Ushauri wa Bure kwa CHADEMA

tatizo sio kuwashawishi waislam ili wakipende chadema, tatizo ni kwamba hiki ni chama chenye sera za kidini na kikabila. Na hii imetokana na na kuwa na uchu mkali wa kuingia ikulu haraka haraka, hivyo kulitumia kanisa ili chati yao ipande kwa haraka sana. Hii inawagharimu sana

hata mbeya ambao walikishabikia na kupata wabunge kupitia chama hicho, wakagombana kwenye ugawaji wa viti maalum. Asilimia 80 ya viti maalum vilikwenda moshi na arusha. Sasa unatarajia kuwaeleza nini wananchi ikiwa katibu mkuu wa chadema alishasema kama hawataki wahame chama. Maana udikiteta uliopo hakuna hata majadiliano.

Ikiwa mgombea wao wa urais katika uchaguzi mkuu 2010 alipoulizwa kuhusu tuhuma za kuhusishwa chama chake na udini, alishindwa kujibu au kuwashawishi wananchi kuwa hizo shutuma ni za uongo. Sasa ndugu yangu unatarajia huyu mtoa hoja atawezaje kuwashawishi waislam kuwa chadema ni poa, haina udini.

Jisafisheni kwanza ndani ya chama chenu kabla waislam wanaowapenda hawajawapigia debe.

wabunge wa viti maalum chadema ni 25 , 80% ya 25 ni 20 je unaweza kuwataja hao wabunge 20 wanaotoka arusha na mosh?
Kuhusu udini, kati ya cdm na ccm ni chama gani cha kidni? Mfano tamko la bakwata igunga lililenga chama gani kupiwa kura na waislam hamieni facebook ndio eneo la hoja mfu
 
Jina lako , kiswahili chako na mawazo yako pia ID yako VP= Visiwani Pemba , mshenzi sana sana wewe nilitaka kukutukana kakini najua naweza kukumbuna na tuhuma ila nasema Chadema ni Chama cha Siasa .Sasa kinafanya siasa , sijawahi waona wala wasikia Chedema wanatoa salam zozote kwa Wakristo muda wowote wa sherehe zao .Kama nikmekosea nielezwe hapa .Baada ya nasema watanzania wote wenye nia njema waende chadema regardless imani zao za dini .
 
Hii hoja ni nzito sana na ninaomba WanaJF msikiponde ila tuijadili. Alichosema huyu ni cha kuzignatiwa sana. Naomba viongozi wa CDM muitafakari.
 
Demographics ziko wazi na zinaonesha kwamba chama chochote ambacho kitasusiwa na Waislamu ama Waristu hakiwezi kutwaa dola. Siri moja kubwa ya CCM kushinda ni kuvutia dini zote.
Huu ni mchoko wa kifikra, waislamu, wahindu, wakristo, wayahudi,atheists, Banyan,Taoism, .................wanamahitaji tofauti ya kidemokrasia?Haya huyo raisi muislam tuliye naye sasa amewaletea maendeleo yapi ya kipekee waislam?Hoja za kidini zinachosha sana ubongo nawashauri mzipeleke huko huko kwa wanaotaka kwenda mbinguni!
 
Safi sana mleta mada!! Ndg zangu wana jf, mtakumbuka baada ya uchaguzi wa Igunga nilileta thread iliyokuwa na heading"CABINET CHADEMA". Nilielezea suala hili nikawaomba viongozi wetu walishughulikie.
Ndg zangu msisahau kuwa ukombozi unaotafutwa sasa ni wa watz wote bila kujari imani zao, hivo basi ni jukumu la kila mmoja wetu hasa viongozi kuhakikisha tunaondolewa MZIZI WA UDINI unaomwagiliwa na chama tawala.
Mambo haya si ya kubeza hata kidogo ikiwa tunaitaji ukombozi wa kweli.
Ndg zangu wana jf, tambueni UDINI na athari zake, tujiulize wanaochochea udini wana malengo gani, tuukemee kwa nguvu. Najua kuna wengine walipwa kwa kuuchochea udini kisa wanaoukemea wamelenga kuimalisha cdm pasipo kujua walitendalo!!
WA TZ TUSHIKAMANE, WAKRISTO KWA WAISLAM TUJENGE TZ, TUPINGE UFISADI KWA PAMOJA!!
 
Tatizo sio kuwashawishi waislam ili wakipende CHADEMA, Tatizo ni kwamba hiki ni chama chenye sera za kidini na kikabila. Na hii imetokana na na kuwa na uchu mkali wa kuingia IKULU haraka haraka, hivyo kulitumia kanisa ili chati yao ipande kwa haraka sana. Hii inawagharimu sana

Hata mbeya ambao walikishabikia na kupata wabunge kupitia chama hicho, wakagombana kwenye ugawaji wa viti maalum. Asilimia 80 ya viti maalum vilikwenda Moshi na Arusha. Sasa unatarajia kuwaeleza nini wananchi ikiwa katibu mkuu wa CHADEMA alishasema kama hawataki wahame CHAMA. Maana udikiteta uliopo hakuna hata majadiliano.

Ikiwa mgombea wao wa Urais katika uchaguzi mkuu 2010 alipoulizwa kuhusu tuhuma za kuhusishwa chama chake na udini, alishindwa kujibu au kuwashawishi wananchi kuwa hizo shutuma ni za uongo. Sasa ndugu yangu unatarajia huyu mtoa hoja atawezaje kuwashawishi waislam kuwa CHADEMA NI POA, haina udini.

Jisafisheni kwanza ndani ya CHAMA CHENU kabla waislam wanaowapenda hawajawapigia debe.
Usije hapa kuandika bila data unafikiri sisi wote hapa jf vilaza wenzako, sema mgombea urais wa chadema aliulizwa nini kuhusu udini akashindwa kujibu? aliulizwa na nani? mimi najua cdm haiwezi kuingia kwenye mtego wa kipumbavu wa ccm ambao cuf waliteleza wakaingia na wakaua chama, kusema cdm ni chama cha wakristu ni ujinga uliopitiliza maana ukichukua viongozi sita wa juu wa chama wanne ni waislamu sasa huo udini uko katika nyanja zipi?
viongozi FREEMAN MBOWE MKRISTU MWENYEKITI, MAKAMU MWENYEKITI BARA, SAID ARFI,ZANZIBAR SAID ISSA MOHAMED WAISLAMU .KATIBU MKUU DR SLAA MKRISTU, NAIBU KATIBU MKUU BARA ZITTO KABWE MWISLAMU ZANZIBAR HAMAD MUSSA MWISLAMU. sasa hizo propaganda za ccm ni upuuzi mtupu na watu wenye akili wanajua ccm inatumia baadhi ya waislamu wenye njaa kali inawalipa kueneza huo ujinga. muasisi wa udini ni kikwete baada ya kushikwa pabaya na DR SLAA kwenye uchaguzi na nchi hii ikiingia kwenye tatizo la udini atakae jibu ni kikwete na ccm.
 
Huu si ushauri wa bure, ni ushauri aghali na una athari kubwa. Nakutaarifu kuwa CCM haijawahi kushinda kwa maelezo yako. Inapora haki na zoezi la kupiga kura kwa wizi na kutangaziwa ushindi kwa mfumo iliojiwekea. Ndiyo maana ya kudai Katiba Mpya na yenye kuzingatia maoni ya wananchi wote. Uislamu ukristo ni kitu binafsi si cha kukiingiza kwenye siasa kama unavyokiri kuwa ndio mchezo wa CCM.
 
mh nchi hii inamatatizo mengi sana kuliko,udini kuna katiba mbovu na hila za kuleta katiba mbovu zaidi! kuna magonjwa ya kawaida yanaua watz miaka 50 ya uhuru,kuna ukosefu wa huduma za jamii hata maji tu hakuna wakati 13% ya maji baridi yako TZ! KUNA raslimali zinaibiwa! kuna ukosefu wa utawala bora ukiukwaji wa misingi ya demokrasia ! hivi sisi waislamu tunawaza nini? mbona tusiwape CHADEMA support kwanza kwa mambo ya jumla tunajibagua HATUONI KAMA NI UBINAFSI MKUBWA ? na CDM imeandika wapi kwenye katiba yake kuwa haiwajali waislam mpaka tuweke hofu!? WAISLAM TUNAENDA WAPI?

hahahaaa eti ustaadh!
 
mtoa mada una point kubwa sana na muhimu sana kwa ustawi wa chama chetu
 
Nakubaliana na wewe kuhusu kuwa na mijadala na watu mbalimbali vikiwepo vikundi vya dini. Ila kitu kimoja ambacho sikipendi kabisa ni hii tabia ya viongozi na hasa rais anatoa chakula kwa watoto yatima au wazee n.k wakati wa sikukuu za dini au kitaifa na kuita 'zawadi'! Chakula ni zawadi?

Najua kuwa huu ni utaratibu wa siku nyingi lakini kwa nini karne hii watu hawataki kufikiri wanaongoza nchi kwa ku-copy & paste? Rais anawapa chakula watoto yatima au wazee wasiojiweza wakati wa shule je baada ya sherehe watakula wapi? Nani mwenye jukumu la kuwapa chakula wazee wasio jiweza au watoto yatima? Na inakuwaje unaita chakula zawadi?

Mfano kalamu ni inaweza kuwa zaidi, na unaweza kuishi bila kupata zawadi hiyo (kalamu) lakini huwezi kuishi bila chakula! Sasa inakuwaje rais wa nchi akumbuke kuwapa chakula maskini hawa wakati wa sherehe baada ya hapo anapotea! Haya ni makidai ya makumpuni binafsi, nilitegemea serikali iweke sera/mpango wa kuhakikisha kuwa hawa wazee wasiojiweza wanapata chakula muda wote wa mwaka na sio kuwafanya kama maonesho wakati wa sherehe wakimata mbuzi eti na unga - eti zawadi?

maneno yako yamenigusa sana, najifunza ni jinsi gani niwe kiongozi bora. Mwenye uelewa atakuwa amejifunza la muhimu sana ndugu. Naddhani wewe ni aina ya viongozi tunaowahitaji ila tunawakosa. God bless you.
 
Na mimi nishawahi kuwaza kama mleta mada. Natamani CCM watoke madarakani kwa kushindwa kwa kishindo ili wasipate mwanya wa kuchakachua na ndipo suala la kutegemea kura za waislamu linapojitokeza. Lakini baada ya kuwaza sana hasa katika kufikiria ni mkakati gani chadema wanaweza kuutumia kupenya kwenye ngome za waislamu nikagundua pengine si muhimu sana kwa Chadema kuhofia jambo hili la kufanya jitihada za makusudi kuvutia kura za waislam au kutamani sana kwenda ikulu. Kama watanzania walio wengi (wakiwemo waislamu) hawataipigia kura chadema eti kwa sababu fulani fulani za kidini au kikabila badala ya kuangalia hoja na sera basi huo hautakuwa udhaifu wa Chadema bali wa wapiga kura wenyewe. Na kinachoifanya Tanzania iendelee kuwa na umaskini, ujinga na maradhi, ni kwa sababu wapiga kura wengi ni maskini, wajinga na wagonjwa kiasi cha kushindwa kuchagua chama sahihi. Sasa hapa tusitegemee miujiza. Mpaka pale watu watakapoanza kupambanua kwamba dini zetu hazitusaidii kupambana na ufisadi, ujinga wala maradhi, na makabila yetu hayatusaidii, na kwamba tusitumie vigezo hivi katika kuchagua chama au mgombea.....basi hapo ndipo tutakapokwamuka kama watz, waislam, wakristo, pamoja na makabila yetu.
asante mkuu! Kwanini watu kama wewe msigombee uongozi? Halafu haya mambo ya kutumia id feki humu yanasababisha tusiwajue watanzania wenye machungu na nchi yetu. Ufike mda tuliangalie hili ili watu kama wewe mjulikane mtusaidie.
 
siku hizi kuna usemi kuwa “kakumbuka shuka huku kumekucha”. Ni usemi ufananao na “majuto mjukuu”. Mwanasiasa makini ni Yule anaesoma alama za nyakati na kuwa na dira ya kumfikisha kwenye mafanikio. Mwanasiasa hodari lazima awe anabadilika kutokana na mazingira yaliyopo. Tatizo la vyama vyetu vya siasa na wanasiasa, hawapendi kusikia upande wa kukosolewa! Wanachotaka kusikia ni sifa! Ukawsifu wanafurahi. Natoa nasaha zifuatazo kwa vyama vya siasa Khasa ccm, chadema na cuf huku nikieleza mapungufu / kasoro za kila chama.

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

chama cha ccm ni chama kikongwe. kina makada wazoefu wa siasa za kila aina. siasa baridi, siasa safi na siasa chafu. kina mabingwa wa propaganda. pana uwezekano, kina mamluki katika KILA chama cha siasa. Ccm kina sifa kuu moja: kimeunganisha watanzania kutoka ktk kila kanda, dini, rangi na kabila. hali hii imetokana na kuwa chama pekee kwa miaka mingi hadi mwaka 1992. huwezi kusema ni cha wakristo au waislamu. wote ni chama chao. Kina kasoro nyingi ambazo zinatokana na KUKOSEKANA UWAJIBIKAJI NA UTAWALA BORA. kinasuasua ktk kuwaadhibu wanachama wake wanaotajwa ktk kashfa mbalimbali za rushwa. kukumbatia wala rushwa ni ishara ya kwamba rushwa ipo na imeshamiri. hali hii inatusababishia maendeleo duni. Baadhi ya wapinzani wanasema maana ya ccm ni chukua chako mapema. Kauli hii inatokana na wizi wa mali ya umma wakupindukia wa viongozi wa serikali. Sera ya KULINDANA inaharibu utendaji wa ccm na serikali yake. Ccm wana mtaji wa watanzania wengi ambao ama hawajafikiwa na vyama vya upinzani (hufikiwa siku moja tu ya kampeni ktk miaka mitano) au wana mapenzi ya kupindukia kwa ccm. Hali hii inawasaidia sana ccm

ccm wana hali ngumu kuhusu mgombea urais 2015 lkn wana sifa moja. wanaweza kwenda dodoma (kizota) wakiwa na tofauti kubwa. la ajabu wanatoka wakiwa kitu kimoja na wagombea wanapeana mikono. sijui huwa wanafanyaje!!!!!!!!!!!!! Sasa hivi kuna makundi ya wagombea lkn atapitishwa mmoja na wote watakaa kimya!



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
chama cha chadema ni chama ambacho kimefanya vizuri sana ktk uchaguzi wa mwaka 2010. idadi ya wabunge wake imeongezeka sana na ndiyo chama kikuu cha upinzani. kina viongozi jasiri ambao ni wabunifu na hawana uwoga ktk kueleza na kutetea ukweli.
Chadema kina kasoro kadhaa zifuatazo:-
a). viongozi wake wakuu wana ushindani wa kisiasa, sifa na umaarufu. hili ni tatizo kuu chdm. kushindana huku kumewafanya waogopane na kuoneana wivu. wanaweza kuonekana wana safu moja lkn ukiangalia kwa jicho la kiuchambuzi utagundua kuwa slaa, mbowe, zitto, lissu, msigwa, mnyika nk...... wana matabaka ya ndani kwa ndani.

b). chama chochote lazima kianzie ktk eneo mojawapo ktk nchi yetu. chdm kilianzishwa na mtanzania kutoka kasikazini. bila shaka mizizi yake ilianza kuimarika kaskazini. ccm wakatumiya mwanya huu kukipaka matope kuwa ni chama cha kikanda na kikabila hadi wakatafsiri chadema kuwa ni chagga development manifesto (ilani au mradi wa kuwaendeleza wachagga). hali hii imefanya watanzania wengine waogope kujiunga na chama cha chdm.

c). ccm wamepakaza kuwa chdm ni chama cha wakristo. wakawa wanatoa mfano wa viongozi wake wakuu. wakasema dk. kabourou alipokua katibu mkuu, alipigwa vita kwa kuwa ni muislamu. kutodhihirika kwa majina ya kiislamu ya bob makani na zitto kabwe, kulifanya watu waamini kuwa viongozi wote wa chdm ni wakristo. chdm hawakujitahidi kuweka wazi kuwa bob makani, zitto kabwe na mzee arfi ni waislamu. japo mzee arfi anajulikana lkn amekua hapewi nafasi ktk majukwaa ya chdm licha ya kuwa ni makamu mwenyekiti. Propaganda za kuwa chdm ni chama cha wakristo, zimewafanya waislamu waliowengi waogope kujiunga chdm. CHDM WATAFAKARI NAMNA YA KUTOKOMEZA MADAI HAYA!

d). chdm kimeridhika kwa kuwa na mashabiki na siyo wanachama wakereketwa. kimesahau kuwa kasoro ya ccm ktk kura za maoni mwaka 2010, ndizo zilizochangia chdm kupata wabunge waliohama ccm. Vilevile baadhi ya wanaccm walikikomoa chama chao kwa kuipa chdm kura. Hii ilitokana na hasira za kura ya maoni ndani ya ccm. huu ndiyo ukweli kuhusu mwaka 2010. MFANO MDOGO NI KWAMBA IRINGA MJINI WALIMTAKA MWAKALEBELA. ALIPOPITISHWA MBAGA, WANACCM WOTE WAKAMPA KURA MSIGWA WA CHDM. HAWA BADO NI WANACCM HADI LEO NA WANAIPENDA CCM! pana uwezekano mkubwa kuwa iwapo ccm itacheza karata vizuri, itarudisha sehemu kubwa ya viti vyake katika uchaguzi wa mwaka 2015. ufunguzi wa matawi ya chdm unafanywa sn vyuoni na nje ya nchi kuliko vijijini. hii ni kasoro! CHADM inategemea mikutano ya hadhara ya siku moja kuliko uhaasishaji wa kila siku matawini.

e). kinyang'anyiro cha kumtafuta mwenyekiti wa chama na mgombea urais mwaka 2015 nalo ni tatizo chdm. mbowe, zitto, lissu na slaa wote nadhani wana nia ya kugombea urais (japo kuna utata kwenye umri wa zitto). slaa alifanya vizuri 2015 lkn wengine wanamuona kama mzee ambae huenda asiwe na mvuto 2015. Kashfa lukuki anazo undiwa wengine wanasema zinatoka ndani ya chdm! mbowe ana sifa lkn ile propaganda ya ccm kuwa chadema ina wenyewe, inamgharimu kwa kufanya wanachdm kutoka mikoa mingine wasimkubali.


f). lugha inayotumiwa na wanachama wa chdm kuwaelimisha wanachama wa vyama vingine ni kali sn. Inatumika jazba sn kuliko busara! Hili jambo linafanya ongezeko la wanachama chdm kusuasua. Vijana wasomi kutoka vyuo wanajazba na wanataka mabadiliko leo hii siyo kesho. Chdm kina jukumu la kuwaelimisha vijana wake kuhusu lugha ya kutumia kuwavutia wanachama. SILAHA KUBWA NI KUMUELIMISHA MTU SIYO KUMTUKANA!


Civic United Front (CUF)
chama cha wananchi cuf hakikufanya vizuri mwaka 2010 tofauti na chaguzi zilizotangulia. ni chama ambacho kina kasoro zifuatazo;
a). uongozi wa juu wa chama haubadiliki. japo prof lipumba na maalim seif wamejaribu kufafanua kuwa wao ni wapiganaji ambao wako vitani hivyo makamanda huwa hawabadilishwi kama nguo. Wakibadilishwa malengo yatapotea. kutobadili viongozi wa juu kumetumiwa na ccm pamoja na chdm kuisulubu cuf.

b). ccm ilianzisha propaganda kuwa cuf ni chama cha waislamu. kama ilivyo chdm, cuf nayo ilianzia sehemu mojawapo ya jamhuri yetu. wakazi wa eneo la visiwani wengiwao ni waislamu. cuf ikawa na wanachama wengi wa mwanzo wakiwa waislamu. hali hiyo ikatumiwa kisiasa na ccm kuwa cuf ni chama cha kidini na wakristo waliowengi jambo hilo limewatia hofu kujiunga cuf! wengi wanakiita chama cha wapemba na waislamu

c). licha ya profesa lipumba kuwa msomi lkn ameshindwa kuwavuta wasomi wenzake kujiunga na cuf. chdm kimefanikiwa kuwavuta wasomi wengi tu! kosa hili la lipumba limekiathiri sn chama.


d). safari za mara kwa mara za lipumba na za muda mrefu nje ya nchi zinachangia kudumaza chama. Hafanyi uhamasishaji hadi kipindi cha kampeni. Jembe linalo saidia cuf ni Julius mtatiro. Akiwezeshwa kifadha, anaweza kuamsha hamasa za watu kujiunga cuf. Vilevile atafuta dhana ya cuf ni chama cha waislamu.


e). hakuna asiejua hali na mpasuko wa kisiasa ulivyokua visiwani kati ya ccm na cuf. ilifikia waamue kuungana ili kusitisha tofauti zinazo irudisha nyuma znz. ni jambo zuri lkn chdm wamelitumia kwa kuisulubu cuf. wanaiita ccm B. si kweli kuwa cuf ni ccm b lkn kisiasa chdm wanahaki ya kusema hivyo. cuf wanadai kuwa vile wamo serikalini, 2015 watachukua znz. hawatoibiwa kura tena. yetu macho!


vyama vya nccr, tlp, udp nk....... havifanyi vizuri sn. inasemekana kuwa ushindi wa nccr kigoma ni kutokana na mgombea wao urais wa 2010, mzee hshim rungwe kuwa mwenyeji wa kigoma. walimpa kura za "tusimuangushe mtoto wetu...". mrema kwishnei, cheyo yupoyupo........



KWELI CCM ITANG'OKA 2015?
jibu la haraka ni kuwaHAPANA. pana uwezekano mkubwa wa ccm kushinda. kwa nn nasema hivi?

1- ccm wanauzoefu wa kumpitisha mgombea na tofauti zao zikaisha. rasharasha huwepo lkn huwa chache sn!
2- vijijini bado wana imani kubwa na ccm na hata baadhi ya miji.
3- tofauti za safu ya juu ya chadema zinaweza kukipa zilzala (mtikisiko) kipindi cha uchaguzi wa mwenyekiti na mgombea urais. Hii itakua neema kwa ccm.
4- propaganda za ukanda na udini zimekua mwiba kooni mwa chadema. hakikubaliki sn kwa waislamu. anae bisha apitie matokeo ya uchaguzi wa 2010 ktk tovuti ya NEC. Ataona chdm ilivyofanya ktk maeneo yenye waislamu wengi nchini.
5- cuf imekuwa ikiiharibia chadema. uwepo wa cuf ni kihunzi kwa chadema. na hivi sasa uadui bungeni wa cuf na chdm ni mkubwa. Cuf itaendelea kupunguza kura za chdm.
6- ili ccm ifanye vizuri, pana uwezekano ikakubaliana kuwapa cuf znz ili wanacuf wa bara wote waipigie ccm. Mpango huu unaweza kuinufaisha ccm huku bara. Ktk siasa lolote linawezekana. WANASIASA NI WANAHARAMU SANA! (ashakum…!)
7- siyo siri uchaguzi wa 2010 ulitawaliwa na udini (anaekataa hili atakua na matatizo). ccm ilikua na mgombea muislamu. cuf ilikua na mgombea muislamu. chdm ilikua na mgombea mkristo. wakristo wengi walipeleka kura zao chdm. kura za waislamu wengi zilikwenda ccm na cuf. mwaka 2015, pana uwezekano mkubwa ccm watampitisha mkristo. hali hii itapunguza kura za chadema. maaskofu ambao walikuwa upande wa chdm, wakiona mgombea mkristo ccm, bila shaka watahama na wafuasi wao kwenda upande wa ccm.
Ikumbukwe kuwa ccm inajua KULA VIZURI na viongozi wa dini!

Bado hakujakucha! Shuka bado lina umuhimu kutokana na baridi iliyopo.
Ili chama kifanye vizuri 2015, kizingatie ushauri wangu. kusema ccm inaweza shinda 2015, hayo ni maoni yangu binafsi! hata ccm inaweza kuangushwa vile ktk siasa lolote linawezekana!

nimeandika makala haya kwa kutanguliza uzalendo mbele!
Wakatabahu: wakuziba (mzee wa maneno yanayochoma nyoyo)
 
umeeleza mambo mengi lakini nitakubaliana na kwa mtazamo wa sasa cdm kinaonekana ni chama mbadala lakini je kimejitayarisha kuwa chama mbadala.Naishauri iwe na makada ambao wanaelewa chama chao nini sera ya chama na malengo ya chama kusema inapigana na ufisadi haitoshi kuwashawishi watanzania kukipa dhamana lakini kuna hili kama la kupinga ufisadi na bado ukawa na kiongozi ambaye ni wakili wa mafisadi hiyo ni moja ya silaha kubwa wanayotumia ccm hasa maeneo ya vijijini kuonyesha kuwa cdm si kweli wapinga ufisadi na pia wanachanganya watu namana gani wanaweza kuongoza nchi na kutenganisha maslahi binafsi.kuna hili la cdm kuwa na mahusiano na vyama vya republican na conservative vyama hivi vinajulikana kama vyama ambavyo wafuasi wake wengi ni watu wa matajiri na pia havijari watu maskini cdm lazima ijue watanzania wengi ni maskini na sababu kubwa ya ccm kukosa mvuto ni kutokana na kuwakumbatia matajiri wachache na kunyanyasa wanyonge lazima cdm ije na maelezo ya kuridhisha ni sababu gani zimewafanya kuwa na mahusiano na vyama hivyo.Pia kuna tukio la juzi la kamati ya mambo ya nje kutembelea balozi za ulaya na asia wakati wa bajeti miongoni mwa wajumbe wa kamati ni wabunge wa cdm lakini chamam halijaonyesha makali yake kwani tulitegemea wabunge hao wangekuwepo kipindi cha bajeti kuchangia hoja mbalimbali hii inatupa mashaka kama cdm itakuwa madarakani itapoteza udhibiti wa wabunge wake kama tunavyoona sasa hivi wabunge wakiweka mbele madai ya kuongezewa posho,kuwa wajumbe wa bodi pia waangalie uteuzi wa wabunge wa vit maalumu wawaige ccm ambao wanataka kuwepo na ukomo kuna wabunge wana zaidi ya vipindi viwili naa bado hawajaonyesha nia ya kugombea mpaka sasa na upuuzi mwingine naamini cdm kama watajipanga vizuri wana nafasi kubwa ya kuchukua dhamana ya nchi
 
kaka nakubaliana nawe mambo mengi sana na machache tunayotofautiana hayatowi zana kamili ya ushindi wa ccm 2015.na mwisho swali langu kwa hivi vyama vya upinzani,ni kweli vinalengo la kumsaidia Mtanzania au kunajambo zaidi ya hapo. Kwani lengo kama ni jema mbona njia hazionyeshi amani umoja na mshikamano,mbona lugha zinazotumika hazionyeshi ukomavu wa siasa.CCM inanafasi tena kubwa tu na si muda haya maneno yatatimia.
 
