Ushauri wa bure kwa Kikwete

Mimi sijazungumzia Magazeti; nimezungumzia taarifa za Election Observers walioshiriki katika mchakato wa uchaguzi.

Magazeti yana hulka ya kuandika vichwa vya habari na taarifa zitakazouzika.

Binafsi, sijazungumza kuwa mimi ni mshabiki wa Chama Tawala, bali naongea kama MZALENDO wa taifa la Tanzania. Gross Conclussion kuwa Uchaguzi wetu ulikuwa na Uchakachuaji sio suala muafaka.

NEC ishajibu hoja.

Kama ishu ni uchelewaji wa majibu; most of results zimetolewa within the TIMEFRAME agreed.

Ni jambo lililo dhahiri kuwa Tuhuma za UCHAKACHUAJI zilianza hata kabla ya Uchaguzi kama selling point ya CAMPAIGN huku ikiwa ni uchochezi.

Hali ya uchakachuaji Tz tunaijua sisi watanzania si hao observers, hawana huruma na sisi, wana lao jambo. Akili yako isiwe tegemezi. Tulia vizuri utajua ukweli.
 
Hii sijibu kutokana na hiyo signature message yako, we are located at different frequencies

tumia akili ya kuiga hata ya kuzaliwa nayo ama kusoma shuleni huna wewe Makame umeonesha
udhaifu mkubwa sana kwenye hiyo posti yakom......jitambue kwanza
 
OBSERVERS ni wa KIMATAIFA.

UCHAGUZI ni INternational Phenomena, na hao wana uzoefu wa kusimamia mazoezi kama hayo maeneo mbali mbali.

Sasa kama IMANI na OBSERVERS imetoweka ghafla, siwezi kusaidia sana; ila ingelikuwa hakuna maana kuwa na imani na taarifa zao; wasingekuwa wanaombwa kushiriki katika mazoezi ya aina hiyo.

Hali ya uchakachuaji Tz tunaijua sisi watanzania si hao observers, hawana huruma na sisi, wana lao jambo. Akili yako isiwe tegemezi. Tulia vizuri utajua ukweli.
 
Wana Blog wenzangu naona amnapoteza muda na huyu anayejiita Makame. Kwa kadiri ninavyomsoma yeye ni mtu wa kaaribu na Kikwete au ni mdau wa ufirauni wa CCM. Mtapoteza muda tu kubishana naye, mnajuaje pengine ni mdau halisi wa ufisadi wote uliotendeka na utakaotendeka kwa miaka mitano ya utawala wa wachakachuaji kura hawa? Hivi ni kweli yupo bado mtanzania wa kuzungumza lugha ya kuitetea CCM na ufisadi na uhaini wake ilioufanya kwa umma wa watanzania baada ya kushuhudia dhulma iliyotendeka? Binafsi namsifu sana Dr. Slaa kwa hekima yake ya kuamua kunyamaza maana yaliyotendeka itabaki kuwa ni aibu katika historia ya nchi hii. Namsifu kwa maana mamilioni ya watanzania waliogeuziwa uamuzi wao wa kumchagua wampendae na kufanywa ndondocha wangekuwa tayari kwa lolote endapo malumbano yangeendelea au serikali kuonyesha dalili za kumyanyasa. Ingefaa basi iundwe tume itakayojumuisha wajumbe wa kimataifa kuchunguza na kuwaridhisha watanzania kama haki yao ya kutawaliwa na serikali ya ridhaa yao haikuporwa na genge la CCM liikisaidiwa na vyombo vya dola. Wanaoisifia tume ya uchaguzi naona wana ajenda zao kwani imewaangusha kabisa na kuwakatisha tamaa watanzania. Baada ya maandalizi ya miaka mitano mizima maelfu walipoteza haki yao ya kupiga kura kwa kutoona majina yao! Huku wakijigamba kuweka kumbukumbu za wapiga kura kwenye mtandao na kufikia hatua ya kuhamasisha watu kucheki kwenye mtandao ili kucheki hadhi zao za upigaji kura - tume hiyo hiyo iliyosheheni wanaoitwa wataalamu wa mawasiliano ilishindwa kabisa kubuni program ya kumtamba mpiga kura na kumuwezesha kupiga kura popote nchini. Tumeshindwa hata na nchi kama Msumbiji na Burundi ambako mtu angeweza kupiga kura yake popote hata nje ya nchi!
Ni mamilioni mangapi ya wapiga kura walioshindwa kuwepo walipojiandikishia hivi kupoteza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura? Halafu tunashangaa kisanii eti walijiandikisha milioni 20 na waliopiga kurani milioni nane tu? Haya ikaja hatua ya kuhesabu (kujumlisha) kura ambayo ilitia kichefuchefu ati kuhesabu kura za kata moja zipatazo elfu sitini ilichukua zaidi ya masaa 72 kisa; ati walikuwa wakiingiza matokeo kwenye tarakilishi (Computer)! Kama hilo ni kweli basi inafaa tuwafukuze wote kwa kushindwa au kutokujua kazi. Lakini ukweli mtanzania yeyote anaoujua ni kwamba zilikuwa mbinu chafu za kuongeza kura za wagombea wa CCM ambao walishindwa vibaya na wapinzani, haswa wa CHADEMA. Ushahudi ni watu kukamatwa na kura zilizokwishawekewa alama kwa wagombea wa CCM au yule waliyemkamata aliwa na kura tatu tatu ili aongeze kura za CCM.
Kituko cha Tume cha nwisho ni kile cha kutangaza matokeo ya kura za urais kama santuri bila ya kujali malalamiko ya mmoja wa wagombea! Kulikuwa na shida gani kulinganisha matokeo waliyokuwa wanayasoma kwa manufaa ya kuliepusha taifa letu na vurugu kama za Kenya?
Mwisho nasema ni sawa CCM na Kikwete wamelazimisha kuitawala miili yetu, lakini rohoni tunaye aliyekuwa tamanio la wengi waliodhulumiwa. Hivi maana ya uhaini ni ipi kama si hii ya kuipindua ridhaa wa wananchi? Je tunapaswa kuwapongeza walouhatarisha mustakbali wa amani wa nchi yetu?

k
 
Simply beautiful! hii thread ni nzuri ila ina matatizo yale yale ya kikwetu!
Uzushi, kufikirika na kuongea bila evidence!
 
Kwa hakika AKASHUBE hongera..................!!!!!!!!!!!!!!!!!si vema kutia pamba masikioni..... tusome nyakati ndugu zangu......!!!!!!!!! kama ndivyo vidonda mbona havijakauka bado vinaendelea kutibiwa????????????????????
 
Sielewi hizi tuhuma dhidi ya Mheshimiwa Kikwete unazitoa wapi?

Election Observers kutoka taasisi mbalimbali za kimataifa wameshiriki na kusema kuwa Uchaguzi wa Tanzania ulikuwa wa Huru na Haki, na pia kama kuna tuhuma zozote za aina hiyo; kuna utaratibu wa kuziwasilisha ili kubaini kama haki imetendekea au la.

Akashube ndugu yangu, nakusihi usiwe MCHOCHEZI

Tuambie utaratibu wa kuwasilisha tuhuma ukoje Tanzania?
 
Kule CHADEMA every one is a suspect. Inategemea matendo yako na ndio maana Zitto alipotaka kugombea Uenyekiti (alikuwa-suspect) aliposhindwa kujieleza akaambiwa "njia nyeupe". Kwa hiyo usiwe na wasi wasi kazi anayofanya Mabere pale Chadema ni ushauri wa kisheria, haijarishi wewe ni UWT (sorry UWC) au vipi. Kule NCCR alikuwa kiongozi akakosea kumpisha Mrema na chama kikaanguka.
 
Ushauri unaompa kikwete ni wa kweli and if he is a smart guy he should take up your advice seriously- baada ya kiwete kutangazwa mshindi niliwahi kuwaeleza wanajamii kwamba ushindi wake ni misiba mingi na vilio vingi vya watanzania kama anawapenda watanzania kama anavyojipenda yeye. hapa kipimo chake kipo katika uamuzi wa jinsi atavyo ongoza nchi wakati akijua fika hana watu wa kuwaongoza.
 
Watu wamempa kura kikwete kwenye ballot box.

Waosha vinywa bado hawajakubali, pamoja na kwamba slaa wao amekubali baada ya kukurupuka!

W
ushauri unaompa kikwete ni wa kweli and if he is a smart guy he should take up your advice seriously- baada ya kiwete kutangazwa mshindi niliwahi kuwaeleza wanajamii kwamba ushindi wake ni misiba mingi na vilio vingi vya watanzania kama anawapenda watanzania kama anavyojipenda yeye. hapa kipimo chake kipo katika uamuzi wa jinsi atavyo ongoza nchi wakati akijua fika hana watu wa kuwaongoza.
 
ZITTO

Mheshimiwa Zitto Hakushindwa Kujieleza.

Mheshimiwa Lema nimeanza ku doubt leadership capability yako following that posting.

Mheshimiwa, BORA UKAE KIMYA KULIKO KUPOST POINTLESS.

Naomba ukumbuke kuwa wewe ni mtu mwenye Dhamana kubwa, hivyo kauli yako ni NZITO, hasa hasa kwenye Public Forum kama hii.

Au na wewe unakurupuka Kama Slaa?

Kule CHADEMA every one is a suspect. Inategemea matendo yako na ndio maana Zitto alipotaka kugombea Uenyekiti (alikuwa-suspect) aliposhindwa kujieleza akaambiwa "njia nyeupe". Kwa hiyo usiwe na wasi wasi kazi anayofanya Mabere pale Chadema ni ushauri wa kisheria, haijarishi wewe ni UWT (sorry UWC) au vipi. Kule NCCR alikuwa kiongozi akakosea kumpisha Mrema na chama kikaanguka.
 
AKASHUBE

HUO NI USEMI WA KIDEMOKRASIA ILIYOKOMAA.

HAKUNA ALIYESHINDA, walioshinda ni wananchi [Wapiga Kura]; ndio walioamua.

sasa wewe kama unafikiria OTHERWISE, umepotea kidogo.

Wamarekani wanajuta...... na mfano ukiwa tamko la Collin Powell mwaka 2005 ....wanajuta kwa kitendo cha majeshi yao na yale ya washirika wao kuvamia Irak.

Msemo unaotumiwa ndani ya shirika la ujasusi la marekani CIA na Uingereza MI6 pamoja na lile la Canada CSIS ni 'Sadam has killed many in death than when he was alive'.

Kama historia imetufundisha lolote haki huua wengi zaidi inapokuwa imekufa kuliko inapokuwa hai.

Kikwete jaribu kukaa chini na wagombea wenzako muelewane....jifunze mlichofanya Zanzibar ambacho kimewawezesha kuiba bila kupingwa.

Wagombea wa Upinzani na wapiga kura wao watasababisha uharibifu mkubwa usiotibika kwenye kushindwa kwao kuliko hata kama mngeacha haki ichukue mkondo wake.

Kikwete mustakabali wa Taifa hili uko mikononi mwako..Kaeni viongozi wote mtusaidie wananchi.....KUMBUKA...HAKUNA ALIYESHINDA AU ALIYESHINDWA UCHAGUZI HUU....UNAELEWA FIKA KWA NINI MSEMO HUU ULITUMIWA NA WAGOMBEA WAWILI WA ZANZIBAR.....SHAURI YAKO!!!!!!!!!!!!
 
Angalia anayeandika; na alietoa ushauri, na alieshauriwa.
Hivi kwa hali ya kawaida tu ya KUTAFAKARI, bila ya USHABIKI; yupo hapo anayemuingia Jakaya Mrisho Kikwete

1. Rais Wa Jamhuri
2. Cabinet minister Mzoefu
3. Mwenyekiti wa CHAMA

Dk Slaa Hajawahi kukamata hata mojawapo ya Sensitive Posts alizokamata yeye.

Halafu Somebody anayejiita CROOKED [Kweli yuko crooked] anamuita atrophied brain; LOOK who has that BRAIN?

I don't think if he can work on this,he has an atrophied brain!!!
 
Angalia anayeandika; na alietoa ushauri, na alieshauriwa.
Hivi kwa hali ya kawaida tu ya KUTAFAKARI, bila ya USHABIKI; yupo hapo anayemuingia Jakaya Mrisho Kikwete

1. Rais Wa Jamhuri
2. Cabinet minister Mzoefu
3. Mwenyekiti wa CHAMA

Dk Slaa Hajawahi kukamata hata mojawapo ya Sensitive Posts alizokamata yeye.

