Ushauri wenu tafadhali

Natal Vice

Member
Dec 8, 2013
16
8
Habar zenu wana Jamii Forums.

Mimi ni mgeni humu ila nimeona niingie humu kwa kupata ushauri zaidi,ni miaka miwili tangu nimeolewa na nashukuru Mungu ninaishi vizuri na mume wangu na pia Mungu katujalia tumepata mtoto mmoja na pia kwa sasa nina ujauzito.

Tatizo langu kubwa ni kwa huyu mume wangu kila naposhika mimba hasa mimba inapofikia umri wa miezi mitatu, mume wangu hapendi kabisa kukutana kimwili na mimi,mwanzoni nilivyokuwa mjamzito i mean kwa mtoto wangu wa kwanza.

Nayo ilikuwa hivyo hivyo,nikawa najitahidi kujiweka fresh zaidi lakini hali ni vile vile na sasa hivi napo naona hali ni vilevile,nisipokuwa mjamzito kwa kweli tunashiriki vizuru tendo la ndoa lakinu nikiwa mjazito hali inakuwa hivi.

Naombeni ushauri wenu tafadhali.
 
Angejua wajawazito walivyo watamuuuu... Nicheck pm kuambie kitu
 
usijali bibie nicheki pm hajui kuwa ya mjamzito ni tamuu
 
Haya uliyoyaandika hapa umeongea na mumeo kujua mawazo yake?
 
Itakuwa mmeo ndo mwathirika wa maluwe luwe ya mimba, usishangae na kisirani akawa nacho yeye plus kichefuchefu...no way muache tu mtu halazmishwi kufanya mapenzi siku akiwa tayari mtafanya!!!ila anajiwekea mazingira mazuri ya kupigiwa huyo....
 
Anakosa Joto moja ka Abuja sana. Maana uvungu wote wa moto kipindi hicho
 
Nimeongea nae sana kuhus hili,huwa ananijibu kuwa atalifanyia kazi

Basi mpe muda...

Najua unapata tabu kidogo kwa kuwa ashki ya mwanamke mjamzito kidogo ipo juu...

Pengine mumeo ni muoga haswa aonapo kitumbo kimejitokeza ni jukumu lako kumuonesha hakuna shida katika hilo...
 
Pole sana shosti, umesema unamtoto mmoja ndoa yenu ina miaka miwili na una mimba nyengine? nadhani mpaka sasa utakua umeshamjua ni mume wa aina gani jee umemuliza labda kuna chochote anachojisikia? manake mie nikiwa na Mimba nakua mzima kama vile sina,lakini mumewangu kutapika yeye maembe mabichi yeye ndimu yeye kuchoka yeye ila kwenye tendo la ndoa humwambii tena ikiwezekana anaitaka kila siku..........
 
nendeni kwa doctor wote wawili, atapewa ushauri kwa sababu kuna watu wana imani kwamba mke akiwa na ujauzito haingiliwi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom