Radio Producer
JF-Expert Member
- Feb 4, 2011
- 724
- 295
Habari yako msomaji!
KWA WAMILIKI WA RADIO CLOUDS FM.
Mimi Radio Producer napenda kuandika ushauri wangu kwako/kwenu wamiliki wa clouds Fm. Ni ushauri tu ukiupenda karibu, ukiona kawaida hakuna shida, silipwi wala sikulipi!
1. Nawapongeza sana Clouds fm kwa kujipanua na kusikika sehemu nyingi za nchi yetu ya Tanzania. Usikivu wenu ni mzuri kabisa, na mna kitu unique kabisa katika muonekano wa radio yenu. Nawapongeza sana kwa hili kwa sababu kila tunapotune radio hii huwa tunaipata bila shida kabisa! Hongereni pia kwa kujitahidi kutafuta wafanyakazi wenye uwezo wa kazi na ubunifu wa hali ya juu, ukweli wapo wafanyakazi katika radio yenu wanafanyakazi vizuri sana!
2. Pili napenda kuzungumzia vitu hivi (Format, Goal and Targeted Audience) ya radio yenu. Kwa harakahara bado natatizwa sana na format ya radio yenu, je ni music format au? hapa bado napata shida kulingana na mpangilio wa vipindi! Ninachoshauri hapa jaribuni kuiangalia format na muitumie kuprogram vipindi vyenu itasaidia sana. Goal yenu ni ipi hasa? je, mnaitumia kama ipasavyo? Tatu walengwa wenu (Targeted audience) ni akina nani? Mara nyingi nimekuwa nikifuatilia kwa karibu wakati mwingine nimeambiwa walengwa ni Vijana. Kama ni vijana je. format mnayotumia inapendwa na vijana? kama ni music format inaweza kuwa yes, lakini je goal yenu inafika sawasawa? (HAPA NDIO RADIO CLOUDS INAPOSABABISHA MAMBO YASOMEKE TOFAUTI KWA WASIKILIZAJI) kwanini??
3. Kwa sababu 1. Lugha- mara nyingi lugha inayotumika hasa kiswahili cha wadada hao na wakaka hao hakiendani na na wala hakiwezi kusimamia goal iende sawa. Kama mna malengo mfano ya kuielimisha vijana, unadhani kwa hali ya lugha inayotumika unajenga nini? Uharibifu mkubwa wa utamaduni wa mtanzania kwa matumizi mabaya ya lugha ya kiswahili. Nyinyi kama chombo cha habari mlitakiwa kuwa mstari wa mbele kuwafundisha vijana kutumia lugha vizuri zaidi ili tuwe na taifa lenye nguvu na utamaduni wa kupendeza!
4. Kwasababu 2. Uwezo wa baadhi ya watangazji. Kuna baadhi ya watangazaji wanashindwa kuitendea haki clouds fm kwa kushusha sifa na maadili ya radio. Si unajua mtangazaji akiharibu ameharibu jina la radio husika?? Wengine hawana uwezo mkubwa na wa kufikiri lakini hao ndio wanakuwa wategemewa wa kuchangia mijadala mbalimbali matokeo yake wanachangia kwa hisia zao wenyewe, ni hatari sana! Narudia tena ni hatari sana kwa mtangazaji kuruhusu hisia zake anapokuwa kwenye kipindi.
5. Kwa sababu 3. Vipindi vyenu- Jaribuni kuviangalia vipindi vyenu upya! vyaweza kuwa vizuri sana lakini format yake ndiyo inaharibu! angalieni maadili ya mtanzania pia! Hasa kwenye hivyo vipindi vya mapenzi na mahusiano jaribuni kuviprogram upya vikae katika hali ya kufundisha na kuelimisha jamii siyo tu kuburudisha! Tumieni lugha nzuri kwenye vipindi hivi ili atu waone userious wa kipindi. Wekeni vitu vizuri kwa walengwa, isije kuwa ka kuwa walengwa ni vijana kwa hiyo muwaandalie vipindi vya mtindo huo ili wafurahi, hiyo itakuwa ni hasara! Hata kama vijana ndio walengwa nia mathubuti ni kwamba wao wajifunze kutoka radio yenu siyo wajifunze lugha mbaya, matusi na mambo ya kiajabuajabu!
6. Kwa sababu 4. Balance- hata kama walengwa ni vijana waangalieni hata bonus audience! Kuweni na balance wapendwa media zinawatu wengi hata kama ni wa namna tofauti ila wote hujumuika pamoja na kusikiliza au kutazama! Sasa mmeandaa kipindi cha mapenzi kwa ajili ya kijana, watangazaji wenyewe tu wanaonekana wamelewa na mahaba unadhani kipindi hiki kitaangaliwa ma familia yote? kitamfundisha kijana au kumchochea kwenye hisia mbaya?
7. Mwisho, angalieni sana watangazaji wenye majina, wasifanyekazi kwa kuangalia majina yao! Wanaharibu lazima wafuate utaratibu kwa kituo husika! mtapata pesa sana lakini kama maadili yanapotea pesa hiyo haitawasaidia kitu kwa sababu mtakuwa manapotosha jamii! Jaribuni kuuangalia uongozi wenu hasa PROGRAM MANAGER! huyu bwana angekuwa serious hayo yote yasingetokea! Hapo ndio ikulu, kama PM yuko vizuri mambo yote yatakuwa safi tu upande wa programming!
Acheni kutumia lugha mbaya/mtaani/chafu/uchochezi, acheni kutumia hisia zenu mnapokuwa hewani, angalieni format yenu, goal yenu na targeted audience wenu, angalieni uwezo wa watangazaji wenu hakika mtajenga taifa!
Asanteni kwa kusoma.
Radio Producer
UK.