USHINDI WA ARUMERU - M.M.Mwanakijiji alijuaje?

mpingauonevu

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
623
430
Alianza kama utani. Arumeru CDM ikishindwa viongozi wote wajiuzulu. Nikambishia kwamba CDM haitashinda, Kwa akili yangu nilijiuliza kura 19,000 zitanyan'ganywaje kutoka ccm? akasisitiza, mimi sikumuelewa.

Hatimaye CDM imeshinda na hakuna kiongozi atakayejiuzulu.
M.M.M aliona nini? alijuaje kwamba ni lazima CDM ishinde? alikuwa na uhakika gani mpaka akatoa msisitizo mkubwa hivyo?

M.M. Mwanakijiji nakukubali.

Kwa nini tusikuweke Ikulu utusaidie kuona mbali?
 
Ukiondoa Mtwara, Lindi na Tabora, mahali kwingine kokote ukifanywa uchaguzi wa marudio na chadema wakadhibiti mianya ya wizi wa kura, basi kushindwa ccm haihitaji mtabiri. MMKJ aliliona hilo mapema.
 
Basi tunaweza kabisa kuepuka gharama kubwa ya chaguzi kwa kumtumia Mkjj, iwapo utabiri na muono wake ni 89% accurate... 11% ya anapokosea isitufanye tulazimike kuingia kwenye uhasama baina yetu kwa kutukanana na kurushiana matusi ya nguoni kwa gharama kubwa majukwaani wakati tunaweza kutumia utabiri wake na kuteua viongozi wetu!!!
 
Mtu yeyote aliyewahi kucheza mchezo wa "Hiki na hoko"... anaweza kuchagua tu kwa usahihi kati ya vitu viwili. Wanasema penye pande mbili za kuchagua uwezekano wa upande mmoja kutokea ni fifty percent!
 
Nampongeza MMM kwani mbinu ile aliyoitumia ni ya hali ya juu sana .Amini usiamini habari zile alizorusha humu MMM zilisambaa nje ya JF kwa kasi ya ajabu .

Hizi ni mbinu mbadala za kuwapa watu hamasa hususani kuweza kushinda mbinu chafu za CCM.Aliwajenga watu kisaikolojia kuwa tumeshinda msikubali kunyang'anywa ushindi hatua za mwisho.Hii mbinu ilitumika Moshi mwaka 2000 wakati Ndesa Pesa aliposhinda kwa mara ya kwanza.

Vyombo vya usalama huwa vikishapata habari kuwa matokeo halisi yashavuja ,mara nyingi wanajihami kujiingiza kwenye uchakachuzi kuepuka machafuko.Ila kama wakigundua bado watu hawan taarifa huwa wanasimamia shughuli ya uchakachuzi wenyewe.
Hongera sana MMM.
 
Mwanakijiji, alikuwa anaangalia upepo unavyovuma kwenye uchaguzi wa Arumeru! watu wengi mbona walijua mapema tu kuwa Chadema wameshinda baada ya kufanya majumuisho ya kila kituo hakuna cha ajabu alichokifanya Mwanakijiji, alitumiwa matokeo na Chadema akaanzisha thread humu JF.
 
lakin mwenyewe HAJASEMA hayo usemayo!
 
lakin mwenyewe HAJASEMA hayo usemayo!

Mkuu, jiulize mwenyewe na tumia akili yako Mwanakijiji, aliyapataje matokeo ya Arumeru Mashariki na idadi ya kura wakati hayupo Tanzania!
Mie nakuambia hivyo sababu matokeo aliyotumiwa Mwanakijiji, walitumiwa watu wengi.
 
Hakika M.M. Mwanakijiji ni mtu wa M4c, anauchukia ufisadi na mafisadi na anaipenda Tanzania na Watanzania wote. Big up kwake.
 
mwana k, tuambie Kama malecela w. Atashinda a,mashariki. Makongoro?
 
Mmkj hakuguess bali inaonesha ana mawasiliano ya karibu na watu waliokuwa jikoni, guess gani ile hadi tofauti ya kura,
hongera mkuu kwa kazi nzuri!
 
Mwanakijiji, alikuwa anaangalia upepo unavyovuma kwenye uchaguzi wa Arumeru! watu wengi mbona walijua mapema tu kuwa Chadema wameshinda baada ya kufanya majumuisho ya kila kituo hakuna cha ajabu alichokifanya Mwanakijiji, alitumiwa matokeo na Chadema akaanzisha thread humu JF.

Umerudi tena?'wenzio wako wapi mbona wote mlitoweka ghafla??
 
Mwanakijiji, alikuwa anaangalia upepo unavyovuma kwenye uchaguzi wa Arumeru! watu wengi mbona walijua mapema tu kuwa Chadema wameshinda baada ya kufanya majumuisho ya kila kituo hakuna cha ajabu alichokifanya Mwanakijiji, alitumiwa matokeo na Chadema akaanzisha thread humu JF.

ritz1 karibu tena, siku ya kutangaza matokeo wewe na rejao mlijificha kabisa. poleni sana, watanzania hawatawaamini tena.......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom