Ushuhuda: Nilikimbia Ualimu Kuepuka Matatizo

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,179
85,337
Tumekusanyika wote, tumependeza kweli, ni kozi mbalimbali na tumetengwa vivyo hivyo!! Mimi nahitimu kozi ya Elimu ya Watu wazima (Bachelor of Education in Adult Education) ni furaha kweli. Ila kuna kitu kinaniumiza sana kila nikikumbuka shule niliyopangiwa.

Kweli hii si shule bali ni majengo tu, hayana madirisha mazuri, sakafu chafu, imetoboka toboka! Nashindwa kufundisha kutoka na vumbi lile, ubao wa kufundishia haueleweki, ofisini sina hata rula, inabidi nijinunulie kalamu! Lakini mbaya zaidi ni hawa wafuatao; wanafunzi wawili wenye ulemavu wa viungo, inabidi wakae chini pale mbele maana hawawezi kukaa kwenye madawati na pia baskeli zao hazipiti kwenye milango ya madarasa. La pili, wanafunzi wangu wanaonekana kukata tamaa ya maisha kabisa na kila ninavyojaribu kuwaelimisha hawaonekani kabisa kunielewa. Wanauliza maswali magumu kuliko uwezo wa kuyajibu, hawana maabara hata moja, kuna gunia moja na box ambalo tumehifadhia mifano ya test tube, spatula na n.k

Walimu wenzangu nao wanaonekana wamefika mwisho wa maisha yao, ni walevi wa kutupwa (si walaumu) na nguo zao zinaonyesha fadhaiko kubwa na kukata tamaa kwa hali ya juu, ni kilio kikubwa. Niko kwenye nyumba ya kupanga, naonekana kama ndio Mungu wao, mwenyewe nimepigika!

Siku moja nikaenda Halmashauri kufuatilia madai yangu, nilichokikuta ilikua ni pigo jingine, kauli za wahasibu wale zilinikatisha tamaa sana sana, ni kauli zilizojaa jeuri na kiburi, mbaya zaidi namuona kijana mmoja ambae tulimaliza mwaka mmoja kwa kozi tofauti (Accounts) ni mmoja wa wahasibu/cashier wa pale, yeye anapendeza jamani si haba hakuna ulinganisho wa mimi na yeye kwa namna yoyote ile. Naelekea kwenye ofisi za TSD huko nako nakuta kituko majibu ya hovyo sana, roho inauma sana.

Ninaporudi jioni nimechoka sana maana hata basi la kurudia kwangu nililikosa na hivyo kupanda Landrover, nimejaa vumbi sana, nimechoka na kesho natakiwa tena niwepo darasani nifundishe wanafunzi wangu!!! Usiku ule unakuwa usiku wa maumivu makali sana kwangu, nikijiuliza kuwa kwanini nilifanya chaguo baya? Maana nilifaulu kwa kiwango cha Division One point Seven kwa form six.

Asubuhi naamua kuongea na wanafunzi wangu badala ya kufundisha tu kila siku, tunabadilishana mawazo, maana si mwalimu wala si wanafunzi wanaoneka wana ari ya kusoma tena!!!!! Nawauliza, ni wapi alipo Asha Amiri? wanacheka na mmoja anasimama na kuongea kwa kejeli, "ameshaolewa, yaani mwalimu huna habari?"

Ni jioni sasa, nipo nje pale nyumbani, wanakijiji wanaendelea na shughuli zao, huyu anachota maji hawa wanarudi machungani, nina kiredio kidogo nasikiliza nisichokielewa! Maana hakika mawazo yangu yako mbali sana, ile degree haina maana tena, sina wa kumfundisha maarifa yale! Naonekana kituko pale kijijini kwa kutaka kuwafundisha watoto wale!!! Ghafla, napata ujasiri wa ajabu, yes ujasiri wa ajabu sana. NIMEAMUA KUACHA KAZI. Kesho ni Ijumaa kwa hio nitaomba niende mjini mara moja lakini hapo ndipo mwisho wa kukaa hapa.

Narudi mjini na kuamua kuanza maisha ya tofauti sana na kujaribu kuisahau ndoto ile kwamba ningekuwa Mwalimu mzuri, nimeachana na vituko vya kukatwa pesa ya MWENGE kwa ajili ya kufungua miradi ya watu binafsi, nimeachana na maumivu yale ya kudharauliwa na watumishi wenzangu walioko halmashauri, sijawahi pia kukaa nikafahamu mshahara wangu ni shilingi ngapi hasa, maana kila siku unabadilika kwenye payslip.

Walimu wana haki sawa na watumishi wengine, tuwapende, tuwajali na tuwatunze!!!

Mwalimu Elli
 
Kama naivuta hii picha ya Mwalimu Elli, nina mdogo wangu ni mwalimu acha nimpigie simu nijue kinaendelea nini maana inauma sana.
 
Asante sana kwa mchango wako huu. Inasikitisha kuona wanayotendewa walimu. Hivi, ikifika simu WALIMU WOTE nchini, wanaofundisha shule za Serikali, wakiamua KUACHA KAZI, itakuwaje?
 
kazi kwelikweli!!!!!!!!!!!!!! inauma sna ila ifike wakati wa kujitambua coz mawazo ya wengi wetu ni kwamba ukienda chuo ukimaliza sasa unasubiri ajira tena serikalini!! Serikali ni mfanyabiasha kama wafanyabiashara wengi tu. watakutumia we ili ipate faida na si wewe kupata faida, ndio maana inanakupa kiwango cha chini cha kipato ili uendelee kuitumikia milele daima. Sasa ni wakati wa kujiajiri wenyewe ni heri ukaweka kibanda chako cha nyanya na utapata vijisenti ambapo faida yote inakuja kwako kuliko kutoa faida kwa mtu usiyemjua au kumfahamu.
 
Mmmh hapo ndio kila mtu atatia akili sasa
Asante sana kwa mchango wako huu. Inasikitisha kuona wanayotendewa walimu. Hivi, ikifika simu WALIMU WOTE nchini, wanaofundisha shule za Serikali, wakiamua KUACHA KAZI, itakuwaje?
 
Bed Ade,..from udsm,2liambia kua 2ngekua wakufunzi,inauma sana npo kwenye shule ya kata na baadh ye2 walimu ni wanafki cz mpaka muda huu wapo wamejikalisha kwenye mashule,nataman sana kujiunga na jesh la wananch cz hi field haithaminiwi...
 
uko sahihi kabisa mi nilijua naenda kuwa Mkufunzi TTC, wapi Mpwa niliishia hukooo ambako watoto wanapotezewa muda na serikali tu
Bed Ade,..from udsm,2liambia kua 2ngekua wakufunzi,inauma sana npo kwenye shule ya kata na baadh ye2 walimu ni wanafki cz mpaka muda huu wapo wamejikalisha kwenye mashule,nataman sana kujiunga na jesh la wananch cz hi field haithaminiwi...
 
Nami nipo kwenye hii field mwaka wa pili cha maana nilichofanya ni kununua kiwanja karibu na shule tu. Ila hii field ukifanya kazi kwa miaka 5 hakuna ulichopata ila ni wewe kupoteza kila siku km si hela ni upeo wako. Km kijana km elli ni kujipanga na maisha ni heri mie kuliko elli hayo mazingira si rafiki kabisa na ndio shule nyingi ndio zilivyo. Kupata za town eti mpaka kujuana ama rushwa. Hata nami nakimbia nazichanga nikapige jiwe la pili field tofauiti na si mwl. Wa science tena.
 
Inasikitisha sana maana sote tumefundishwa na walimu. Kuna rafiki yangu ni mwalimu na kutokana na kujishughulisha na tuition aliweza kujijengea nyumba nzuri tu ya kisasa. Mtaani kwake watu wana kila aina ya viulizo, mara ohooo haiwezekani mwalimu kujenga nyumba! Udaktari ni wito na daktari akijenga hamna shida! kweli ualimu ulilaaniwa.
 
Nina mpango wa kuanzisha chama huru cha Walimu, kisiwe na siasa yaani kifocus purely kwene ualimu tu ili niwasaidie na wengine huko waliko maana kuna baadhi yao ukiongea nao kama vile sijui unawapigia kele, yaaani wamekata tamaa kabisa, ukiwaambia hili linawezekana, ndio kwanza wanakushangaa!!!
Inasikitisha sana maana sote tumefundishwa na walimu. Kuna rafiki yangu ni mwalimu na kutokana na kujishughulisha na tuition aliweza kujijengea nyumba nzuri tu ya kisasa. Mtaani kwake watu wana kila aina ya viulizo, mara ohooo haiwezekani mwalimu kujenga nyumba! Udaktari ni wito na daktari akijenga hamna shida! kweli ualimu ulilaaniwa.
 
Jiwe la Pili ni muhimu ila pia Vision na Mission ni muhimu sana maana wakati tuna-graduate jiwe hilo la pili, nilishangaa kwenda Rufiji Utete ( usiombe kufika hujo) nikakutana na jamaa mmoja tulimaliza wote hilo jiwe la pili eti anafundisha CIVICS shule moja pale Utete huku yeye ni Biology!!! Sasa Bilogy na Civics wapi na wapi mmmhhh
Nami nipo kwenye hii field mwaka wa pili cha maana nilichofanya ni kununua kiwanja karibu na shule tu. Ila hii field ukifanya kazi kwa miaka 5 hakuna ulichopata ila ni wewe kupoteza kila siku km si hela ni upeo wako. Km kijana km elli ni kujipanga na maisha ni heri mie kuliko elli hayo mazingira si rafiki kabisa na ndio shule nyingi ndio zilivyo. Kupata za town eti mpaka kujuana ama rushwa. Hata nami nakimbia nazichanga nikapige jiwe la pili field tofauiti na si mwl. Wa science tena.
 
Jamani hii kazi ni ya kujitolea pia unasaidia wa Tz wenzako na unapata swawabu.Ukiacha kaz unaandaa taifa la wajinga,makahaba na vibaka ambao haohao watakukaba wewe au nduguyo ata kwetu TANGA kuna shida tele za elimu ndio mana vijana wanakuwa wanganga
 
Ni kweli kabisa lakini kwangu mimi niliona kuliko niendelee kuwadanganya watoto wale si afadhali nijiondoe tu nisiwe sehemu ya tatizo
Jamani hii kazi ni ya kujitolea pia unasaidia wa Tz wenzako na unapata swawabu.Ukiacha kaz unaandaa taifa la wajinga,makahaba na vibaka ambao haohao watakukaba wewe au nduguyo ata kwetu TANGA kuna shida tele za elimu ndio mana vijana wanakuwa wanganga
 
Wadau wanasema field ya ualimu usipo kimbia ndani ya miaka miwili au mitatu ujue wewe usha dumaa kimaisha.
 
Pole sana,mie pia "mwalimu" kitaaluma lakini si mwalimu kikazi, serikali iliniletea sanaa na mimi nikaifanyia usanii, ilikula kwao na bado inaendelea kula kwao, nilifanya maamuzi magumu miezi 8 iliyopita. Nawasikitikia waalimu wenzangu ,sijui kipi kinachowafanya wawe waoga wa kukabiliana na changamoto, nadhani wanaogopa kuachia tawi kabla ya kushika tawi, na kama hiyo ndio sababu basi hawawezi kuruka ng'o. Ukitaka kuruka sharti uagane na nyonga..
 
Ni kweli kabisa unachosema Mpwa

22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom