Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
This is a b..... f..... government and their leaders -- kuendekeza vitu vya imani huku watu wanakufa. Katika miaka ya mwanzoni ya 80 Nyerere alimfukuza kasi DC mmoja (enzi hizo wakiitwa ma-AC) Idi Sungura kwa kuendekeza mambo kama haya.
Gazeti la The African la Jumamosi hii lina habari ukurasa wa mbele kuhusu malalamiko ya mratibu wa masuala ya HIV/Aids Mkoa wa Manyara aitwaye Elizabeth akisema tangu Babu aanze tiba yake wanaokwenda kupima vvu kwa hiari kutoka mkoa huo na wale wanaoutumia ARVs imepungua sana. Gazeti lilimnukuu mratibu huyo akilalamika kwamba wanaogua ukimwi hawaendi kupata dawa zao kama zamani na akasema kwamba wala hawaendi kupima tena wanaporudi baada ya kupata kikombe kwa babu.
Hii sasa ni hatari -- ile kampeni nzima ya JK aliyoanzisha ya kupima vvu kwa hiari sasa inakufa na watu wanakufa, huku yeye mwenyewe wala hatoi tamko lolote -- kwa mfano kuwahimiza wale wenye vvu wakitoka kwa Babu waendelee na ARvs.