Ushuru wa mabasi na kauli za wanasiasa.

mnduoeye

Senior Member
Jun 30, 2012
166
73
Ndgu zangu wana J.F juzi tarehe 6.9 nilisoma kwenye gezeti la Mwananchi kuhusu ushuru wa mabasi kituo kikuu cha mabasi Manispaa ya Moshi nikashangazwa pia na matamshi ya Katibu wa Akiboa Bw MRUTU.Sijaamini kama kauli hiyo ilitolewa nae au mtu mwingine na kwa kuwa hajakanusha basi nalazimika kuamini hiyo ni kauli yake;

Katika Mkoa huu wa Kilimanjaro njia ya kuelekea Dar kuna vituo vitatu vya mabasi ambavyo ni kituo kikuu,kituo cha Njia panda na kituo cha Mwanga.Kituo kikuu cha Manispaa kina ubora kuliko vyote kikiwa na huduma zote ikiwemo eneo kubwa la kuegesha mabasi,huduma za migahawa,maduka .maji na umeme nyakati za usiku hivyokituuo hicho kuwa na usalama usiku.Kituo cha Njia Panda ndio kinachofuatia lakini hakina eneo kubwa na huduma ni duni kidogo.Kinachofuatia ni kituo cha Mwanga ambacho hakina huduma yeyote kuanzia maegesho hakuna,huduma hakuna ni eneo tu pembeni ya barabara limetengwa kwa ajili ya kukusanyia ushuru Kinachonisukuma sasa kuhoji matamshi ya katibu wa Akiboa ni hili:

Katibu huyo ni Diwani wa muda mrefu katika halmashauri ya wilaya ya Mwanga.Ni mmajawapo wa waliopitisha sheria ya ushuru halmashauri ya Wilaya ya Mwanga ambako hakuna huduma ya namna yeyote katika kituo hicho.Na zaidi amashiriki kupitisha sheira ya kupandisha ushuru kufikia shs 1,500 na sheria hiyo itaanza kutumika mara Waziri mwenye dhamana akiipitisha.Hapo ndio nilikoshindwa kumwelewa katibu huyo.

Kwa nini ameishupalia Manispaa ya Moshi au kwa kuwa inaongozwa na CDM?Haoni huduma zinazotolewa kituo kikuu cha Manispaa ukilinganisha na ule uchochoro wa kukusanya ushuru pale Mwanga? Atatuambia nini halmashauri yake itakapopokea sheria ya kupandisha ushuru wa Mwanga ataratibu mgomo kupinga maamuzi aliyoyashiriki?

Je ukandamizaji anaoufanya kituo cha mabasi Moshi cha kutumia vijana kukusanya fedha kwa wasafirishaji kwa kisingizio cha kilo hawaogezei mzigo wafirishaji wenzake ?MWAMBIENI ATUPE MAJIBU NA HAO NDIO WANASIASA NA KAULI ZAO
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom