Ushauri wa bure kwa ccm kuhusu maandamano ya chadema...

Mazee

Senior Member
Dec 6, 2007
128
24
Ninawashauri ccm na wale wanazi wa ccm kuacha kupiga kelele na badala yake na wao waandamane kushawishi wananchi na kuhamasisha katika hoja zao ambazo wao wanaziona kuwa zinafaa kama cdm wanavyofanya by the way falsafa ya cdm imekuwa ni nguvu ya umma kabla ya matukio ya afrika magharibi hayajaanza kutokea hivyo jamani acheni ugomvi na uzabizabina nyie ccm... Na nyie andamaneni na mfanye mikutano ya hadhara ....wananchi watajaa zaidi ya cdm...
 
Mkuu nani ataenda kwenye Maandamano ya Kifisadi au kutetea ufisadi? Kama ccm wanataka kuandamana waandame ila wasitegeme kuwa watu watawaunga mkono katika hayo maandamano yao labda wanaonufaika na Ufisadi. Unawachuuza mkuu, wakiandamana haki ya mtu hawatopata watanzania wa hayo maandamano kwa jinsi watz wanavyoichukia ccm mimi wala sisemi sana watoke waingie mitaani ndio watajua jinsi watu wanavyoichukia hiyo CCM a.K.a Chama Chama Madowans
 
..hakuna ulazima wa CCM kuandamana.

..CCM na SERIKALI yake wahakikishe wanazifanyia kazi tuhuma zinazoelekezwa kwao na CDM.

..tuhuma hizo ni kama kupanda kwa gharama za maisha, bei kubwa za pembejeo, mikataba inayolitia hasara taifa, mfumo mbovu wa afya na elimu, miundo mbinu mibovu etc etc.

.CCM wakitatua kero nilizozieleza hapo juu, na zaidi wakasitisha UFISADI na WIZI WA RASILIMALI ZA TAIFA, basi CDM hawatakuwa na hoja zinazowateka wananchi.

NB:

..mtaji wa CDM udhaifu na kukosa maono kwa Kikwete, pamoja na ufisadi wa CCM.
 
Na shauri wana CCM wa andamane kumuomba msajili wa vyama vya siasa akifute hiki chama kwani ni cha kishetani na tena kinaweza kumpiku shetani nafasi yake katika uovu.
 
mkuu nani ataenda kwenye maandamano ya kifisadi au kutetea ufisadi? Kama ccm wanataka kuandamana waandame ila wasitegeme kuwa watu watawaunga mkono katika hayo maandamano yao labda wanaonufaika na ufisadi. Unawachuuza mkuu, wakiandamana haki ya mtu hawatopata watanzania wa hayo maandamano kwa jinsi watz wanavyoichukia ccm mimi wala sisemi sana watoke waingie mitaani ndio watajua jinsi watu wanavyoichukia hiyo ccm a.k.a chama chama madowans

nimekupata mkulu lakini hawa jamaaa wanajigamba bado kuwa wao ndio chama kikubwa na kinachokubaliwa na watanzania wengi uthinitisho ni wao kupewa dola miezi mitatu iliyopita hivyo bila shaka wanao wengi tu wanaowahusudu ni ngumu kuwapoteza kwa kipindi cha miezi mitatu tu......

Ila tu waangali wasijewakaishia kuchakachua mali za umma kwa kuwakusanya wananchi na magari kuwapa t-shirt pia posho ili tu wajaze mihadhara yao hiyo...
 
na shauri wana ccm wa andamane kumuomba msajili wa vyama vya siasa akifute hiki chama kwani ni cha kishetani na tena kinaweza kumpiku shetani nafasi yake katika uovu.

chama cha kishetani wakati ktb mkuu wao anasema hawajaua hata mende!!!!!!!!!!!!!!
 
Haya maandamano ya CDM yamebadirisha kabisa mfumo wa siasa hapa nchini; kabla ya maandamano haya bunge ndilo lilikuwa muhimili wa siasa hapa nchini. Hivyo serikali ilipokuwa inataka jambo fulani lifanyike inadhibiti bunge. Hivi sasa mambo ni tofauti, serikali inapotumia wingi wa wabunge wake katika bunge kuidhibiti CDM bungeni, inajikuta imekwama kutokana na huu utaratibu mpya wa CDM wa kupeleka hoja zake moja kwa moja kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom