Ushauri wangu kwa Lowassa

hajanituma mtu kaka mimi ni mtanzania wakawaida tu na ninahaki ya kutoa maoni yangu.

Umetumwa tu wewe, tunajua JF imevamiwa na mamluki wa Lowassa. Nyie vibarua wa mafisadi hata mfanyaje kamwe hamuwezi kubadili mawazo na msimamo wa Watanzania zaidi ya milioni 40! Lowassa apelekwa mahakamani tu, hiyo ndio njia pekee ya kujisafisha
 
kweli kabisa anaweza kutumia pesa nyingi sana kwa njia anayoitumia ila mimi binafsi naona kujitokeza hadharani na kujibu maswali kwa watanzania itakua ni njia bora zaidi kwake. Kama kweli anasema tuhuma hizo hazimhusu basi itakua ni kazi rahisi sana kwake.

Ushauri wenu ni mzuri sana tena utamaliza ubishi ,minon'gono yote,na hata kutuhakikishia kama Lowasa anaonewa au kuwepo kwake nje ya jela ni ujinga wetu tu.kuna vitu viwili hapa:
1.ikitokea katika hao waandishi watakao alikwa wakaja na ushahidi na uthibitisho tosha jinsi alivyolihujumu Taifa kwa kutumia nafasi yake si atakuwa amejimaliza tena hata gari la polisi liwepo tayari .

2.Ikiwa ataweza kujieleza na kutoa uthibitisho kuwa hahusiki na yote ,hakuingilia ugawaji tenda ya Richmond,Hana uhusiano wa kibiashara na RA.Basi atajijenga sana hivyo ni uamuzi wake njia lipi achague.
jumatano iliyopita MM.MWANAKIJIJI Alimshauri vizuri sana achague njia y kupita ili apate.vinginevyo he will loose again.
 
:juggle: USHAURI WANGU KWA LOWASA
kwa yeye alivyo si lazima kuja kugombea Uraisi kama ndoto yake nihiyo atulie hata hizo hela nazomwaga mara makanisani mara vijijini atulie nazo kuna mambo mengi ya kufanya kwa mtu mwenye hela kama yeye japo sijui amepata wapi mamilioni hayoa nayogawa kila siku,naanza kuona kuna tatizo asiwe kama kina Papaa.WANAOGAWA HELAOVYO.
 
Naunga mkono aje hadharani ,aweke mambo haf=dharani ili kuondoa hii sintofahamu.Ni heri ikbidi akiri baadhi nakuomba radhi kwa umma ,atakuwa kiongozi ambaye ameonyesha mfano na kutoogopa watu.Kuliko hivi sasa kutumia watu,kwani kila anayemtetea hivi sasa anaonekana anatumika naye,bora aje yeye tumsikie
 
Hivi kiongozi akijiuzulu kwa makosa ya watu wa chini yake ni ufisadi??Mwinyi alipowajibika alikuwa fisadi?halafu nani asiyejua uchapaji kazi wake,nani angeamini kuwa katika kata ambazo viwanja vya shule katika mijiji mingi vilishagezwa kuwa mali binafsi leo vilirudi kwa amri Lowasa,leo twaweza kumwita mkuu wa shule za kata,Mfano:
 
Hata nyie mnaolipwa kwa ajili ya kumchafua mnamatatizo makubwa.mtuhumiwa gani aliyekwenda mahakamani akajishitaki ebu nenda kafungue kesi dhidi yake si una ushahidi kuwa yeye ni fisadi takuja kujibu tuhuma.Tatizo kubwa la watanzania liko hapa kuamini kila kitu wanasikia kutoka kwa yoyote na kufanya wao ndio wenye ushahidi wa kutosha kuliko hata yule aliye walisha uvumi huo .nimetoa changamoto dhidi ya tuhuma ambazo zinadaiwa zinamuhusu LOWASA tuwe huru kifikra ebu nitajie udhaifu na uwezo wa E L wakati yuko madarakani usianze matusi kashfa na kauli za kuudhi kuwa mpole makini taja.MIMI LOWASA NIMEMKUBALI NA KAA HURU KIFIKRA UTAMKUBALI TU.KWANI WENYE FIKRA HURU NDIYO WANA UONO WA UKWELI JUU TUHUMA ANAZOPEWA E L DHIDI YA MAADUI WAKE WA KISIASA WAKIAMINI WATU KAMA NYINYI WA KUSAMBAZA HABARI HIZO BILA YA KUULIZA WASWALI YA UCHAMBUZI UMPO.TOA USHAHIDI WA KISAYANSI UELEWEKE
 
Habari ndugu zangu wana JF. Kwa mara ya kwanza najitokeza kwenye jukwaa hili, kwa muda mrefu nimekua nikisikia tuhuma nyingi zikielekezwa kwa aliyekua waziri mkuu wa jamhuri ya Tanzania Mheshimiwa Lowasa, yeye binafsi anapinga tuhuma hizi na kusema kua sio za kweli.

Ushauri wangu kweke ni kwamba naomba aitishe mdahalo wa wazi utakaompa nafasi ya kujibu maswali mbalimbali yatakayoulizwa kwake ili watu tujue ukweli ulipo.

Binafsi namkubali sana ila nakua namashaka sana na hizi tuhuma zinazoelekezwa kwake kwa hiyo naomba aje ajieleze mbele wa wananchi tujue ukweli uko wapi. Naomba kuwasilisha.

Midahalo sio njia ya kumsafisha mtu, ila mtuhumiwa apelekwe mahakamani na wanaomtuhumu ili ukweli ujulikane. Vinginevyo mimi naamini kabisa tuhuma zote ni chuki binafsi za baadhi ya wasiopenda uchapakazi, ukali na uwezo wake wa kufanya maamuzi magumu.
 
Vyombo vya habari gani vya kumhoji Lowassa? Waandishi wa habari gani wa kufanya mdahalo na Lowassa wakati wahariri wengi tayari wako mfukoni mwa Lowassa? Hii itakuwa danganya toto tu! Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Absalom Kibanda, ambaye pia ni mhariri wa Tanzania Daima ni mfanyakazi wa Lowassa. Saeed Kubenea wa MwanaHALISI ambao wengi mnamuona ni shujaa wenu naye kanunuliwa na kuwekwa mfukoni na Lowassa.

Huo mdahalo na waandishi wa habari si utakuwa stage managed tu? Hapa ni usanii tu, sina imani na waandishi wa habari wa Tanzania kutenda haki mbele ya fisadi Lowassa.

Kama mdahalo uwe hivi, kambi ya mafisadi ( Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge) vs kambi ya wapambanaji (Samuel Sitta, Dr. Harrison Mwakyembe na Nape Nnauye). Huo ndio utakuwa mdahalo wa kweli, si wa wahariri walionunuliwa na Lowassa.

Njia pekee ya Lowassa ya kujisafisha ni kupelekwa mahakamani kama Jacob Zuma wa Afrika Kusini, akishinda kesi ya ufisadi wa abuse of public office kwa kutoa tenda kwa richmond na kuwa na utajiri usioelezeka (unexplained wealth) basi hata mimi nitamkubali.

Mamluki wanaolipwa vijisenti ili kumtetea fisadi Lowassa wana kazi kweli kweli....

Mh...wasiwasi wangu ni hao uliowaita wapinga ufisadi! How clean are they!?
 
Back
Top Bottom