Halafu Somebody anayejiita CROOKED [Kweli yuko crooked] anamuita atrophied brain; LOOK who has that BRAIN?

Yaap hata Iddi Amin amewahi kukamata nyadhifa kubwa mno kuliko wagombea wote wa kiti cha urais ikiwa ni pamoja na JK. Kumbuka alikuwa Army General na baadaye Field Marshal na kisha Rais. Tofauti yake na JK ni kwamba yeye hakuungwa mkono na mataifa ya magharibi. Kwa hiyo vitendo vyake havikubatizwa.

Mtindo wa vyeo vya Idd Amin hauna tofauti na Jakaya Kikwete, Mfano udokta, urais, e.t.c
 
LET US COMPARE DR SLAA AND PRESIDENT KIKWETE

Socialy, Slaa amechakachua ndoa yake na Ndoa ya Watu wengine; akapora Mke wa watu. Kikwete Hana Uchafu huo.

Kikwete anaweza kufanya analysis na kuweza kubaini kama anachomekewa, angalia mfano wa ile issue ya AMBULANCE ya LONGIDO; slaa anakurupuka; angalia ILE BARUA.

Kikwete ana maamuzi na anajiamini; Slaa hana hata kimoja NDIO MAANA KIKWETE ALIGOMBEA URAIS NDANI YA CCM 1995, akashindwa na MKAPA; na akaheshimu Demokrasia. Akarudi tena 2005; akashinda. 2010, akashinda TENA. On the contrary, Dr Slaa alifanya kubembelezwa na wanachadema akagombee. Alishawishiwa, URAIS UNAHITAJI MTU KUJUA QUALITIES ZAKO; ukimuona mtu anasitasita; JUA HANA QUALITIES HIZO.

Ndio maana watu MUHIMU WANAMUHESHIMU KIKWETE.

BLAIR, BROWN, CAMERON, BUSH, OBAMA, CLINTON, MANDELA ni among INternational figures zinazomuheshimu

Usiongee tu

Masuala ya uchafu wa ndoa muulize Kikwete kama yuko tayari kujadiliwa kwa hilo. Hapa unaandikia watu wenye kujua mengi, sioni hekima ya kujadili haya, kama ungekuwa mtu wake wa karibu usingejaribu hili..

Kuhusu kuchomekewa, naona kuna 'research' unaifanya hapa hivyo sikupi faida.

Kuhusu kuheshimu maamuzi ya 1995. Hayo ni mambo ya CCM kwamba kuna mtu au kikundi cha watu wachache kinaamua nani awe kiongozi. Maana ukweli ni kuwa Kikwete aliwabwaga Msuya na Mkapa mwaka ule. Uamuzi wa CCM kuongozwa na matakwa ya dikteta fulani au kikundi fulani cha kisultani isiwe ndio msaafu kwamba hata Dr. Slaa afuate nyayo za nyoka.

Ukiondoa Mandela ambaye anaheshimu watanzania wote hata kama ingekuwa Zuzu kawa Rais wa Tanzania, na sababu ya Mandela kufanya hivyo unaijua fika.

Hao wengine unajua fika wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi. Pia sioni kama ni vema kuorodhesha hapa makampuni makubwa ya uchimbaji madini, utafiti madini, ushauri na maeneo mengine ambapo nchi zao zinafaidika kwa kiasi kikubwa.

Kama kweli Kikwete amefanya kazi nzuri miaka mitano iliyopita, kwa nini pamoja na kuiba kura ameshuka kutoka zaidi ya 80% hadi 61%???

Utetezi wako unafaa ndani ya CCM peke yake. Upeleke huko wakupigie makofi, lakini fanya haraka kabla ya wiki ijayo maana utakosa washabiki. Wengi wanakenua na kupiga makofi saa hizi kwa ajili ya uwaziri, ubunge viti maalum, ukuu wa wilaya na mengineyo mengi. Maana mnadai CCM kazi nyingi....au kupeana kwingi???? kwa manufaa ya nani?????
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom