Ushauri: Wiki imeisha hataki kuongea na mimi

Mkuu usioe kwanza inaonekana akili yako bado haijakua kiasi cha kuweza kuhimili mikiki ya ndoa

pixel
Hili tu limekuchanganya kaka ndoa kweli utaiweza ndoa ina mikiki inatakiwa uwe tayari kwa changamoto huwa wanasema ndoa ni full of changamoto,Muache tu mpaka atakapoamua kukutafuta na ajieleze mwenyewe usimuulize ukaanza kulia lia atakutesa huyo kuwa mkakamavu
 
Nina mpenzi wangu ni mwaka sasa tuko kwenye uhusiano na tumepanga kuoana mwakani. Yeye yupo Morogoro mimi nipo Dar. Sasa cha kushangaza wiki moja imeisha kaniblock namba yangu hataki kabisa kuongea na mimi hata nikimtumia meseji kumuuliza kama ameniacha hajibu yupo kimya, nikimuuliza dada yake (hawaishi naye) ananiambia labda kuna vitu vimemtinga eti nimuache tu akikaa vizuri atanitafuta mwenyewe.

Sasa hii inanichanganya sana, naombeni ushauri.

Poleeeee
 
Dah,kwa kweli haya mambo yapo kushare experience niliwai kukutana na kisanga cha aina hiko nilijitoa kweli kumuhudumia kwani niliamini kabsaaa nachukua jiko lakini akakutana na jinamizi lililoshindikana akampa ushauri wa kunitikisia kibiriti akawa jeuri kweli kila unalosema kwake baya na vikwazo kibao nikasoma alama za nyakati nikajitoa kimya kimya baada ya miezi mingi kupita anatuma watu kuwa yupo tayari kuolewa nipeleke barua eti....mh,
 
Atskua kama huyo maana Mara nyingi nilikua nsmuambia nipeleke barua anasema nisubiri nisiwe n hataka cha kushangaza kakata mawadiliano na hataki kuongea chochote.
 
Ukiingia kwenye ndoa na mtu kama huyo utajuta! na utaamini wote walio oa wanaishi kwa tabu kama wewe.

Kumbe kuna watu wana enjoy ndoa zao balaa!!

Tafuta akupendae, hakika utaipenda ndoa yako!
 
Hivi unatuuliza seriously tukushauri au unatusimulia tushee majonzi yako?

Hebu kuweni serious jamani saa ingine na headings

Kwanza sisi sio rafiki zako, ungewauliza rafiki zako huko Ilboru sijui Tosamaganga labda mngeshauriana vizuri
haha
 
Nina mpenzi wangu ni mwaka sasa tuko kwenye uhusiano na tumepanga kuoana mwakani. Yeye yupo Morogoro mimi nipo Dar. Sasa cha kushangaza wiki moja imeisha kaniblock namba yangu hataki kabisa kuongea na mimi hata nikimtumia meseji kumuuliza kama ameniacha hajibu yupo kimya, nikimuuliza dada yake (hawaishi naye) ananiambia labda kuna vitu vimemtinga eti nimuache tu akikaa vizuri atanitafuta mwenyewe.

Sasa hii inanichanganya sana, naombeni ushauri.
Sasa hivi kwangu mapenzi ya mbali hayana nafasi kwangu, nimeshajuta mkuu tafuta mwingine hao viumbe hawafai na si wakuamini, ni vingonga hao wanabadilika kutokana na mazingira
 
Kweli aisee maana imekua ghafla sana na wala hatujagombana
 
Me mwenyewe ishu yangu ipo ivo ivo we c wakwanza najua inauma sana, mpotezee hujazaliwa nae huyo, mmejuana ukubwani tuu.
 
Back
Top Bottom