analysti
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 729
- 612
- Thread starter
- #21
Wapo kuku kama 50, nawafunga ndani lakini wanazunguka ndani ya fensi.yes nilipa chanjo ya new castle miez kama miwili na nusu iliyopita mkuu.
Nawalisha mchanganyiko wa pumba za mahindi, mahindi, mashudu, dagaa, mifupa na chokaa pia uwa nawapatia na majani atleast mara 3 kwa wiki.
Asante mkuu
Well, kwa dalili ulizozitaja, itakuwa ni Newcastle disease, Huwa inaweza kutokea hata kama umechanja, kutokana na vaccine failure, na ndo maana walioathirika ni wachache kwa maana wanakinga tayari, otherwise maumivu yangekuwa ni makubwa. Ikitokea incidence nyingine fanya yafuatayo:
1. Mtenge kuku mgonjwa kutoka kwa wenzake
2. Wape kuku wote antibiotic, preferably OTC 20% kwa muda wa siku tano, hii ni pamoja na kuku mgonjwa
Zaidi ni kwamba usisahau kuwachanja tena dhidi ya Mdondo 2wks from now!!.
Karibu sana Kiongozi!