Ushauri wa bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako, Jiondoe kugombea NEC ya CCM!

Mkuu Saint Ivuga, jukwaa hili pia kumbe huwa unatembelea?, nimekozoea kule kwako!.

Du graduation ya yupi, jumla ninao 6, nimehudhuria graduation ya mmoja mdogo kamaliza chekechea, anakwenda kuanza la kwanza, nikahudhuria ya mwingine kamaliza la saba hizi shule zxetu za Kayumba, anasubiri kuchaguliwa shule ya kata aanze form one!, pia nimehudhuria ya mwingine kamaliza form 4 hizi shule zetu za kata, wengine wawili pia nao wako sekondari hizi hizi za kata!, nilitamani sana wanangu nao wasome hizi shule za academy, ila kipato chetu sisi waandishi hakiruhusu!.
Sasa mkuu kipato hakiruhusu wakati unalipwa mahela kibao kwa ushauri, poa lakini nazidi kukuheshimu coz tayari nasikia Sumaye keshaangukia pua huko nyumba ndogo so usahauri wako si wakupuuzia, hembu mshauri na Zito naye.
 
BAK,

Unajua masuala yafuatayo carry totally different meanings when attended individually:


  • A Fan – Mshabiki;
  • A Follower – Mfuasi;
  • A Supporter – Kumuunga mkono mtu;

Mimi nadhani Pasco angekuwa na majibu kwa swali lako iwapo angesema yeye ni Follower au Supporter kwani by being a follower or supporter, it involves a certain ideological belief, or school of thought or political orientation; Vinginevyo kwa suala la ushabiki, nadhani utakuwa unamwonea tu Pasco kwani sote tunajua chanzo cha ushabiki in any context ni nini – mara nyingi hutokana zaidi na FAME OR ACHIEVEMENTS/ACCOMPLISHMENTS za anayehusika, iwe ni timu ya michezo, muigizaji filamu, mwanamtindo, mwanasiasa n.k

Pasco wakati wote amekuwa akijieleza in that context i.e. anajenga hoja zake kwa vigezo vinavyolalia zaidi
FAME OR ACHIEVEMENTS/ACCOMPLISHMENTS, na ni haki yake kufanya hivyo, ili mradi anaeleweka namna hiyo na yeye analijua hilo. Vinginevyo kama nia ya Pasco ni kukukusanya watanzania kwa levels zaidi ya ushabiki, ni muhimu abadilishe his style of presentation na iegemee zaidi towards him being a ‘FOLLOWER' OR ‘SUPPORTER', otherwise kwa mtindo wa SHABIKI, atazidi kuacha watu na maswali mengi kuliko majibu, huku muda kuelekea 2015 ukizidi kuyoyoma;
Mkuu Mchambuzi, asante kunisaidia, mimi ni mshabiki tuu, I'm neither a follower nor a supporter!.
 
kwanza unaonekana umetumwa na aliyekutuma naye hakujua anakutuma ukafanye nini,na wewe huelewi umetumwa kufanya nini,ushauri wako ni kama vile unamshauri mtu atapike chakula alichokula miaka 10 iyopita.KESHO KARIBU TUSHANGILIE USHINDI WA KISHINDO WA M-NEC KUTOKA JIMBO LA MONDULI MH EDWARD NGOYAI OLE LOWASSA
 
Haya 'mahaba' uliyonayo kwa lowassa yananipa taabu sana kufikiri.
Ni njaa au ushabiki.
Unaposemwa hakupi hela ni kama unampelekea ujumbe kuwa mzee hebu fanya mpango basi maaana kijana wako nimejitoa lakini mafao hujatoa.
Kilio chako nina imani amekisikia.
 
Pasco, umenifurahisha saana!. Kila aliyechangia maoni yako, kwa kuyapenda au kuyaponda umeyakubali na kusema umeyapenda. ume-like hata nonesense!. Si ajabu hata hii koment utai-like!. Ngoja nisubiri!
 
Wanabodi,


Pasco.
NB. Pasco wa jf, ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, ila ni mshauri wa mambo ya kisiasa na hulipwa
mahela mengi kutoa ushauri huo kwa wageni
!. ila kwa hapa jf, hutoa ushauri wangu bure kwa kujitolea, bila kulipwa
hata senti tano na yoyote, popote!. Baadhi ya shauri zangu, huzitoa kwa malengo maalum, ila ushauri huu
wa leo, lengo ni kumsitiri tuu na aibu huyu Waziri Wetu Mkuu Msataafu.

Huishiwi vituko Pasco?
 
Last edited by a moderator:
Pasco umechana mistari.Ila hujamshauri na Zitto.BY the way Zitto hawezi vunja CDM ila Lowasa anaweza vunja CCM.Na ilipo CCM ni kwamba hata CDM ikijeruhiwa CCM haiwezi pima ubavu kwa mgombea yeyote takayebeba bana ya CDM. Hakuna mtu mwenye nia letsa lone alone uwezo wa kumsafisha Lowasa.Na CCM wakimtosa mazima Lowasa anao uwezo wa kuiangamiza CCM kama si kwa mtandao basi kwa kauli ya mwisho kabla hawajakata mtandano ana kum kolimba.

Hii ni ishara kuwa CCM imeamua kumbana Lowasa lakini Chenge kubaki>Kweli Kasakazini CCM si yao.Ubaguzi to the maximum.
 
Pasco naona umegunduwa unafiki wa JK,ni vizuri kumshauri jamaa yako EL maana yule jamaa ni mnafiki haaminiki.Hata mimi nimeshangazwa kweli yani mke wake na mtoto wake wamemzidi licha ya yeye kumnusuru madaraka.

Sana sana alichoambulia ni kunyenyuliwa mkono juu kwenye kampeni,kusema hawajakutana barabarani,pamoja na ile kauli ya "Hii ni ajali ya kisiasa".Ushauri wako una ukweli,maana anaingizwa chaka.

JK hakutakiwa awe rais bana,huo ni ukweli.
 
Last edited by a moderator:
Pasco: I guess your thread is quite interesting for most JF members. Personally, reading it was I was exceedingly inspired given the reasoning and articulation of possibilities and circumstances you presented. Napata tabu ni jinsi gani hii message itakavyomfikia mlengwa? Au unategemea wana JF wampelekee hii information au ataisoma mwenyewe?

Naona kuna siri kubwa kati ya vigogo wa CCM ikiwa ni pamoja na Lowassa mwenyewe. Anaogopwa ndani ya chama chake mbona hawakuthubutu kumwengua mapema kama walivyomfanya Sumaye? Wanaogopa atamwaga mboga na ugali kwa mpigo au?? Kweli siasa ni mchezo wa ajabu mno especially where transparency is lacking.
 
Pasco said:
ni dalili za awali kuwa hatimaye, CCM itamtosa Lowassa kama ambavyo, watamtosa Sumaye!.
Kwa mujibu wa habari zilizomo humu, Sumaye keshatoswa
 
Kwa dhana iliyojengeka CCM, ili uwe mgombea Urais ni shurti uwe member wa NEC. Sasa EL atagombeaje Urais 2015 bila kuwa M NEC? This is a lifeline for Lowasa 2015 campaign. Akishindwa/au akiacha kugombea U NEC, ameshindwa Urais 2015, effectively making Membe a defacto president.
 
Kwa dhana iliyojengeka CCM, ili uwe mgombea Urais ni shurti uwe member wa NEC. Sasa EL atagombeaje Urais 2015 bila kuwa M NEC? This is a lifeline for Lowasa 2015 campaign. Akishindwa/au akiacha kugombea U NEC, ameshindwa Urais 2015, effectively making Membe a defacto president.
The only thing itamwokoa EL,ni kama atafunguka kuhusu Richmond,otherwise akajipumzikie zake Monduli akiomba Mungu asiingie madarakani rais atayeanzisha uchunguzi dhidi ya mafisadi.Maana nilisikia Januari Makamba akisema hawataki rais atakayekuja awe na visasi,pengine ndicho JK anachoogopa especially kuhusu Sumaye.
 
pasco;
"selfish, with unicentric view ambao wanaona upande mmoja tuu wa shilingi,, their side which is the right side, hawaoni, hawasikii, wala hawaambiliki, wanalotaka wao ni lazima liwe!"


1.huyu na zito wakisikiliza ushauri wako watakuwa hawana hizo sifa tajwa maana watakuwa wanaambilika!

2. Hakuna mtu anayekuwa na sifa ya 'uselfish with unisentric view ' alafu akabadilka kuwa kiongozi mzuri popote.
 
Pasco:

i) Lowasa hawezi kushindwa uchaguzi wowote ndani ya CCM. He is currently the most powerful politician in CCM. Kumlinganisha na Sumaye ni kutokuzingatia context. Nguvu ya Sumaye ilikufa mara pale uwaziri mkuu wake ulipoisha. Kumbuka sifa pekee aliyekuwa naye Sumaye kama waziri mkuu ni kwamba alikaa miaka kumi katika nafasi hiyo na hivyo akatengeneza cronies wengi sana ndani ya CCM waliopata madaraka na ulaji kwa kupitia yeye. Lakini sasa miaka kumi baadaye hana kitu kwa sababu hao jamaa aliowaweka wameshasambaratishwa wote. Tofauti ya Lowasa ni kwamba bado anaendelea kuwa na watu ndani wanaomwamini kama taasisi na kusema kweli ndani ya CCM yeye ndiye mwenye akili zaidi za kisiasa, kifikra na kiutendaji. Hii pia inaeleze jinsi CCM ilivyo hoi kwa sababu hakupaswa kuwa na taswira hiyo. Kwa hiyo, Lowas madamu unahusisha kura, Lowasa atashinda uchaguzi wowote ndani ya CCM.

ii) Uchaguzi nje ya CCM-Lowasa ni mwepesi na ni mzito pia. Ni mwepesi kama atapambana na wanasiasa wenye sifa maalumu kama akina Dk Slaa. Kwa maoni yangu Dk Slaa ana sifa moja kubwa inayomtofautisha na wanasiasa wengine active kwa sasa, nayo ni ukweli kwamba yeye ni mkweli na mhalisia (genuine and honest). Hii ni sifa ambayo ni adimu sana kwa wanasiasa wa Tanzania. Ni mzito kama ukimgombeanisha Lowasa na mwanasiasa mwingine ambaye si aina ya Dk Slaa, ambaye itakuwa vigumu kupata sifa za ziada za kumshinda Lowasa.

Let's wait and see!
 
Back
Top Bottom