na serikali ya nyerere haikujiandaa kivita, km ni uvamizi uliokuwa umeandaliwa wale wanakagera wasingeuawa kinyama namna ile, iddi amini aliingiza majeshi kagera na kuwaua raia wasiokuwa na hatia wakiwemo watoto na wakina mama, unavyomtetea eti alikuwa anawakomboa wanakagera kutoka kwenye ujamaa huo ni ujuha sawa na wa huyo idd amini, malengo ya idd amini ilikuwa kuchukua hadi mkoa wa tanga ili nayeye nchi yake iwe na bandari. hakukuwa na urahisi wa kumuondoa idd amini, nguvu ya umma (hapa namaanisha mgambo waliofunzwa kwa muda wa mwezi mmoja tu akiwemo baba yangu mzazi) ndio waliowekwa mstari wa mbele kupambana na majeshi ya idd amini, walikufa mgambo wengi sana ila kutokana na uwingi wa wanamgambo wa tz na kwa ushirikiano wa wananchi wa uganda (kumbuka hapa idd amini alikuwa pia anawatesa waganda wenzake kwa kuwaua na unyanyasi wa kila namna) ndio waliofanikisha kumn'goa idd amini, pia serikali ya china iliisaidia sana tz kwa silaha. unaweza ukamkosoa nyerere kwa mengi lakini hili la vita vya kagera kamwe usimtetee iddi amini, mimi nina shaka na uraia wako, lazima wewe ni mganda na huenda unanasaba ya karibu sana na huyo nduli iddi amini.
zumbemkuu

Umeongea kweli kabisa tumlaumu Nyerere kwa mengine lakini kwa hili la vita he was very right to defend its people and land na hasara/lawama zingekuwa nyingi kama angemwacha Amini achukue ardhi yetu, ni kweli tulivamiwa ghafla sana Animi alikuwa amejiandaa tena vya kutosha akisaidiwa na Gaddafi, ni kweli kabisa mgambo wetu wengi walikufa kwa vile walikuwa hawana mafunzo ya kijeshi tulikuwa tunakushanywa vijijini na kukimbia mchaka mchaka siku moja tu kesho yake unapelekwa Kagera believe me kwa sababu wengine tulihusika na operation hiyo.

Kuna kipindi baada ya kama mwezi hivi Tanzania ilizidiwa baada ya kuvunjwa kwa daraja la mto kagera tukashindwa kusonga mbele lakini kwa kusaidiwa na warusi lilijengwa daraja la muda Amini alitumia wakati huo kuwaua wanajeshi wetu waliokuwa wameshavuka daraja kwa vile hawakuwa na msaada wowote. kuna kitu cha warusi kinaitwa BM Katyusha rocket launcher kilisaidia sana kilikuwa kinapiga umbali wa maili kama sikosei 10 na kuwafanya ma engineer wamalize lakini tayari tulikuwa tumeumizwa sana, binafsi natofautiana na Nyerere kwa mambo mengi lakini kwa vita ya Kagera nitamtetea hadi kesho.
 
sijaelewa hapo. Nyerere alimtusi mtu/watu au yeye ndiye alietusiwa? It should be remembered that the late nyerere was not god. Ingawa kuna mikakati ya kumfanya saint ili iwe kila alichofanya na alichosema ni kitakatifu. Siasa zina mizengwe sana.nyerere (1) fought for african liberalization(2) ameleta muungano(3) ameondosha ukabilapia(1) amepigana vita uganda kwa kutaka amrudishe swahiba wake obote madarakani(2) ameleta azimio la arusha na operation vijiji - vyote vilifeli(3) alisababisha mgao wa sukari na unga, sabuni ilikuwa hakuna, maduka hayana bidhaa. (4) ilikuwa hakuna uhuru wa kuongea, vyombo vya habari na uwekezaji.tumetoka mbali. Uzuri wa binadamu, hawakawii kusahau
(1) ni bora vita ya uganda alishinda kuliko vita ya ufisadi, mgao wa umeme iliyotushinda sasa na maandamano yasiyo na tija kila kukicha,(2) azimio la arusha lilishindwa kwa sababu nyerere hakutaka kudictate, alitaka watanzania waione nia thabiti katika maneno na matendo ya azimio hilo,ila tamaa za watanzania wachache na hasa wana ccm kipindi hicho hawakutaka usawa aliouwaza nyerere!(3) hakuna mzalendo kama nyerere, aliyeweza kufanya maamuzi magumu na kuyasimamia hata kama mabeberu wakiweka vikwazo.ndio maana aliona ni bora kuzalisha malighafi za kitanzania na zitumike tanzania kuliko kuruhusu soko holela!(4) ni km ilivyo tbc leo,haiwezi kuzungumzia mabaya ya rais,hata voice of amerika haiwezi kufanya hivyo!ni mtanzania gani wakati huo aliomba kuanzisha chombo cha habari akakataliwa hatuna ushahidi,hata hivyo nia ya ndani ya mwl na utashina utu wake vinamfanya watanzania tulio wengi tuendelee kumuona alikuwa kiongozi asiemithilika katika ulimwengu wa sasa!hauwezi ukaongea upuuzi kuhusu mwl mbele ya kadamnasi usipigwe mawe je bado leo hakuna uhuru wa kuongea,mbona bado watu tunamheshimu na kumuona kielelezo!hili sio kwa watu wa hali ya chini tu hata wasomi wa vyuo vikuu pindi wanapodai haki zao huimba ule wimbo maarufu wa " kama sio juhudi zako nyerere.....kama sio juhudi zako nyerere ....."hauwezi kupata urais wa nhi hii kutokana na kura za watanzania km utamponda mwl jukwaani!je bado hakuna uhuru mpaka leo?kubali ukweli mwl nyerere hafananishiki katika kizazi cha sasa!jaribu kufikiri km wewe ungekuwa rais leo ungekubali kufa maskini?kuishi kijumba km cha mwl?kusomesha wanao hapahapa bongo?kutenganisha famailia na uongozi?kujali nchi na wananchi kwa dhati km mwl?unaweza......??.....
 
... an angry dude like you ought to transform this anger into actions. Katiba mpya and the likes, ought to be one of the solutions. Some have rightfully gone further by identifying current CCM as enemy number four who has to... apopolewe mawe hadi afe!
 
Nakubali kwamba mwalimu alikuwa kiongozi mahiri; hilo siwezi kulipinga. Ninachokipinga ni justifications zako za kutetea mapungufu yake. He was HUMAN and NOT GOD NOR AN ANGEL.

Vita ya kagera na Umeme wa mgao ni two separate elements ambazo hazilinganishiki. Na sikumbuki hata mara moja kusema naunga mkono umeme wa mgao na kuzalisha umeme kwa utaratibu wa emergency; unless you just wanted to bring that as a justification of your lame argument.

Eti Mwalimu hakutaka ku diktate; unayajuwa yaliowakuta akina Bibi Titi Mohammed? Fukua upate uhalisia wa mambo. Kambona had to flee abroad, merely because he had a different view; sasa hapo utasema nini nini hicho? Mwalimu alisimamia 'fikra sahihi za mwenyekiti' wakati wote; ukileta valangati hata ya ku kunja uso - RUPANGO!

Ishu ya kutosikiza mabeberu ni sahihi; ila alipaswa kuleta maendeleo na sio tu kutowasikiza mabeberu. Kweli makao makuu ya ukombozi wa nchi za afrika yalikuwa DSM na kuna wakati yakiongozwa na Brigedia General Hashim Mbita. tumechangia sana katika kukomboa Afrika; ikiwemo Afrika ya Kusini ambao hadi hivi karibuni walikuwa wamesahau fadhila na kuwataka watanzania waingie kwa viza. Ila kuwakatalia mabeberu sio kuwanyima wananchi basics. mbona Cuba na China walifanikiwa na sisi ndio ilikuwa mifano yetu? Poor management and supervision. Yeye alikuwa akiona TV ya Satelite IKULU, sawa? Kama hakutaka kusomesha familia yake au sijui unasema kitu gani, hilo ni shauri lake; ila kusomesha familia yako sio ufisadi; tena una wajibu wa kufanya hivyo kama mzazi.

