Ushauri wenu wana JF!

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,672
Habari zenu wana Jamvi, yuko dada mmoja ambaye ni jirani yangu kaniomba ushauri ambao binafsi nimeshindwa kumshauri. Hivyo naomba mawazo yenu. Ni kitu ambacho kidogo kimenishangaza. ni dada mwenye watoto wawili kwa maelezo yake ni kuwa mumewe alimpa karipio kali kuwa hataki mtoto tena, anasema kwa bahati mbaya siku za hivi karibuni alizembea kutumia vidonge vya uzazi, sasa imeshaingia.

Anachonieleza ni kuwa kwa jinsi anavyomjua mumewe anaogopa kumwambia kwani anaweza kujikuta akipata talaka kwa kosa hilo tu! Pia swala la kutoa anaogopa kwani anahisi iwapo yatatokea matatizo atazusha tatizo kubwa zaidi! Je afanye nini kujinasua na tatizo hilo?
 
Hiyo mimba ni ya mumewe au ni ya mtu mwingine? Laba tuanzie hapo kwanza
 
hakuna shortcut hapo..., amueleze mumewe kwamba alizembea dawa so kapata ujauzito..

Hicho kiumbe ni cha wote wawili na inabidi kushirikina, kama huyo mumewe hawezi kuelewa hilo, then maybe alifanya makosa kuolewa nae. Na kama ni Talaka atapewa huenda ikawa blessing kuondokana na mtu ambaye sio considerate
 
Hiyo ipo kwenye jamii, aende kwa wakweze awaeleze wao ndiyo waje kumhabarisha na amwambie ukweli kwamba aliogopa kusema kwake ndiyo maana akawashirikisha wazazi wake. Simple kama ni talaka basi itoke tu. Kutoa mimba asijaribu, hawezi jua anaamzaa nani? who knows! Mungu amtie nguvu.
 
hayo ndiyo matatizo ya wanawake kuwategemea wanaume hasa kiuchumi,amwambie ukweli na afanye atakalo,nafikiri kuna haja ya wanawake kujiamini kimaisha na kujifunza kujitegemea
 
Assumption: Hiyo mimba ni kweli ya huyo bwana. hivyo basi,

Mwambie huyo mama namuamini kumwambia mume wake habari hiyo kama alivyokuamini wewe hadi akakwambia masuala nyeti ya ndani. Inabidi ajiamini kwa mumewe, asijidhlilishe kwa kuogopa talaka.

Ni nani katika dunia hii ataamini ya kuwa bwana kampa talaka mke kwa sababu amepata ujauzito ambao yeye bwana ni chanzo. Kama talaka ilikuwepo basi ipo either kuna ujauzo au hapana. Mfundishe huyo mama kuwa ana haki sawa na mumewe kwenye nyumba labda kama anayesikiliza hadithi ni chizi..
 
hakuna shortcut hapo..., amueleze mumewe kwamba alizembea dawa so kapata ujauzito..

Hicho kiumbe ni cha wote wawili na inabidi kushirikina, kama huyo mumewe hawezi kuelewa hilo, then maybe alifanya makosa kuolewa nae. Na kama ni Talaka atapewa huenda ikawa blessing kuondokana na mtu ambaye sio considerate

Mkuu haina haja hata ya kusema kazembea, hivi kwani kuna guarantee ya 100% kwamba ukitumia hayo madawa haupati ujauzito?
Halaf hii ya mwanaume kutoa talaka sababu ya mimba yake mwenyewe,hii ni new release aisee. Khaaaa!
 
Don't worry Gazeti, mwambie asiogope. Siku zote tunapoweka limit ya watoto, huwa kuna balance ya mtoto mmoja. Namaanisha kuwa, mtu akisema anataka kuwa na watoto wawili tu, huwa ni watoto 2 + 1. Kwa hiyo baada ya hapo wanandoa wanaweza kuamua kufunga kizazi ili waendelee na malezi ya watoto wao.
 
kama huyo m.me alikuwa hataki mtoto kwanini na yeye asizuie?sio kila kitu ni kazi ya m.ke.kama raha ya mchezo wanaipata wote,na yeye angekuwa makini vile vile
 
amwambie ukweli huyo mume wake. Asijaribu kutoa hyo mimba, atakuwa anajiongezea matatzo! Afu huyo mume nae si angeshiriki kuzuia mimba isipatikane??
 
Hiyo ipo kwenye jamii, aende kwa wakweze awaeleze wao ndiyo waje kumhabarisha na amwambie ukweli kwamba aliogopa kusema kwake ndiyo maana akawashirikisha wazazi wake. Simple kama ni talaka basi itoke tu. Kutoa mimba asijaribu, hawezi jua anaamzaa nani? who knows! Mungu amtie nguvu.
Hivi hili nalo ni la kupeleka kwa wakwe kweli? Naona linaweza kutatuliwa na wanandoa wenyewe tu.
 
wanawake,wanawake,wanawake lini tutasema hapana kwa unyanyasaji wa namna hii....kwani jukumu la uzazi ni la mama peke yake na huyo mbaba anaekojoa hovyo kama kuku...msonyoooo!
 
wanawake,wanawake,wanawake lini tutasema hapana kwa unyanyasaji wa namna hii....kwani jukumu la uzazi ni la mama peke yake na huyo mbaba anaekojoa hovyo kama kuku...msonyoooo!

kwani kukojoa ni kosa???????
 
Back
Top Bottom