The way the cookie crumbles
Ukitaka mega kidogo pande kubwa lakatika,
Ukitaka mega kubwa kajipande,
Ukikata mega katikati waambulia chenga.
 
Umechambua vizuri,walau hapa umeepuka kuegemea sana upande ulee,lakini makosa yanayofanywa na ccm na serikali yake ni zaidi ya ulivyoyaainisha wewe,hata hivyo hujataka kuelezea ukweli mchungu kwa ccm kuhusu mgawanyiko mkubwa wa ndani, na uhasama/visasi vya kimakundi na sio kwa kigezo cha udini.pia kushindikana kutekelezwa kwa zaidi ya robo tatu ya ahadi za mwenyekiti wa ccm Jk is yet another blow ukiachia mbali kibarua walichonacho kama serikali kujinasua na kashfa za kufisadi raslimali za nchi hii. Kazi bado saana kwa chama tawala mkuu. Kashfa za kuundwa dhidi ya viongozi wa CDM as individuals hazitakuwa na nafasi vichwani mwa watanzania wa leo! LET'S WAIT AND SEE!
 
1]chadema wanabidi waanze kwenda vijijini kutafuta kura za 2015. huu ufisadi kwa asilimia kubwa tunaujua sisi huku mjini tu, huko vijijini watu hawana internet na tv wala magazeti yenye uchungu kama mwanahalisi ayafiki huko.. wenyewe wanasubiri pilau na vitenge

2] chadema wanabidi watoe image ya wao ni watu kaskazini. hii ni mbaya kwasababu watanzania wengi wanaona hivyo. ccm pamoja na ufisadi wao lakini hawana image kama hiyo.

3] chadema wanaonekana kama ni chama cha dini moja. tanzania ni nchi yenye watu wa dini zaidi ya moja. sasa ukiwa na chama ambacho kinaoneka kipo upande mmoja watu wa dini zingine wanakua hawawaelewi vizuri.

4] chadema wanazugumzia ufisadi wa ccm vizuri. lakini tunataka kusikia wenyewe watapambana kivipi na njia gani watatumia mfano raisi wa zambia alikua wanawaambia wananchi wake jinsi akavyo pambana na ufisadi

5] chadema waanze kutuambia watawasaidiaje wakulima ambao ndo asilimia 75% ya watanzania.. zamani bibi yangu aliwasomesha [kenya] mama yangu na kaka zake wote kwa kulima tumbaku. siku hizi mambo kama haya hayapo tena.

6]Elimu imeshuka sanaa miaka ya siku hizi. chadema wanamipango ipi ya kuboresha elimu. kuna jamaa yangu aliniambia kuna wanafunzi wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika.. nilisikia dr. slaa anasema elimu inaweza kutolewa bure. sasa Kwa huyu mwanafunzi ambaye hajui kusoma wala kuandika haitamsaidia chochote

7]tanzania tuna madini na raslimali yingi lakini bado ni nchi maskini. sasa chadema wanamipango gani kutumia hizi raslimali zetu kuendeleza nchi yetu..

8] tanzania tuna matatizo ya umeme na maji. tanesco imekufa kabisaa chadema watuammbie wata solve vp haya matatizo.. tunasikia ufisadi wa tanesco tu lakini hatujasikia plan za kusolve hii ishu ya umeme na maji

kuna mambo mengine mengi... mnaweza kushare
 
Back
Top Bottom