Ushuru wa biashara!

shogholo

Member
Aug 2, 2010
7
0
Wandugu wa JF, naombeni mnisaidie kwa wale wenye uzoefu au utaalam wa biashara! Mimi nina mtaji kidogo tu kiasi cha (millioni kumi tu), ila nimeshindwa kuanza biashara kwani kila ninapopiga mahesabu naona kama mtaji wangu ni mdogo, hivyo naomba msaada wa mawazo nifanye biashara gani ambayo itaweza kuwa endelevu kwa kiwango hicho?
 
Bwana Shogolo
Jee unafanya shughuli gani? umesomea nini na jee unapenda kufanya kitu gani? Haya ni maswali muhimu kujiuliza kabla hujaamua kufanya biashara yoyote. Kutokana na tiofauti tulizonazo binadamu katika vipaji kuna baadhi ya biashara huziwezi kwa sababu huna kipaji nazo au huzipendi. Ili kujibu Swali lako natakiwa kwanza nikague vipaji vyako ndiyo nikushauri ufanye biashara gani. Kwa suala la mtaji mtaji ulionao ni wa kutosha kuanzisha biashara tatizo ni biashara gani ufanye.
Naomba nitafute nikushauri nipigie simu namba 0755394701. Mimi ni mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri.
 
Kwa kuongezea, biashara yoyote ya kutafuta faida ya hela, ifuatavyo: 1. Jua hela zitaingia vipi na zitatoka vipi, 2. Jua wateja wako wapi. 3. kuna kitu gani wewe utafanya tofauti na wenzio waliokutangulia ambao wako tayari wanaendelea na biashara na wengine wamekwenda muflis. 4. Uendeshaji wa biashara, je utahiji mfanya kazi? je utahitaji machines. au serikali inahiji vibali, liseni zipi. 5. Je una plani ya baadae kazi ikishaanza? yani kuifanya biashara idumu.

Haya maswali zio magum, lakini yanahiji uangalifu. Kuwasiliana na Babalao ni kitu muhimu. Hata Mjasirimali wa Kashata kwa tangawizi, hujibu haya maswali yote. Kwa kua biashara yake ni ndogo na mahesabu machache basi hufanya hizi taratibu moja mpaka tano, kichwani.
 
Mkuu, kama una milioni kumi mkononi lakini unaona kama haitoshi basi inawezekana unajiwekea malengo makubwa mno (hilo nitatizo!), ushauri wangu kama ni mkopo basi ulifanya haraka sana kuuchukua kabla haujajua utaufanyia nini, kama ni vyanzo vingine ni vizuri ukaiweka bank kwanza uwaze na kupata wazo utalolimudu (pia inategemea uko wapi).....Usitegemee sana mawazo ya kuanzishiwa, anzisha mawazo yako kadhaa kwanza kisha tafuta ushauri kwa wadau kama humu! all the best.
 
Ziweke kwanza katika Fixed Deposit benki unapotafuta na kupangilia biashara ya kufanya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom