Usia kwa wasanii wa Bongo Movie na Bongo Flavour

mdundo ngoma sana

JF-Expert Member
Jan 2, 2016
1,002
954
Naona mnajisahau duniani na kuona kila kitu ni halali.mnabadilishana waume kwa wanawake kuhalalisha uzinifu wenu. Mmewekeza kwenye ngono na kuipa jina la kutafuta "kick".

Mmekuwa walevi kupindukia.wengine mlilewa sifa mkazama kwenye madawa ya kulevya sasa mnataka kuhurumiwa, mnajidunga masindano ili makalio yawe makubwa kuridhisha nafsi zenu zilizosheheni pombe na ngono.

Mnajivika ustaarabu pale mnapopata misiba ndio haswa wakaa uchi nyie mnakuja na mavazi ya staha.

Kumbukeni mnafanya kazi ya shetani kwa asilimia mia. Nyimbo zenu ni nzuri sana pale zinaposindikizwa na pombe.

ENYI WASANII SIKILIZENI IWAINGIE AKILINI. Kuna uzee unakuja umejipanga vipi kukabiliana nao? Kuna maisha baada ya kufa je duniani myafanyayo ni mema? We choma sindano ongeza makalio, wewe imba kusifia pombe na ngono, wewe tafuta kiki kwa kubadilisha wanawake na wanaume KUMBUKA SAA ILE YAJA MTAJIBIA TU.

TAFAKARI WALIOTANGULIA MIAKA YA ELFU MBILI TU HAWAJAAMKA HADI LEO. IPENDE DUNIA KWANI DUNIA NI JELA KWA WATENDA MEMA NA NI PEPO KWA WENYE KUKUFURU!
 
Topic hii murua kabisa.

Umetoa ujumbe mzuri sana ila hawazingatia isipokuwa WENYE AKILI SALAMA.
 
Back
Top Bottom