Ushetu Kahama hali bado tete

majukumu kitambi

New Member
May 6, 2015
2
0
Ikiwa ni takribani muda wa juma moja tu tangu kutolewa tuhuma dhidi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu kwa Matumizi mabaya ya ofisi, kuwapandisha vyeo watumishi wasio na sifa, kuendesha Halmashauri kwa ubabe na upendeleo kwa baadhi ya watumishi kimaslahi.

Leo wananchi wa kata ya Bulungwa wiyani hapa wameibuka na kutoa shutuma dhidi ya kile walichodai ni ubadhilifu na matumizi mabaya ya Michango ya Wananchi iliyochangwa kwa lengo la ukarabati wa kituo cha afya cha Bulungwa ikiwa ni pamoja na fedha zaidi ya Tshs 40.000,000= zilizotolewa kama ruzuku ya fedha za maendeleo iliyokusudiwa kuboresha majengo katika Kituo hicho cha afya lakini shuguli hiyo haikufanyika kama ilivyokusudiwa.

Tuhuma hizo zimetolewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mseki kata ya Bulungwa ambao ulihutubiwa na Mbunge wa jimbo la kahama, James Lembeli.

Hata hivyo inasadikiwa kwamba tuhuma hizo pia ni mlolongo wa kashfa zinazomkabili Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu ambazo ni bomu linalosubiri kulipuka. Mkurugenzi huyu anatuhumiwa pia Kufuja na kubadilisha matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya afya, maji na barabara.

Katika tuhuma zinazohusiana na kupendelea baadhi ya watumishi pia anatuhumiwa kumpa kibali na kumruhusu kwenda masomoni mwanasheria judy aliyekuwa amemkaimisha kuwa afisa utumishi baada ya kaimu afisa Utumishi kusimamishwa kazi licha ya Mtumishi huyo kutokuwepo kwenye bajeti huku watumishi wengine wakinyimwa haki kwa lugha ya ukosefu wa fedha.

Hata hivyo wananchi wa kahama- Ushetu wanaamini kwamba hatimaye vyombo husika vitachukua hatua na kutenda haki.
 
Back
Top Bottom