Ushauri wenu kabla sijajiingiza kwenye bidhaa za Oriflame

kambagasa

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
2,241
1,748
Wakubwa habari zenu, wadogo marahaba.

Ndugu zangu jana nilitumiwa message na rafiki yangu akiomba aniunganishe katika biashara ya bidhaa za Oriflame Sweden (kama alivyoziita yeye). Kwa kuwa ni rafiki yangu nilimuuliza endapo zina tija na kama ni inshu serious. Baadae niliunganishwa na kutumiwa taarifa mbalimbali ambazo kwa kweli zilinivutia sana.

Kuna kipindi nilisoma uzi humu unahusu bidhaa za forever living ambapo nilipata elimu kubwa kuhusu bidhaa za forever na nikaamua kukaa pembeni. Hivyo naamini hapa Jamii forum kuna watu waelewa sana na huenda wana ufahamu zaidi na hizi bidhaa za Oriflame.

Karibuni sana wana wa Mungu ili nifahamu kabla sijajiingiza huko.
 
Wamejikita sana kwenye vipodozi na urembo. Mimi hapa member Oriflame pia na Trevo. Tatizo WanaJF nyinyi ni wagumu sana kufanya maamuzi. Kinatomaso sana nyinyi. Nimewatangazia humu ndani Trevo mkaishia kunitukana. Hamtaki kuielewa kiufasaha. Wengine humu ndani kazi hamna. Tunaleta Neema kwa wote mnakandafua. Sasa kwa taarifa sisi tunaendelea, mtakapozinduka ndipo utasema kwanini sikukata shauri tangu mwanzo saa hizi ningekuwa mbali. Uoga wako kuamua jambo ndio umaskini wako.
 
Umenigusa sana japo nimeuliza hapa kwa nia zuri. Mfano nimeandaa order na kutuma pesa je nikipigwa kimya inakuwaje?
 
Ukitaka mali utayapata shambanii....Huo uchuuzi ni survival tu ule uvae lakini hauna sustainability...Nitajie tajiri yeyote ambaye yupo kwenye hizo makitu? Wengi ni low income na middle class ndo ambao hamuelewi concept ya utajiri ipoje. If you want to be rich just understand how capitalism works..
 
Hii ni sawa na MATAIRI ya gari, kazi kubwa na kupeleka body ya gari na waliokaa humo wafike wanapotaka. Tairi zitakabiliana na jua, mvua, miba, na kila aina ya vikazwo. Mwisho wa safari zimechakaa, zimepata moto, zimelika, yaani ziko taabani. Tafakari chukua hatua with this puzzle
 
Umenigusa sana japo nimeuliza hapa kwa nia zuri. Mfano nimeandaa order na kutuma pesa je nikipigwa kimya inakuwaje?
Utakapokuwa member ni lazima uifahamu ofisi yako (maanaake hiyo ndio ofisi yako). Kama unataka kuwa mtumiaji wa bidhaa tu sio member nikwamba utafanya order kupitia aliyekufahamisha biashara. Hawezi kukupiga kimya ni illegal kwenye hizi biashara.
 
Nilitumiwa pia namba ya siri kwa ajili ya order kama mwanachama lkn naona nitakapo andaa order naona ni vizuri niende mwenyewe kuchukua bidhaa
 
Nilitumiwa pia namba ya siri kwa ajili ya order kama mwanachama lkn naona nitakapo andaa order naona ni vizuri niende mwenyewe kuchukua bidhaa
Kumbe ulishajiunga na mpaka namba ya siri ya uwakala unayo(ina maana hadi kiingilio ushalipa) we sasa unataka ushauri wa nini tena wakati ushafanya maamuzi...au ndio unataka ubadilishie gia angani kama mimi
 
Kuwepo macho na hawa watu wanao tuona sisi kaa jalala la bidhaa zao, wapo akina Forever, Travo,GNLD na hao walio kufata hawa watu mmmmhhhh...... miaka mingi imepita kidogo nilipigiwa cm na hawa watumwa wa GNLD na kuanza kuniambia kuhusu bidhaa zao na semina zao, nikaenda kwenye semina zao mmmhhh.......... kuweni macho na utajiri wa kwenye makaratasi.... kigezo kikubwa wanachotumia eti ukiwa member utapata nafsi za kusafiri mara kwa mara kwenda kutembelea sehemu mbali mbali na kukutana na watu walio tajirika na hizo bidhaa..... sasa na mimi mwaka kesho naanza kupaki dawa aina ya MBILIZI naombeni member wa kuwauzia
 
Kaaa pembeni usije ukajutia...Hizi biashara mpaka uje utajirike ni baadae sana..

Huko sana sana utaishia kufanyia watu kazi zao wao wanatajirika huku wewe ukipata kidogo mno..

Ni bora ufungue biashara yako nyingine uishughulikie mwenyewe tu..Huko ni majanga ndugu... Bidhaa zenyewe ni za PREMIUM PRICE na zinahitaji HIGH CONVINCING POWER kwa mteja anunue..

We nenda utarudi kutupa mrejesho hapa ukiwa unajuta...!!!
 
Bidhaa zao ni nzuri kwa ngozi!
Nataka kwa ajili ya matumizi tu sio bness!

Bness ni kupoteza muda,ni watz wachache wana uwezo wa kununua hizo bidhaa
 
Kaa mbali na hiyo business, infact kaa mbali na Network marketing business nyingi ambazo zinauza products... kama una gari nitafute nikushauri kuhusu Uber upate hela ya uhakika. its the only Online business yenye kichwa na miguu, zingine zote ukiingia utalia.. nilishafanya kazi na jamaa wanaitwa Organo Gold, pesa ilienda na hamna nilichoambulia... Njoo Uber kama una gari
 
Kuingia huko lazima ujitoe ufahamu yaani uwe kama PROFESA vile, ukimkuta mtu njiani unamsalimia kwa adabu ambayo hujawahi msalimia mzazi wako halafu unaanza kumpa elimu ya UTAJIRI atakapo jiunga na hiyo ORIFLEM kupitia wewe, unampa uwezo wa kujingenga kisaikolojia kuwa akitumia ORIFLEM uzee si tu mwisho chalinze bali hata zeeka hata akiwa na umri gani, yaani ni biashara ua kuweka matumaini kwa mtu tena unamlazimisha aote ndoto ukiwa nae barabarani, kama unaweza kuwa na akili flani hivi za kuparamia watu kwenye shuguli zao na kuwapa mahubiri ya bidhaa za kizungu, ingia haraka.
 
Kumbe ulishajiunga na mpaka namba ya siri ya uwakala unayo(ina maana hadi kiingilio ushalipa) we sasa unataka ushauri wa nini tena wakati ushafanya maamuzi...au ndio unataka ubadilishie gia angani kama mimi
Si kwamba kupewa namba ya siri unakuwa umejiunga. Sijalipia chochote ninachotaka kufahamu hapa ni kwamba je hawa jamaa wapo nchini na mienendo yao ikoje. Kama wako na taratibu salama pamoja na huduma zuri basi tajiunga lkn kama hawaeleweki naachana nao. Sina nia mbaya na kampuni.
 
UFAFANUZI.

1/Hiyo ni biashara ya mtandao(Sio mtandaoni) ambayo iko katika mfumo wa Pyramid, yaani kama upatu fulani(Wengi wanatumika kuwafaidisha wachache).

2/Ni biashara halali katika nchi yetu na mataifa mbalimbali duniani, kiufupi hakuna nafasi ya kirahisi ya kutapeliwa pesa zako kama ukikubali kujiunga(Taratibu zao ziko wazi kabisa).

3/Biashara hiyo haina tofauti yoyote ile kimfumo na Forever Living, Trevo nk. Utofauti upo kwenye bidhaa, mtaji wa kujiunga na Ukubwa wa faida.

4/Bidhaa zake ni bidhaa halisi, zenye ubora, Ghali zaidi na haziuziki kirahisi kwa mazingira ya Tanzania au watu wa kawaida au chini.(Unaweza ukakuta dawa ya mswaki(Meno) tube moja tu inauzwa shilingi Elfu 15, wakati Colgate ya ujazo huo huo inauzwa mtaani kwa shilingi Elfu 3)

5/Kufanikiwa katika biashara hiyo hapa Tanzania kwa sasa ni jambo la bahati nasibu sana. Kwa sababu faida kubwa haipo kwenye kuuza bidhaa zake bali ipo kwenye kutengeneza network follow up ya watu wengine watakaojiunga kwenye biashara hiyo nyuma yako. Huo ndio mtiti wake, ni issue nzito kushawishi watu wajiunge, sio jambo rahisi kwa watu kutoa mitaji yao ili wajiunge kupitia wewe.

6/Siku zote wahusika wa biashara hii watakuvutia kwa maneno mazuri ya kuonyesha Biashara hii ni rahisi kuifanya na itakuletea faida kubwa ya mamilioni tena kwa muda mfupi, na kamwe hawatakueleza upande wa Pili wa sarafu wa biashara hii kuhusu changamoto zake au hasara. Ni vizuri ukawa makini na mtafiti zaidi ili kujua kila kitu kabla ya kuamua kujiunga nayo.

Kwa leo nitaishia hapa.....
 
Back
Top Bottom