Ushindi wa CDM Arumeru CUF wapate funzo gani?

Yasser5

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
207
17
Kama kawaida wana JF pipoooooooooo ..............

Swali langu ni fupi kwa waheshimiwa wa CUF

ushindi wa CDM arumewru CUF wanajifunza nini?

Itfaki imezingatiwa naomba kuwasilisha
 
Watu 60 wameiangalia hii, wakasepa. Kunani?
Na mimi niliiangia nikatoka, lakini nimerejea kwa sababu nadhani inahitaji angalizo.
Mada yako - Ushindi wa CDM Arumeru CUF wapate funzo gani? - Mimi nahisi kama kuna funzo lolote kwa ushindi wa CDM Arumeru, funzo hilo kama hakuna budi basi liwe kwa CCM (hao CUF uliowataja hapa hata hawakushiriki uchaguzi), lakini hasa, funzo hilo ni kwa vyama vyote na Watanzania wote.

Kama Mtanzania niliyekuwa ninafuatilia mchakato wa Arumeri, nimejifunza mengi kutoka pande zote lakini mambo mawili yameganda akilini mwangu. 1. Ni rahisi kuwadanganya watu wote siku moja na sio siku zote. CCM imekuwa ikiwadanganya Watanzania wote siku zote, imefika pahali Watanzania wameanza kupaza sauti zao - kwa njia ya amani - ndani ya visanduku. Kuna siku ikiwa visanduku vitaendelea kuchakachuliwa, hawatapaza sauti bali wataonesha hasira mitaani. Mungu ajalie yasitufike hayo.

2. Takriban viongozi wote wa CCM (na baadhi ya vyama vyengine), walifikiri kuwapa wananchi kile wanachotaka - kusikiliza umbeya na matusi - nani katoga sikio, nani anakanyagwa, nani si mtoto wa nani, uongo wa jogoo, wenye mimba...Watu wanataka kuyasikia hayo kwani umbeya mtamu, lakini watu hawahitaji hayo, wanahitaji maendeleo. Hayo maneno ya udaku, matusi na umbeya watayapata vibarazani au hata kwenye vyombo vya habari visivyo na maadili, lakini MAENDELEO HAWATAYAPATA KUPITIA MATUSI, UBABE NA UMBEYA.

Kwa ufupi, ushindi wa Arumeru unapaswa kuwa kigezo kwa Watanzania na hasa kwa wanasiasa, kuwapa kile Watanzania wanahitaji.
 
Kwanza, Ushindi wa Arumeru hauna mahusiano na utoaji wa elimu wala mafunzo achilia mbali CUF bali kwa CCM na subsidiaries zake zote za kisiasa wala kwa mwanasiasa au kambi yoyote ile ya kisiasa bali ni sauti kubwa kwamba wananchi hawaitaki CCM.

Pili, huu sio muda wa kutafakari mambo katika mtazamo huu, huu ni Muda wa kushangilia ushindi mpaka sikukuu za pasaka ziishe, acheni kupenda maisha ya shida kila wakati, take your time and celebrate with CHADEMA it can add you a minute of life. Shangilia ushindi Arumeru
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom