Elections 2010 ushindi wa tsunami wa Mramba. CCM watachukua hatua gani?

Hili la Mramba pia limetokea kwa Rostam, inawezekana wananchi wa sehemu husika wakawa sehemu ya mafao ya Ufisadi, maana unaweza kuwa fisadi Makini au Fisadi hovyo. sasa Rostam na Mramba wanaweza kuwa Mafisadi Makini, kwamba wanafisadi Mapato ya Watanzania lakini pia wanatumia sehemu ya pesa hizo hizo kuendeleza maeneo wanakotoka, kwa maana ya kujijenga zaidi kwa wapiga kura wao. just my opinion

Ndivyo hivyo ilivyo kaka Saharavoice:Kwani wao wanafisadi lakini ukienda katika majimbo yao utafikiri ni mako makuu ya wilaya!!!:A S-key:
 
watanzania tubadilike, mtu asipokuwa waziri hawezi fanya lolote jimboni zaidi ya kuwatetea tu watanzania kama alivyo fanya kimaro,

hillo ndilo jibu sahihi, asipoapata uwaziri atabaki tu kuwatetea, bila kwenda kuwanunulia mbege, na hatima yake atakosa ubunge kipindi kijacho!!
 
Sikonge,

..wasiwasi wangu ni kwamba kauli mbiu ya kampeni ya Slaa ni vita dhidi ya ufisadi na mafisadi.

..sasa hii kura ya maoni ya ccm inatuelekeza kwamba wananchi hawako interested na kuwaondoa mafisadi. they simply can not connect the dots kati ya ufisadi na uduni wa maisha yao.

..sisemi kwamba Chadema nao waukumbatie ufisadi, lakini ili kupata nafasi ya kuunda serikali na kuutokomeza ufisadi, labda Chadema wanapaswa kuifikiria upya kauli mbiu ya kampeni zao.

Mkuu JokaKuu,
Mie pia napata wasiwasi kama wako. Dk. Slaa inapaswa abadili kaulimbiu yake kwa kuongezea maneno yatakayowapa wananchi matumaini. Makamba ameshaanza kuiponda kaulimbiu hiyo kwa kusema Dk. Slaa hana jipya. Kwa hiyo ni dhahiri wapo watakaoona kwamba kuimba ufisadi ni wimbo ulizoeleka.

Bado nasisitiza kwamba Dk. Slaa anapozungumzia ufisadi akazane kueleze jinsi ambavyo una mahusiano makubwa/unasababisha/unazidisha umaskini na maendeleo duni ya wananchi walio wengi vijijini na mijini pamoja wafanyakazi wa ngazi za chini ambao JK alizikataa kura zao kwa jeuri.
 
The best way to deal na hizi issue za ufisadi nadhani ni kama mkapa alivyosema "Leta ushahidi" evidence! Kama hamna evidence huyu mtu bado ni safi...that is what we have chosen to live.

Kwa hivyo, mimi sioni shida ya mraba as mbunge wa rombo, kama aliweza ku-deliver what he promised his voters kwanini wasimpe kura, sioni shida. If at all akiwa kama waziri amefanya madudu then that is a national issue and be delt at the national level as for jimbo level hana ufisadi and infact he is very realistic when it comes to the district level as amekuwa akileta alichoahidi na anawajua warombo vizuri kwani at one time aliahidi hakuleta wakamwondoa mara moja. So for me go mramba....
 
Prodigal Son,

Hapo umenena. Ukweli mwananchi wa kawaida hasa mkulima aliyoko kijiji nachotoka mimi si rahisi kujua athari au ubaya wa ufisadi na kwamba neno ufisadi hajui maana yake. Elimu ya kuwahamasisha inatakiwa ili wajue ufisadi ndo unaowafanya wabaki masikini wa kutupwa awe CCM, CUF ama CHADEMA.

Ukiangalia upinzani mkubwa uko kwenye miji ambako watu wameshajua madhara ya ufisadi, vijijini hawajui na kwamba wanajua chama ni CCM tu. Hawajui kama kuna CHADEMA wapo, Kijijini kwetu wanakwambia wanasikia kuna mtu anaitwa SILAHA (DR. SLAA) anatembelea ndege lakini hajui atawasaidiaje wao wanajua CCM ndo imewalea na ndo wanaijua.

Na huko ndo UCHAKACHUAJI WA KURA unafanyika.

Wengi wetu tunashabikia siasa na hasa upinzani lakini hatuendi kupiga kura. Wana-CCM karibia asilimia 95 wanapiga kura. ushahidi kura za maoni 2010.

..huyu ni fisadi lakini wana ccm rombo "hawaoni", wala "hawasikii."

..na hili inaelekea kama vile ni tatizo la nchi nzima. hata wale mafisadi walioshindwa ktk mahimbo mengine inaelekea wameshindwa kwasababu tofauti na ufisadi wao.
.
..nategemea kura hizi za maoni za CCM zitatoa mwangaza kuhusu future ya vita vya ufisadi.

..
Joka kuu pole sana kwa kutojua unachokiona/sikia,hata Mh.Cisco Mtiro alishasema msinipime kwa hereni sikioni mwangu,bali kilichopo kichwani pangu,mramba ameshawafanyia mengi mema na ya msingi jimboni mwake,huwezi jua labda huo ufisadi alikuwa anafanya kwa manufaa ya jimbo lake,watu kama hao huwezi kuwashauri lolote juu ya ubaya wa mtu huyo,coz kwao ni mzuri na mleta mazuri,swala hilo ni kama lile la Lowasa,yaani kwake anakubalika kuliko maelezo!!
 
Wananchi waliowapitisha Lowassa, Chenge, Mramba, Rostam ni kwamba wao ni maskini wa mawazo, hivyo kuchambua pumba na mchele hawana uwezo, wanafurahia kwenda kula na kunywa kwa mafisadi. wao wanawashangaa watanzania wengine wanaowaita wabunge wao mafisadi, pia wanafikiri mtu kuwa fisadi ni sifa kama nyerere.
Sitegemei kama NEC ya CCM itakata majina ya hao mfisadi nguli maana watakuwa na hofu ya kususiwa na wapiga kura wa hayo majimbo

mwisho dr slaa anakuzwa na watu na nyombo vya habari, lakini ukweli hana ubavu wa kupata hata kula milioni mbili, na pia dr slaa hakubaliki kama ilivyokuwa A. L mrema mwaka 1995 ambapo alishindwa vibaya na Mkapa
 
Ngoja niwape ishu ya Rombo... Ukweli ni kuwa tofauti na sehemu zingine Rombo imetengwa sana kutoka Tanzania. Kwa taarifa yenu ni kuwa Rombo hakusikiki redio yeyote ya Tanzania kirahisi ukiacha sauti ya injili (moshi). Zaidi ya 90% ya watu kule husikiliza Redio citizen na KBC za Kenya. Miaka michache iliyopita walikuwa wanapata redio one na redio free, lakini siku chache baada ya kuanza kuibuka kwa ishu za ufisadi na Mramba kutajwa, redio free na redio one zikapotea hewani (ukiacha maeneo machache ya Mkuu na Mengwe). Magazeti nayo siku hizi hayauzwi, ukiacha tu sehemu moja pale stendi ya wilayani...

Nimejaribu mara kadhaa ninapokuwa kule kudadisi kwa mfano kwa kiasi gani watu wanafaham kuhusu ufisadi... sana sana watu wahafaham fisadi Kamresh Patney (wa Kenya), na asilimia kubwa neno Rostam, Lowassa, Chenge, Karamagi na wengine kwao ni viongozi wa serikali, ni wachache, tena vijana (ambao hawapigi kura) wanaojua ni kwa nini Lowassa alijiuzulu!!!

Warombo wanaamini kuwa bado wao ni mojawapo ya sehemu zilizoendelea sana Tanzania, na hivyo wamependelewa na serikali, ukiwaambia kumpinga Mramba, hasa baada ya kuwawekea lami, ni jambo zito. Matajiri wote Rombo ni wafuasi wa CCM na mashabiki wa Mramba, ukianzia akina Maulidi Swai, Luka Mchomba, Michael Shirima (mwenye Precision air), Waha, Kanyau, John Marceli, Faida, Oisso, Lasway, Teotim 'mhindi', na wengine kwa mamia. Hii inafanya watu kuhushisha u-CCM na utajiri, hivyo inakuwa ngumu kumwelewesha mtu uhusiano kati ya CCM na umaskini wake. Kila mtu anataka awe tajiri bwana.

Angalau katika siku za karibuni kumekuwa na mwamko kidogo kutokana na watu wengi wanaotoka mijini hasa vijana kusapoti CHADEMA. Ingawa CHADEMA ilikuwa na nguvu kule lakini kitendo cha mbunge wa zamani kwa tiketi ya CHADEMA, Salakana kuhamia CCM hadharani pale Tarakea, na baada ya hapo biashara zake za kampuni ya utalii kuanza tena kufanya vizuri (zilikuwa zimedorora), kwa kiasi kikubwa kiliiua sana CHADEMA Rombo.

Nimepata habari kuwa mwaka huu CHADEMA wameweka mgombea machachari (sijamfahamu ni nani...). Binafsi namtakia kila la heri lakini namtahadharisha ajipange vizuri sana kupambana na wizi wa kura wa Mramba. Yule jamaa anatumia sana nguvu za matajiri wa kule kufanikisha kuchomekewa kwa masanduku bandia ya kura, na wakati fulani (2000), walitumia hata bastola kuescot na kutishia wale wote waliokuwa wanaleta chokochoko. Kwa maana niyo CHADEMA wanapaswa wajipange vizuri pale na wakifanya hivyo watashinda...
 
Hicho usemacho ni kweli kwani hawa jamaa wa Rombo wakati ule huyo mbunge wao aliposema hata watz wakila majani lazima ndege ya rais inunuliwe nilidhani uchanguzi uliofata wasingempa lakini wapi. Lakini pia mimi nadhani watu wa kule wako nyuma ofcourse inawezekan kuna matajiri wachache hivyo wakipewa vitu vidogo vidogo wanadanganyika. Inabidi kuweka kambi sehemu kama hizo kuhakikisha watu wanaelewa somo. Lakini unaweza kuwekwa mkakati na hawa CHADEMA ile operation sangara ilitakiwa ipite kule kuraise awaireness. Kale kazee kana dharau sana.
 
Ngoja niwape ishu ya Rombo... Ukweli ni kuwa tofauti na sehemu zingine Rombo imetengwa sana kutoka Tanzania. Kwa taarifa yenu ni kuwa Rombo hakusikiki redio yeyote ya Tanzania kirahisi ukiacha sauti ya injili (moshi). Zaidi ya 90% ya watu kule husikiliza Redio citizen na KBC za Kenya. Miaka michache iliyopita walikuwa wanapata redio one na redio free, lakini siku chache baada ya kuanza kuibuka kwa ishu za ufisadi na Mramba kutajwa, redio free na redio one zikapotea hewani (ukiacha maeneo machache ya Mkuu na Mengwe). Magazeti nayo siku hizi hayauzwi, ukiacha tu sehemu moja pale stendi ya wilayani...

Nimejaribu mara kadhaa ninapokuwa kule kudadisi kwa mfano kwa kiasi gani watu wanafaham kuhusu ufisadi... sana sana watu wahafaham fisadi Kamresh Patney (wa Kenya), na asilimia kubwa neno Rostam, Lowassa, Chenge, Karamagi na wengine kwao ni viongozi wa serikali, ni wachache, tena vijana (ambao hawapigi kura) wanaojua ni kwa nini Lowassa alijiuzulu!!!

Warombo wanaamini kuwa bado wao ni mojawapo ya sehemu zilizoendelea sana Tanzania, na hivyo wamependelewa na serikali, ukiwaambia kumpinga Mramba, hasa baada ya kuwawekea lami, ni jambo zito. Matajiri wote Rombo ni wafuasi wa CCM na mashabiki wa Mramba, ukianzia akina Maulidi Swai, Luka Mchomba, Michael Shirima (mwenye Precision air), Waha, Kanyau, John Marceli, Faida, Oisso, Lasway, Teotim 'mhindi', na wengine kwa mamia. Hii inafanya watu kuhushisha u-CCM na utajiri, hivyo inakuwa ngumu kumwelewesha mtu uhusiano kati ya CCM na umaskini wake. Kila mtu anataka awe tajiri bwana.

Angalau katika siku za karibuni kumekuwa na mwamko kidogo kutokana na watu wengi wanaotoka mijini hasa vijana kusapoti CHADEMA. Ingawa CHADEMA ilikuwa na nguvu kule lakini kitendo cha mbunge wa zamani kwa tiketi ya CHADEMA, Salakana kuhamia CCM hadharani pale Tarakea, na baada ya hapo biashara zake za kampuni ya utalii kuanza tena kufanya vizuri (zilikuwa zimedorora), kwa kiasi kikubwa kiliiua sana CHADEMA Rombo.

Nimepata habari kuwa mwaka huu CHADEMA wameweka mgombea machachari (sijamfahamu ni nani...). Binafsi namtakia kila la heri lakini namtahadharisha ajipange vizuri sana kupambana na wizi wa kura wa Mramba. Yule jamaa anatumia sana nguvu za matajiri wa kule kufanikisha kuchomekewa kwa masanduku bandia ya kura, na wakati fulani (2000), walitumia hata bastola kuescot na kutishia wale wote waliokuwa wanaleta chokochoko. Kwa maana niyo CHADEMA wanapaswa wajipange vizuri pale na wakifanya hivyo watashinda...
Rombo sasa hamna wazee wale wenye maadili waliomuondoa Mramba Ubunge 1995 na 2000 alipoiba kura (japokuwa kesi ilisuluhishwa nje ya mahakama na cha ajabu shinikizo la Wachagga wengine kwa Salakana lilisababisha afute kesi ya wizi wa kura wa Mramba 2000 (how stupid and undemocratic was that?) kisa eti ahadi za CCM + Mkapa kumpa Mramba uwaziri wakauwa Demokrasia) wote wamefariki! wamebaki wazee mafisadi kama ulivyosema wakina Shirima, Mchomba, Ernest Massawe na wengineo! naskia huyo Luca alitishia bunduki mgombea aliyeshindwa akaripotiwa TAKURURU! Enzi ya kina Kisinani na Maskini haipo tena yamebaki wazee Manyang'au! Na kutengeka kwa Rombo kimawasiliano ni kutokana na geographical location ya huko wako the Eastern side of Mt Kilimanjaro so frequency ni shida yaani wako out of media coverage! huko kukamata TV lazma uwe na buster kali!
 
Back
Top Bottom