Kuhusu TV, si angeruhusu walau Watanzania Bara waangalie TV; kule Zanzibar Karume alifungua kituo cha kwanza cha Runinga coloured 1964. Yeye tangu 1961 - 1985; hata TV????? That was shameful. Kwani ilikuwa lazima afungue cha mtu binafsi, kwani ile ya Zanzibar ya mtu binafsi?

Kuhusu NYUMBA; Nyerere hakuwa na mpango wa kustaafu na alijua atafia IKULU. Mwinyi alimuenzi kwa kumpatia Nyumba ya Msasani na kuagiza jeshi wamjengee jumba la kipekee kule Butiama. Ushafika ukaliona hilo Jumba; kwako wewe lile Banda?

Mwisho, kama alitaka kuishi kama mtanzania, angefia Muhimbili au sana sana India. Yeye ni mbinafsi as any other leader. Ana mafanikio na ana mapungufu PERIOD.

Kuhusu hiyo nyimbo; ni kwa kuwa ndio slogan ya kufanya rioting; haina any significance what so ever.

(1) ni bora vita ya uganda alishinda kuliko vita ya ufisadi, mgao wa umeme iliyotushinda sasa na maandamano yasiyo na tija kila kukicha,(2) azimio la arusha lilishindwa kwa sababu nyerere hakutaka kudictate, alitaka watanzania waione nia thabiti katika maneno na matendo ya azimio hilo,ila tamaa za watanzania wachache na hasa wana ccm kipindi hicho hawakutaka usawa aliouwaza nyerere!(3) hakuna mzalendo kama nyerere, aliyeweza kufanya maamuzi magumu na kuyasimamia hata kama mabeberu wakiweka vikwazo.ndio maana aliona ni bora kuzalisha malighafi za kitanzania na zitumike tanzania kuliko kuruhusu soko holela!(4) ni km ilivyo tbc leo,haiwezi kuzungumzia mabaya ya rais,hata voice of amerika haiwezi kufanya hivyo!ni mtanzania gani wakati huo aliomba kuanzisha chombo cha habari akakataliwa hatuna ushahidi,hata hivyo nia ya ndani ya mwl na utashina utu wake vinamfanya watanzania tulio wengi tuendelee kumuona alikuwa kiongozi asiemithilika katika ulimwengu wa sasa!hauwezi ukaongea upuuzi kuhusu mwl mbele ya kadamnasi usipigwe mawe je bado leo hakuna uhuru wa kuongea,mbona bado watu tunamheshimu na kumuona kielelezo!hili sio kwa watu wa hali ya chini tu hata wasomi wa vyuo vikuu pindi wanapodai haki zao huimba ule wimbo maarufu wa " kama sio juhudi zako nyerere.....kama sio juhudi zako nyerere ....."hauwezi kupata urais wa nhi hii kutokana na kura za watanzania km utamponda mwl jukwaani!je bado hakuna uhuru mpaka leo?kubali ukweli mwl nyerere hafananishiki katika kizazi cha sasa!jaribu kufikiri km wewe ungekuwa rais leo ungekubali kufa maskini?kuishi kijumba km cha mwl?kusomesha wanao hapahapa bongo?kutenganisha famailia na uongozi?kujali nchi na wananchi kwa dhati km mwl?unaweza......??.....
 
zumbemkuu

Umeongea kweli kabisa tumlaumu Nyerere kwa mengine lakini kwa hili la vita he was very right to defend its people and land na hasara/lawama zingekuwa nyingi kama angemwacha Amini achukue ardhi yetu, ni kweli tulivamiwa ghafla sana Animi alikuwa amejiandaa tena vya kutosha akisaidiwa na Gaddafi, ni kweli kabisa mgambo wetu wengi walikufa kwa vile walikuwa hawana mafunzo ya kijeshi tulikuwa tunakushanywa vijijini na kukimbia mchaka mchaka siku moja tu kesho yake unapelekwa Kagera believe me kwa sababu wengine tulihusika na operation hiyo.

Kuna kipindi baada ya kama mwezi hivi Tanzania ilizidiwa baada ya kuvunjwa kwa daraja la mto kagera tukashindwa kusonga mbele lakini kwa kusaidiwa na warusi lilijengwa daraja la muda Amini alitumia wakati huo kuwaua wanajeshi wetu waliokuwa wameshavuka daraja kwa vile hawakuwa na msaada wowote. kuna kitu cha warusi kinaitwa BM Katyusha rocket launcher kilisaidia sana kilikuwa kinapiga umbali wa maili kama sikosei 10 na kuwafanya ma engineer wamalize lakini tayari tulikuwa tumeumizwa sana, binafsi natofautiana na Nyerere kwa mambo mengi lakini kwa vita ya Kagera nitamtetea hadi kesho.

Self defense ni fair game, but why offensive? hapo ndipo Nyerere alipoanza propaganda za kwenda kumtoa Idd Amin. Kuna watu wa karibu ambao wanasema kwamba uamuzi wa Nyerere kwenda kumtoa Idd Amin ulikuwa zaidi ubinafsi wake Nyerere, na kutaka kulipiza visasi, ni fact. Gharama za vita zimeicost TZ mabilion ya hela. Baada ya vita Nchi ilikuwa taabani kuanzia 1981,82,83, hadi ilipofika 85, Mzee Nyerere ikabidi aachie ngazi, ni facts. Let's be honest
 
Nyerere mobilized his citizen army reserves and counterattacked, joined by Ugandan exiles united as the Uganda National Liberation Army (UNLA). The Ugandan Army retreated steadily, expending much of its energy by looting along the way. Libya's Qadhafi sent 3,000 troops to aid fellow Muslim Amin, but the Libyans soon found themselves on the front line, while behind them Ugandan Army units were using supply trucks to carry their newly plundered wealth in the opposite direction. Tanzania and the UNLA took Kampala in April 1979, and Amin fled by air, first to Libya and later to a seemingly permanent exile at Jiddah, Saudi Arabia. The war that had cost Tanzania an estimated US$1 million per day was over.
*****
In the fall of 1978, Ugandan troops, under orders from dictatorial president-for-life Idi Amin (1925-), invaded northern Tanzania and, after blowing up the only bridge over the Kagera River, occupied about 700 square miles of foreign territory, called the Kagera Salient. In response, President Julius K. Nyerere (1922-) of Tanzania sent an army, reinforced by Ugandan exiles who had fled their homeland to escape Amin's tyrannical rule, across the border into Uganda (October 1978). Soon the invaders were advancing through southern Uganda after winning some skirmishes. They surrounded the Ugandan capital of Kampala, but were halted briefly by a Libyan force that had come to Amin's aid. On April 11, 1979, Tanzanian troops and Ugandan exiles and nationalists entered Kampala, whose residents welcomed them as liberators. Eluding capture, Amin fled to Libya and left behind an impoverished Uganda and a brutalized people. During the eight years of his rule, he had expelled all Asians, killed thousands of tribespeople and Christians, spent excessively to build up his army, and nationalized all land without compensating the owners.
 
Sijaelewa hapo. Nyerere alimtusi mtu/watu au yeye ndiye alietusiwa? It should be remembered that the late Nyerere was not God. Ingawa kuna mikakati ya kumfanya Saint ili iwe kila alichofanya na alichosema ni kitakatifu. Siasa zina mizengwe sana.

Nyerere

(1) Fought for African Liberalization
(2) Ameleta Muungano
(3) Ameondosha ukabila

Pia

(1) amepigana vita Uganda kwa kutaka amrudishe swahiba wake Obote madarakani
(2) Ameleta azimio la Arusha na operation vijiji - vyote vilifeli
(3) Alisababisha mgao wa sukari na unga, sabuni ilikuwa hakuna, maduka hayana bidhaa.
(4) Ilikuwa hakuna uhuru wa kuongea, vyombo vya habari na uwekezaji.

TUMETOKA MBALI. Uzuri wa binadamu, hawakawii kusahau

Nyerere hakuwa malaika, na indeed mambo mengi aliyakosea lakini always IN GOOD FAITH!
Mwalimu(R.I.P.) aliwahi kusema" sisi tuna mambo mengi tu mabaya tumefanya - lakini yapo na machache mazuri tuliyofanya(how modest he was!) lakini nashangaa waliokuja baada yetu wameendeleza yale mabaya na kuacha machache mazuri tuliyokuwatumefanya!!" nafikiri hata hii inapatikana katika famous Karimjee 1995 press conf - I MISS YOU MWALIMU.

Nyerere alikuwa Rais wa Tanzania kwa miaka 27 na underline 27 - hakuwa na nyumba ya maana pale Butiama na ikabidi JWTZ wamzawadie nyumba baada ya kustaafu, Dar alikuwa na nyumba moja maeneo ya magomeni na ya pili very modest maeneo ya msasani. Linganisheni na watawala (SIO VIONGOZI)wenu wa leo...WIZI MTUPU!!!!!!

Mwalimu ameugua na alikuwa London kwa matibabu hakuwa na nyumba pale na ninakumbuka wakati Makongoro(then in NCCR Mageuzi) alipokuwa anataka kwenda kumtembelea baba yake na ku-complain ktk vyombo vya habari kuwa hana sehemu ya kufikia, ni mzee Cheyo aliyejitolea kumpatia nyumba yake pale London ili jamaa(Makongoro) afikie pale - huyo ndio alikuwa KIONGOZI si akina malecela ambao tunasikia wanamajumba NYC...again WIZI MTUPU!!!
 
I believe amin was pro swahili.

The only problem between amin and nyerere was obote ousted.

Ile vita haikuwa kwa maslahi ya tanzania na watanzania.

Inasemekana kwamba moja ya sababu za Gaddaffi kumsaidia Idd Amin dhidi ya TZ ni kwa sababu Idd Amin alikuwa Mwislamu....... I hope hatumwangalii Idd Amin kama mwislamu bali dikteta aliyeivamia nchi yetu.
 
Ngondya,
Gaddaffi alijagundua baadaye kuwa amedanganywa na Amin na akaomba msamaha kwa Julius Nyerere. Ndiyo sababu Amin alihamia Saudi Arabia.
 
Nyerere hakuwa malaika, na indeed mambo mengi aliyakosea lakini always IN GOOD FAITH!Mwalimu(R.I.P.) aliwahi kusema" sisi tuna mambo mengi tu mabaya tumefanya - lakini yapo na machache mazuri tuliyofanya(how modest he was!) lakini nashangaa waliokuja baada yetu wameendeleza yale mabaya na kuacha machache mazuri tuliyokuwatumefanya!!" nafikiri hata hii inapatikana katika famous Karimjee 1995 press conf - I MISS YOU MWALIMU.Nyerere alikuwa Rais wa Tanzania kwa miaka 27 na underline 27 - hakuwa na nyumba ya maana pale Butiama na ikabidi JWTZ wamzawadie nyumba baada ya kustaafu, Dar alikuwa na nyumba moja maeneo ya magomeni na ya pili very modest maeneo ya msasani. Linganisheni na watawala (SIO VIONGOZI)wenu wa leo...WIZI MTUPU!!!!!!Mwalimu ameugua na alikuwa London kwa matibabu hakuwa na nyumba pale na ninakumbuka wakati Makongoro(then in NCCR Mageuzi) alipokuwa anataka kwenda kumtembelea baba yake na ku-complain ktk vyombo vya habari kuwa hana sehemu ya kufikia, ni mzee Cheyo aliyejitolea kumpatia nyumba yake pale London ili jamaa(Makongoro) afikie pale - huyo ndio alikuwa KIONGOZI si akina malecela ambao tunasikia wanamajumba NYC...again WIZI MTUPU!!!
Mkuu, ebu tujuze kidogo Cheo huyu wa UDP ndio kanunua nyumba London?
 
Ndiye huyo huyo. Haitwi bwana Mapesa kwa bure.
posho hizo za Ubunge mpaka kanunua Nyumba London, Mbezi beach pia kajenga nyumba, Mwanza pia kajenga nyumba, Kwa bariadi pia nyumba!! Nchi hii ufisadi kila kona, vyama vya upinzani, magamba! Sijui tutakimbilia wapi
 
Hapana. Hizo hela alizonunulia nyumba London alizikwapua Swaziland.
 
Inasemekana kwamba moja ya sababu za Gaddaffi kumsaidia Idd Amin dhidi ya TZ ni kwa sababu Idd Amin alikuwa Mwislamu....... I hope hatumwangalii Idd Amin kama mwislamu bali dikteta aliyeivamia nchi yetu.

Nadhani umeona clearly nimesema Obote ELEMENT; hilo suala la dini unalileta ili ku derail majadiliano. Main argument yangu, na itabakia hivohivo, ni kwamba :-

(1) Kulinda mipaka yate ni wajibu wetu kikatiba.
(2) Kuondosha uongozi na kuanza kupandikiza wa kwetu wa UNCALLED for.

Ile vita imegharimu Tanzania na Uganda; kwani sisi tulikula hasara ambayo kama ile fedha Mwalimu angeitumia kusimamia mipango kabambe ya Azimio la Arusha; pengine ingekuwa Success Story. Aidha, Uganda tumewatandika; tukawarudisha nyuma, na zaidi ya hapo; tukaweka utawala legelehe; ikawa mapinduzi ndio utamaduni hadi alipoingia General M7. Pamoja na M7 kuingia, kuna akina kony.

We should regret for that and not shy away from admitting that the offensive policy was a DISASTER.
 
Article ni nzuri. Lakini hakuna mahali inasema UN ilimlaani Nyerere kwa uvamizi huo. In fact UN ilikaa kimya. OAU ilijaribu upatanishi kwa kumtaka Nyerere aondoe majeshi yake. Nyerere aliiambia OAU ilaani kwanza uvamizi wa Uganda nchini Tanzania. Hawakufanya hivyo.

Kulinda raia wako mpaka UN wakuruhusu..?? Linda raia na mipaka yake mengine yatafuatia..
 
Nyerere hakuwa malaika, na indeed mambo mengi aliyakosea lakini always IN GOOD FAITH!
Mwalimu(R.I.P.) aliwahi kusema" sisi tuna mambo mengi tu mabaya tumefanya - lakini yapo na machache mazuri tuliyofanya(how modest he was!) lakini nashangaa waliokuja baada yetu wameendeleza yale mabaya na kuacha machache mazuri tuliyokuwatumefanya!!" nafikiri hata hii inapatikana katika famous Karimjee 1995 press conf - I MISS YOU MWALIMU.

Nyerere alikuwa Rais wa Tanzania kwa miaka 27 na underline 27 - hakuwa na nyumba ya maana pale Butiama na ikabidi JWTZ wamzawadie nyumba baada ya kustaafu, Dar alikuwa na nyumba moja maeneo ya magomeni na ya pili very modest maeneo ya msasani. Linganisheni na watawala (SIO VIONGOZI)wenu wa leo...WIZI MTUPU!!!!!!

Mwalimu ameugua na alikuwa London kwa matibabu hakuwa na nyumba pale na ninakumbuka wakati Makongoro(then in NCCR Mageuzi) alipokuwa anataka kwenda kumtembelea baba yake na ku-complain ktk vyombo vya habari kuwa hana sehemu ya kufikia, ni mzee Cheyo aliyejitolea kumpatia nyumba yake pale London ili jamaa(Makongoro) afikie pale - huyo ndio alikuwa KIONGOZI si akina malecela ambao tunasikia wanamajumba NYC...again WIZI MTUPU!!!

KALOLOKOLA VIII

1. Nyerere Kwa Nafasi ya Waziri Mkuu na Rais alikaa miaka 25 na sio 27; najua ni typing error; but we put the records straight.
2. Nyerere alikaa miaka 7 akiwa mwenyekiti wa CCM baada ya kustaafu kwake. Wadadisi wa mambo walisema kuwa alipenda kuwa na madaraka.
3. Nyerere hakuwa na mpango wa Kustaafu, alikuwa na mpango wa kufia IKULU; ila baada ya hali kuwa sio hali akang'atuka. Sasa nyumba ya nini?

Sijui Mali za Malecela, ila sidhani kama ana majumba hayo usemayo. Watu kwa kuwazushia hawa vingozi ndio wenyewe. Tuliambia Sumaye ndio mwenye mali zote za bakhresa kabla ya Uchaguzi wa 2005. Tuliambiwa RAha Towers ni ya Mama Sitti, jamani; twende walau na a bit of evidence
 
Back
Top Bottom