Ushauri wa bure kwa ccm

MAKUNDA

Senior Member
Apr 5, 2012
115
39
Hakuna asiyejua kuwa CCM imekuwa ikiingiza mkono wake katika maamuzi ya mahakama hasa katika kesi za kupinga matokeo ya Ubunge. Sasa ushauri ninaotaka kuwapa ni kuwa ni bora mwingilie kwa kuomba kila mlikopinga matokeo mshindwe kesi ili kuhepuka uchaguzi mdogo. Hata kule Arusha muombe rufaa ya CDM ipite na Kamanda G.L aendelee na ubunge wake. Kwanini natoa ushauri huu?
Ukweli ni kuwa kila uchaguzi mdogo utakaofanyika CCM itashindwa tu na huu ni ukweli usiopingika. Na katika trend ya kushindwa katika chaguzi ndogo mjue ndiyo Chama kitazidi kuporomoka na kujenga mazingira ya kushindwa 2015. Someni alama za nyakati na kutumia busara ndogo. Hii haiitaji shule kutambua. Makamanda wako juu kila mtakapoweka mguu ni mweleka. Mimi siyo mtabiri wa nyota bali busara ya kawaida inanionyesha hivyo.
 
Broda MAKUNDA,
Sikio la kufa halisikii dawa!
Ni mpango wa Mungu kuwa ccm ife kwa mtindo huo wa ubishi, na watafitiniana bila kugundua kitu, hatimaye tutapita kuitazama CCm sura ya mwisho pale Dodoma kaburini, tutatupia udongo wa kwaheri!
Regime mpya itaanza!
Hadithi mwisho!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom