Sio propanganda mzee mimi nilikuwepo Mwanza wakati ule uliza waliokuwepo Mza kuna jet zililenga kuipiga hospitali ya Bugando
bahati zikarudishwa na kuangusha makombora kisiwa cha saanane, kuna nyumba nyingi tu zilipigwa mabomu mjini Mwanza
sasa unaposema zilikuwa propaganda za Nyerere nakushangaa mkuu.
Nazungumzia offensive ya kuingia ndani ya Uganda kumtoa Idd Amin, ambayo ilipingwa vikali na OAU, Western, hadi Nigeria wakatoa statement kali kuhusu uamuzi wa Nyerere wa kuivamia Uganda.
Self defense ni fair game, but why offensive? hapo ndipo Nyerere alipoanza propaganda za kwenda kumtoa Idd Amin. Kuna watu wa karibu ambao wanasema kwamba uamuzi wa Nyerere kwenda kumtoa Idd Amin ulikuwa zaidi ubinafsi wake Nyerere, na kutaka kulipiza visasi, ni facts.
Ile mistake ya Nyerere kuivamia Uganda ndiyo ilichangia sana kufeli kwa Nyerere ktk 1981,82,83 mpaka akafeli kabisa 85, akaamua kuachia ngazi. Ni mistake ambayo aliifanya, kwa sababu hakupata support yoyote kutoka international community. Na hiyo ni moja ya sababu ya Nyerere kupoteza umaarufu wake internationally.