Alipokuwa anajiandaa kuwania kiti cha PM nchini Uingereza Tony Blair alisisitiza kukifanyia maboresho chama chake cha Labour. Kwa ahadi hiyo alishinda uchaguzi kwa kishindo kwa viti 179. Ushauri wangu kwa JK ni kuwa, aifanyie CCM mabadiliko makubwa. Atafute watafiti kutoka makampuni makubwa ya utafiti ikibidi kutoka nje, wanaharakati na wasomi wamsaidie namna ya kuunda NEW CCM. Ninaamini, bado CCM wana nafasi ya kufanya vema zaidi iwapo tu watajivua gamba walilonalo maana limechakaa. Nina maana wafanye REJUVINATION