Ushuri wenu tafadhali

Kweli kazi si kupenda bali kazi ni kumpenda akupendaye....... kaza msuli kijana labda utafanikiwa cha muhimu uupate ukweli ili hata unapoamua kumwacha uwe na sababu ambazo zinaeleweka vinginevyo utaonekana haukua serious.
Kila la kheri

Akiamua kupiga chini yeye apige chine tu coz mimi naona hapo jamaa anajitwisha gunia la misumari wakati amenyoa kipara
 
huyo si mke kijana kwa umri wake kimawazo bado kabisa, kila utachokifanya au atakachokuhisi kitakuwa hewani mtaa wa pili au atakimbilia kusema kwa mama na maisha ndani hayaendi hivyo.
kufunga ndoa si sherehe tu au tendo la ndoa pekee yake , ndoa ni kuaminia, kuvumiliana, kusaidiana kuwa mwili mmoja na kitu kimoja hali na mali, sasa kama amekupendea mali ukifulia je? atakupenda?
mchunguzi kama vp jikatae taratiiibu! vuta subira utampata aliye wako toka kwa mungu
 
Sijasoma thread nzima lakini dogo nataka nikuambie jambo moja.Huyo g/friend wako lazima mtaachana tu.Unapoanza uhusiano na mwanamke mwenye umri chini ya miaka 25 lazima mtakuja kuachana tu!
Eiyer ma swt bro are you real serious hapo kwenye red?

anyway to me huyu binti hakufai kabisa aisee. kwanza anaonekana siyo mkweli sikwambii chungua bali achana nae kwani maisha ya uchumba bana ni ya maamuzi mara moja tu. unajua in life you only have one chance to choose and you choice must be perfect and appropriate. usiende ukisema akimrudia mlinzi niatmuacha nikatafute mwingine. NO.

chagua kwa akili ikitokea amebadilika iwe ni kwa jambo jipya ila siyo jambo ambalo ulishawah kuliona ama kulihisi huko nyuma. tafuta binti ambaye anakupenda kwa dhati ila huyu wa mguu nje mguu ndani sikushauri
 
Last edited by a moderator:
Naamini hii yaweza kunisaidia....... jambo ambalo nimejifunza kwa mwenzangu huyu ni kuwa anapoona tatizo kwangu badala ya kuniambia utakuta anaenda kumwambia mtu mwingine. kuna maneno ambayo ninaongea nae tu lakini nashangaa nayakuta kwa watu wengine eti alienda kuomba ushauri. Nimejaribu kumwambia kua km anaona tatizo kwangu ni heri aniambie mimi kwanza kabla ya kwenda kumwambia mwingine so najikuta hata tukioana kuna mambo ya ndani yatakua yanatoka nje.

Nilipomuuliza kuhusu huyo jamaa mlinzi mchumba wangu aliniambia kuwa ni kweli jamaa aliwahi kumtokea lakini yeye binti hakumkubalia ila kinachonichanganya ni kuwa jamaa mwenyewe nafahamiana nae vizuri na ktk hali ya kumdadisi jamaa amekataa kuwa hajawahi kumtokea huyo binti na hapa ndipo ninapopata wasiwasi na ninaona kuna kitu kimejificha ambacho sikijui....
Nakushukuru kwa hizo hints

mdogo wanu sijui mwanangu nmequote hii post makusudi na naomba niiwekee bold post yote kuonyesha msisitizo wa huu ushauri wangu kwako.

kwa hili la kutoa siri huyu bini hafai kabisa. kwa maelezo yako ya yenye kuonyesha nidham ya hali ya juu naomba nikwambie mapungufu ya huyo binti:
- umri its not a big deal so long as ni mentally matured.
-ni mtu asiyekuwa na kifua so tegemea kuyakuta ya chumbani sebuleni.-
-ni binti asiyekuwa na upendo wa dhati kabisa kwako ni mpeda hela
-ni binti atakaye kulipia kisasi siku ukikosea
-ni binti ambaye akili yake bado haijakomaa.
-hana nidham wala heshima hata kidogo kwako

kutokana na mapungufu yote haya hana quality yeyote ya kuwa mke manake sifa za mke ni hizi hapa
-awe msiri na muadilifu
-asiwe mlipa kisasi
-awe amekomaa na kupevuka kiakili
-awe na upendo wa dhati na heshima kwako.
-awe mvumilivu

hizi ndizo tabia za wamama wote unaowaona wako kwenye ndoa hadi leo. so kama hana huyu mchumba wako usijaribu ma dear brother

dada yangu mpendwa gfsonwin yan kila nisomapo comment zako huwa nafarijika sana. mtoa mada je umemsoma huyu mamy? ushauri wake watosha bila nyongeza. . .
 
Last edited by a moderator:
huyo si mwanamke wa kuoa by any standards, piga chini haraka sana kabla hujapewa dozi nzito ya maumivu
 
mdogo wanu sijui mwanangu nmequote hii post makusudi na naomba niiwekee bold post yote kuonyesha msisitizo wa huu ushauri wangu kwako.

kwa hili la kutoa siri huyu bini hafai kabisa. kwa maelezo yako ya yenye kuonyesha nidham ya hali ya juu naomba nikwambie mapungufu ya huyo binti:
- umri its not a big deal so long as ni mentally matured.
-ni mtu asiyekuwa na kifua so tegemea kuyakuta ya chumbani sebuleni.-
-ni binti asiyekuwa na upendo wa dhati kabisa kwako ni mpeda hela
-ni binti atakaye kulipia kisasi siku ukikosea
-ni binti ambaye akili yake bado haijakomaa.
-hana nidham wala heshima hata kidogo kwako

kutokana na mapungufu yote haya hana quality yeyote ya kuwa mke manake sifa za mke ni hizi hapa
-awe msiri na muadilifu
-asiwe mlipa kisasi
-awe amekomaa na kupevuka kiakili
-awe na upendo wa dhati na heshima kwako.
-awe mvumilivu

hizi ndizo tabia za wamama wote unaowaona wako kwenye ndoa hadi leo. so kama hana huyu mchumba wako usijaribu ma dear brother

mtoa mada naona atakuwa ameelewa vizuri zaidi.........
 
tupa kule hakufai huyu....siku zote mwizi huwa anadhani wa2 wote ni wezi.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom