Jana usiku katika kipindi cha majadiliano Radio Kheri Sheikh Mohamed Issa aliwatahadharisha sana Waislamu kuwa waangalifu na makini na huu umoja na ushirikiano uliojitokeza hivi karibuni kati ya Chadema na Nccr na athari zake kwa Waislamu katika swala la uongozi wa Tanzinia kwa siku zijazo. Nilisubiri afafanue ni kwa vipi umoja kati ya vyama viwili vya upinzani uwe tishio kwa Waislamu badala ya kuwa tishio kwa chama tawala sikusikia ufafanuzi wowote. Wana JF au washirika wa Sheikh Mohamed Issa mnaweza kunisaidia kupata tafsiri ya kauli hii?